Tottenham vs ManUManUTottenham

Patashika ya Ligi Kuu ya England itaendelea kwa mchezo kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Manchester United utakaopigwa kwenye dimba la Tottenham mnamo April 27,2023.

Mchezo huu ni vita ya kuwania kumaliza ndani ya nne bora ili kujihakikishia tiketi ya kucheza michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao. Sisi kama Sportpesa blog tunakuletea uchambuzi wa mechi hii.

Hadi kufikia sasa, Spurs waliocheza michezo miwili zaidi ya United (30) wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo wakiwa na alama 53 wakati The Red Devils wenye alama 59 wapo nafasi ya 4 baada ya michezo 30.

Juu ya wapinzani hawa,wapo Newcastle United waliocheza michezo 31 na wamekusanya alama sawa na Man United(59) lakini wana wastani mzuri wa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa (29) wakati Red Devils wana (9).

Takwimu hizo zina tafsiri pana juu ya mchezo huu kwani iwapo Spurs itashinda itaikimbia Aston Villa yenye alama 51 na kuisogelea Man United na itabakisha tofauti ya alama 3 lakini ushindi kwa Man United utawafanya wafikishe alama 62 na wataishusha Newcastle United wenye alama 59 na hapo watakuwa na idadi sawa ya michezo.

Sare baina ya wababe hawa wawili itatoa faida kwa Newcastle United ambao watashuka hadi nafasi ya 4 lakini tofauti kati yao na Man United itakuwa ni alama moja pekee.

Sare hiyo pia, itazisaidia timu za Aston Villa na Liverpool kuendelea kuzifanya nafasi hizo mbili kuwa ngumu kwa timu zote zilizopo kuanzia nafasi ya 3 katika msimamo ikizingatiwa Arsenal na Man City wana uhakika wa kumaliza kwenye nafasi mbili za juu.

Kuelekea mchezo huu,Tottenham Hotspurs inapitia mgorogoro kutokana na matokeo mabovu wanayoendelea kuyapata katika Ligi hiyo na tangu iondokewe na aliyekuwa Kocha Mkuu wao Antonio Conte, vijana hao wa Daniel Levy wameshinda mechi moja pekee kati ya mechi sita walizocheza katika EPL.

Walishinda dhidi ya Brighton &Hove Albion lakini baada ya hapo wamepata sare na kupoteza kikiwemo kipigo kizito cha wikiendi iliyopita dhidi ya Newcastle United cha bao 6-1 jambo linalowafanya waelekee katika mchezo huu mkubwa wakiwa na hofu ya kiwango kibovu cha wachezaji wao.


Ikumbukwe baada ya kuikabili Manchester United,Tottenham Hotspurs watakuwa na kimbembe dhidi ya Liverpool katika mchezo utakaofuata.

Wanakutana na Man United ambayo licha ya kushinda dhidi ya Brighton&Hove Albion katika nusu fainali ya FA,lakini nao ni kama wamezinduka baada ya kupoteza nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ulaya waliponyukwa na Sevilla kwa jumla ya bao 5-2.

Hivi karibuni Kocha Eric Ten Haag aling’aka kwa kusema haitokubalika kuona wachezaji wake wanashindwa kujitoa kwa ubora na viwango vinavyostahili na wanapaswa kuwajibika jambo ambalo ni ishara ya kuamsha morali kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hizi mbili kwenye mashindano yote, Spurs imeshinda mara moja,sare mbili na kupoteza mara mbili wakati Man United wameshinda mara tatu ,sare moja na kupoteza moja hivyo inaonyesha wenyeji wa mchezo huu hawana mwenendo mzuri .

Spurs na United hawajatofautiana sana kwa takwimu kwenye michezo ya EPL msimu huu, wenyeji wamecheza mechi 32, wameshinda mara 16, sare 5, wamepoteza mara 11wamefunga bao 58 na kuruhusu bao 51 wakati wageni katika michezo 30 wameshinda 18, sare 5, wamepoteza mechi 7, wamefunga mabao 46 na kuruhusu bao 37.

Tottenham vs Man UHistoria inaonyesha kuwa Katika Ligi Kuu ya England, Manchester United na Tottenham Hotspurs zimekutana mara 28, The Red Devils imeshinda mara 16 wakati Spurs imeshinda mara 7 na sare mara 5.

Tottenham Hotspurs imepoteza mechi nne za mwisho za EPL dhidi ya Man United na mara ya mwisho kupoteza mechi nyingi mfululizo dhidi ya Red Devils ilikuwa kati ya Septemba 2001 hadi Septemba 200(mechi 7).

Vilevile Spurs imeshinda mechi tatu pekee kati ya ishirini na moja za mwisho kwenye EPL dhidi ya Manchester United katika uwanja wake wa nyumbani na ushindi huo wa michezo mitatu mfululizo waliupata kati ya April 2016 hadi Januari 2018.

Hakuna timu ambayo Manchester United imeifunga mechi nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu kama Tottenham Hotspurs (39).

Harry Kane amefunga bao 29 katika EPL kwenye uwanja wa nyumbani wa Spurs,na amfunga mabao matano dhidi ya Manchester United ila ni moja tu ndilo alilowafunga katika dimba la nyumbani zamani ikijulikana kama White Hat Lane mnamo Mei,2017.

Japokuwa alifunga mabao 10 ndani ya mechi 10 za EPL baada ya fainali za Kombe la Dunia, mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford amefunga mara moja tu katika mechi tano zilizopita.

Kwa wale wanaopenda kubashiria mechi hii watembelee tovuti yetu Sportpesa.co.tz au wapige *150*87#

 

 

Share this: