- Simba SC vs Yanga SC zote zimepenya hatua ya 32 bora kwa ushindi mnono.
- Azam FC 1-0 Endumenti FC Landry Zouzou mfungaji pekee wa goli la ushindi.
- KMC FC vs Azam FC ni kituo kinachofuata NBC Premier League
- Matokeo ya mechi zote tumekusogezea hapa
Azam FC 1-0 Endumenti FC ni matokeo mchezo wa hatua ya 64 bora CRDB Federation Cup. Goli pekee lilifungwa na Landry Zouzou dakika ya 48 kwa mkwaju wa penati. Hiyo ni baada ya dakika 45 za mwanzo ngoma kuwa 0-0.
SOMA HII: Azam FC yaivuruga Simba SC yaifunga mara mbili mfululizo/ Kariakoo Dabi hakuna tena
Vuna mamilioni sasa hivi kwa kupaisha Kindege
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Azam FC 1-0 Endumenti FC, vigogo wapenya 32 bora

Ushindi wa Azam FC 1-0 Endumenti FC unaongeza idadi ya vigogo waliopenya 32 CRDB Federation Cup. Simba SC ilianza kufungua njia kisha Yanga SC wakafuata. Azam FC kete yao usiku saa tatu Februari 19 iliwapa tikete kusonga hatua inayofuata.
Ikumbukwe kwamba bingwa mtetezi ni Yanga SC. Kila hatua ni fainali kwa kuwa ukipoteza safari yako inaishia hapo. Baada ya ushindi Azam FC inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya KMC FC.
KMC vs Azam FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex. Februari 22,2026 saa 10:15 jioni. Wakusanya ushuru waliishia hatua ya 64 bora kwa kufungashiwa virago na Bandari FC wakiwa nyumbani.
Matokeo ya 64 bora Februari 18,2026

| Yanga SC | 2 | 0 | Cosmopolitan FC |
| JKT Tanzania | 7 | 0 | Pan African |
| Kagera Sugar | 3 | 0 | Mighty Elephan |
| Geita Gold | 1 | 0 | Kajuna FC |
| B19 FC | 7 | 0 | Dhujao FC |
| Barberian FC | 1 | 1 | Kijiwe Nongwa FC (Pen: 2-4) |
| Songea United | 2 | 1 | Vijana SC |
| Bigman FC | 0 | 1 | Nyika FC |
| Hausang FC | 2 | 1 | West Sengers |
| Stand United | 4 | 0 | Mabao FC |
| African Sports | 4 | 1 | Kilimo FC |
| Mtibwa Sugar | 5 | 0 | IAA SC |
| Pamba Jiji | 0 | 1 | Alliance FC (Pen: 4-2) |
| Mashujaa FC | 1 | 0 | Nkim FC |
| Mbuni FC | 5 | 1 | 1 Green FC |
Polisi Tanzania vs THB FC (Polisi wamepewa ushindi baada ya THB kutofika uwanjani)
SOMA HII: Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC | Rekodi zake na tuzo

Matokeo ya mechi hatua ya 64 bora Februari 17, 2026

| Simba SC | 3 | 0 | 0 Greenland FC |
| KMC FC | 3 | 3 (P 2-3) | Bandari FC |
| Coastal Union | 3 | 1 | Nyumbu FC |
| Fountain Gate | 1 | 0 | Mapinduzi FC |
| Dodoma Jiji FC | 3 | 1 | Kilimanjaro Wonders |
| Transit Camp | 4 | 0 | Chama la Wana |
Mbeya City vs Biashara United Mara
Biashara United hawakufika uwanjani. Mbeya City walifika na kufuata taratibu zote. Baada ya dakika 30 mwamuzi akamaliza mchezo kwa kuwapa Mbeya City ushindi wa kanuni.
Hitimisho
Azam FC 1-0 Endumenti FC yamefungua ukurasa unaofuata kwa matajiri hao wa Dar. Kituo kinachofuata ni NBC Premier League ugenini Februari 22,2026 Uwanja wa KMC Complex. Wakusanya mapato ya Kinondoni 2025/26 bado hawajawa imara kutokana na matokeo mabaya wanayopata. Je watafanya maajabu mbele ya Azam FC? Dakika 90 zitaamua.

