Benfica vs FC PortoBenfica- -

Klabu ya soka ya Benfica kesho wanawakaribisha timu ya Porto, katika mchezo wa ligi ya Primiera Liga, unaotarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana na namna timu zote mbili zinavyohitaji matokeo ili ziweze kumaliza kileleni.

Benfica ambao ndio vinara wa Ligi Kuu ya Ureno wakiwa na alama 71 itakuwa nyumbani kwao Estadio da Luz kuumana na mabingwa watetezi wa msimu ulioip FC Porto ambao wapo nafasi ya pili katika msimamo wakiwa na alama 61.

Benfica wapo katika kiwango bora hivi sasa ambapo katika mechi 5 za mwisho za Ligi wameshinda zote wakati FC Porto wao wameshinda mechi 3 na sare 2.

Mechi ya mwisho kwa Benfica kucheza dhidi ya Porto ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi, ambapo timu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Lisboa.

Katika mechi hiyo ambayo Porto alifungwa goli moja kwa bila na Benfica, mchezaji Rafa Silva ndiye aliyepeleka kilio kwa timu ya Porto baada ya kufunga goli akiwa amepokea pasi toka kwa David Nerez.

Safari hii, timu hizi zinakutana zikiwa zinatofautiana kwa alama 10, na iwapo wenyeji watashinda,wataongeza wigo wa alama na kuwa 13 dhidi ya mabingwa watetezi wa msimu uliopita.

Kama FC Porto watafanikiwa kushinda mechi ya kesho, basi  watapunguza alama dhidi ya Benfica na zitasalia pointi 7. Na kama Porto itafanikiwa kupata sare, basi  yatakuwa matokeo mazuri kwa Benfica na ikumbukwe zitakuwa zimesalia mechi 9 kabla ya kumalizika kwa msimu huu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                

Licha ya ubora walionao Benfica kwa sasa, rekodi zinaonyesha wamepoteza mara 3 na kushinda mara 1 huku wakipata sare 1 katika mechi 5 za mwisho walizokutana na FC Porto na katika mechi 5 za mwisho hakuna mechi iliyomalizika bila ya bao kufungwa.

Kwa upande wa Porto wao wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya za matokeo dhidi ya Benfica, baada ya kupoteza mechi ya mwisho walipokutana katika mehi ya ligi Oktoba mwaka jana.

Benfica vs FC PortoSafari hii wanakutana wakati Porto ikiwa namba mbili katika msimamo wa ligi, nyuma ya Benfica ambao wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo. Hata hivyo Porto anaingia kwenye mechi hii dhidi ya Benfica akiwa na matokeo ya kuridhisha baada ya kucheza mechi dhidi ya timu ya Portimonese, goli lililofungwa na Fabio Cardoso, siku ya Jumapili, wikiendi iliyokwisha.

Na ili iweze kupata matokeo ambayo yataipa ushindi Porto itawategemea zaidi mchezaji wake wa kimataifa Mahdi Taremi ambaye ndiye kinara wa kupachika mabao katika Klabu hiyo, akiwa na jumla ya magoli (13), akifuatiwa na Wenderson Galeno mwenye mabao (8).

 Benfica nao wataingia uwanjani siku ya kesho wakiwategemea zaidi washambuliaji Joao Mario na Goncalo Ramos, ambapo kila mmoja amefunga bao 17.

Kuelekea mchezo huo kocha wa timu ya Benfica Rogers Schimidt amesema ana matumaini makubwa timu yake itachukua pointi zote tatu dhidi ya Porto na haoni ni kwa namna gani wanaweza wakacheza nao bila kuwafunga.

‘’Nafikiri mnafahamu ubora wat imu yangu na pia mnafahamu najua ubora wat imu tunayoenda kucheza nayo. Nionavyo mimi fomu yetu ya kimchezo ni nzuri sana kulinganisha na wapinzani wetu, hata hivyo na wao wanajitahidi kupambana ili angalau na wao wapunguze idadi ya pointi tulizowaacha katika msimamo wa ligi’’’.

Akimaliazia kocha scmidt anasema anajua pamoja na ubora wao, Porto nao watajaribu vya kutosha kupambana.

Naye kocha wa timu ya Porto Sergio Conceicao kwa upande wake anasema mechi ya kesho ni muendelezo wa mechi zenye umuhimu katika ligi ya Premiera Liga, na wao Porto kama mabingwa watetezi wanajua umuhimu wa kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo.

‘’Najua shauku ambayo ipo hata kwa wachezaji wangu juu ya mechi hii tunayoenda kucheza. Kwa ujumla hatuna fomu mbaya dhidi yao, lakini muda mwingine matokeo huja na bahati ambayo mtakuwa nayo muda mnapokuwa mko uwanjani mnacheza.

Tulipokutana mara ya mwisho mwaka jana, timu yangu ilipata kadi nyekundu hivyo kupelekea Benfica kupata ushindi ki ulaini. Natumai safari hii hawatopata bahati hiyo’’. Alisema

Share this: