Manchester CityArsenalMancity-

Heka heka za Ligi Kuu ya England zinaendelea kurindima siku ya kesho. Stori kubwa zaidi ni mchezo baina ya klabu mabingwa watarajiwa ambao ni kati ya Manchester City na Arsenal ambao wataonyeshana kazi kwenye dimba la Etihad.

Mwenendo wa timu hizi mbili umekuwa wa ushindani msimu huu ukichagizwa na kutokufanya vizuri kwa washindani wengine walio zoeleka kama Liverpool, Chelsea,Tottenham Hotspurs na Chelsea ambazo zimeachwa mbali angalau Manchester United ikijaribu lakini hadi sasa wameonekana kuishiwa pumzi hivyo Man City na Arsenal ndizo ambazo zinafukuzia ubingwa uliopo mezani.

Ukiutazama msimamo wa EPL,Arsenal wapo kileleni wakiwa na alama 74,Man City wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 70 ,Manchester United wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 59 ,Newcastle United wapo nafasi ya 5 wakiwa na alama 56,Tottenham Hotspurs wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 53 wakati Liverpool wapo nafasi ya 8 wakiwa na alama 47 wakizidiwa na Aston Villa na Brighton&Hove Albion na zilizo juu yake chache.

Takwimu hizi zinadhihirisha kwamba Man City na Arsenal zipo kwenye mbio zao wakati Man United,Spurs,Newcastle United,Aston Villa,Brighton na Liverpool nao wapo katika mbio zao za kuwania nafasi 2 ili kukamilisha safu ya timu 4 zitakazoiwakilisha England kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

Arsenal na Man City ndizo timu zenye wastani mzuri wa mechi za kushinda, sare, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tofauti na Klabu nyingine.

Katika michezo 31 ambayo Arsenal imecheza msimu huu wa EPL wameshinda michezo 23, sare 5, wamepoteza mechi 3, wamefunga mabao 74 na kufungwa mabao 31 wanazo alama 74 wakati Man City waliocheza michezo 30, wameshinda 22, sare 4, wamepoteza mara, wamefunga mabao 78 na kuruhusu mabao 28 na wana alama 70 kibindoni wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa takwimu hizo inatosha kuonyesha kwamba wawili hawa wapo katika anga yao,na mchezo watakaokutana unaweza kutoa picha halisi je ni Arsenal waliokamata usukani kwa muda mrefu au mabingwa watetezi Manchester City ambao wanawania kutwaa taji kwa msimu wa tatu mfululizo.

Kiwango cha hivi karibuni,Manchester City wameshinda mechi 5 kati ya 6 za mwisho katika mashindano yote,wamefunga mabao 21,wanao wastani wa kufunga mabao 3.50 katika kila mchezo na hawajapoteza mechi wakati Arsenal nao wameshinda mechi 3 na sare 3 katika michezo 6,wamefunga mabao 16 ambayo ni wastani wa 2.67 katika kila mchezo ,tafsiri yake zinakutana timu ambazo hazijapoteza katika michezo iliyopita.

Ndani ya msimu huu Manchester City imeshacheza jumla ya mechi 51, imeshinda michezo 37, sare michezo 9 na kupoteza mara 5 tu,wamefunga mabao 131 sawa na wastani wa 2.57 wakati Arsenal wamecheza michezo50,wameshinda wameshinda 50,sare 7 na wamepoteza mara 7,wamefunga mabao 114 ambayo ni wastani wa 2.28.

Tangu ianze kuitwa EPL,timu hizi zimekutana mara 22 ambapo Manchester City imeshinda mechi 14 na sare ikijitokeza mara 5.

Katika mechi 15 za mwisho,Manchester City imeshinda mara 14 ikiwemo ushindi wa mechi 7 mfululizo huku wakipoteza mara 1 tu dhidi ya Arsenal.

Rekodi ya muda wote inaonyesha kuwa Arsenal imeshinda mara nyingi zaidi (98) wakati Manchester City wakishinda mara 64 na sare ikijitokeza mara 45 kwenye mashindano yote.

Pep Guardiola anaendelea kutegemea ubora wa kikosi chake ukichagizwa na mshambuliaji matata Erling Braut Haaland ambaye amefunga bao 32 katika EPL huku wakiwa na Hat Trick 4 na ameshafikisha mabao 51 katika mashindano yote huku Kevin De Bruyne mwenye mabao 12 lakini akiwa ndiye kinara wa kutoa pasi za mabao katika EPL (15).

Upande wa Mikel Arteta silaha zake zilizombeba kwenye EPL msimu huu ni zile zile zikiongozwa na Gabriel Martinel bao 14, Bukayo Saka 12, Martin Odergaard bao 11 ambao kwa pamoja wamekuwa katika kiwango bora tangu msimu ulipoanza.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa mnamo Februari 15,2023 kwenye dimba la Emirate nyumbani kwa Th Gunners,Manchester City waliicharaza Arsenal bao 3-1 mabao ya Haaland aliyefunga mara mbili na Jack Grealish na matokeo hayo yaliipeleka kileleni mwa msimamo The Citizen hivyo mechi hii ya marudiano ni ya kisasi.

Manchester CityIwapo Manchester City itashinda itafikisha alama 73, tofauti ya alama 1 na Arsenal lakini vijana wa Pep Guardiola watakuwa na faida ya mchezo mmoja mkononi lakini iwapo The Gunners watashinda wataongeza tofauti ya alama dhidi ya Manchester City na kupunguza shinikizo zikiwa zimesalia mechi chache msimu kumalizika.

Ikumbukwe kwenye ratiba ya kumalizia msimu Arsenal bado wana wapinzani wagumu kama Chelsea na Tottenham Hotspurs (Derby) na Newcastle United ambazo zote hizi bado zinaisaka nne bora.

The Gunners wapo kwenye ndoto yao ya muda mrefu ambayo wanatamani itimie ya kutwaa Ubingwa wa kwanza baada ya kuukosa kwa miaka mingi (Mara ya mwisho ilikuwa 2003).

Tunakusogezea takwimu katika makala hizi ili zikusaidie katika kufanya uchambuzi na kukuongezea uwanja mpana wa kutabiri michezo kupitia Sportpesa.

Mechi tayari ipo kwenye tovuti yetu. Tembelea sportpesa.co.tz, au pakua App ya SportPesa au piga *150*87#.

Share this: