El-Classico-El-Classico-

Ukiongelea mechi kubwa katika ulimwengu wa soka huwezi kuacha mechi ya Dabi ya El Clássico. Hii ni mechi inayokutanisha miamba wawili ya soka barani Ulaya, ambapo kila mmoja kwa wakati wake, ametengeneza ufalme ambao anatamba nao mpaka leo hii.

Hapa tunazungumzia Barcelona VS Real Madrid, mechi ya marudiano ya mchezo wa kombe la mfalme almaarufu kama ‘’Copa del Rey’’, katika hatua ya nusu fainali.

Mechi hii itapigwa katika uwanja wa Camp Nou pale jijini Barcelona, baada ya mechi ya kwanza kupigwa katika dimba la Santiago Bernabeu na Barcelona kushinda kwa goli moja bila majibu.

Kwa namna utamaduni wa mechi hizi ulivyo, mechi hii imebeba hamasa na shauku kwa wapenzi wa mchezo wa mpira wa miguu nchini Hispania.

Hii sio mechi inayotazamwa tu Uhispania, bali huwa inafuatiliwa na kutazamwa mubashara, kwa wastani, na zaidi ya watu milioni 500, ulimwenguni kote.

Kumbukumbu zinaonyesha upinzania wa jadi baina ya timu hizi mbili ulianza rasmi katika msimu wa Mwaka 1928/1929, baada ya chama cha soka cha mpira Uhispania La Liga kuanzishwa.  Unaweza ukashangazwa kidogo na umri wa upinzania huu ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 90.

Ikiwa ndio mechi ya pili tu kwenye ratiba, baada ya msimu wa ligi ya La Liga kuanza, Real Madrid ndio ilikuwa timu ya kwanza kushinda mechi ya El Classico baina ya mahasimu hao wawili, baada ya kuichapa Barcelona 2-1, katika uwanja wa Camp De Les Cortes, jijini Madrid.

Msimu wa Mwaka 1934/1935 ulitoa matokeo ya kihistoria ambayo yamebaki katika mioyo ya wapenda soka nchini Hispania. Katika msimu huo Barcelona aliichapa Real Madrid 5-0, katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi.

Real Madrid naye alilipa kisasi katika mechi ya marudiano kwa kuitandika Barcleona 8-2, katika mpambano ambao ulirudisha upya msisimko wa upinzani baina ya timu hizi mbili,moja ikitokea katika jimbo la Catalan na nyingine Madrilenos, ambayo leo inajulikana zaidi kama Madrid.

Kwa karibu kipindi chote cha miaka 5, tangu kuanzishwa kwa ligi ya La liga, timu ya Real Madrid, ndio ilikuwa bora, ikipata matokeo mazuri kila ilipokutana na Barcelona, hivyo kupelekea bodi ya timu ya Barcelona kukataa timu ya Real Madrid, isishiriki mashindano ya Campionat de Catalunya.

Barcelona vs Real MadridMashindano hayo ya Campionat Catalunya yaliandaliwa baada ya ligi ya La Liga na mashindano ya Campeonato Regional Centro kusimama, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyojuliakana kama ‘’The Spanish Civil War’’ kuibuka Mwaka 1936.

Ilichukua, takriban miaka mitatu na ushehe, kabla ya timu hizi mbili, kuja kukutana tena, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuisha na ligi ya La Liga kuanza tena katika msimu wa Mwaka 1939/1940.

Baada ya Real Madrid, kutawala ligi ya La Liga kwa miongo kadhaa, ikiwemo kuchukua mataji ya La Liga mfululizo. Baada ya kupita misimu ya miaka 1980, kuanzia misimu ya mwaka 1985, Real Madrid, ilichukua mataji ya La Liga mfululizo, mpaka msimu wa Mwaka 1990/91, ambapo timu ya Barcelona ilimwajiri Kocha Johan Cruyf

Ujio wa Johan Cruyf, sio tu uliua utawala wa Real Madrid katika ligi ya La Liga, bali pia ulifanya maajabu katika mashindano ya kimataifa, ambapo Barcelona waliweka historia muhimu, katika msimu wa mwaka 1992, walipoweza kuchukua kombe la Ulaya, baada ya kuichapa Sampdoria, katika uwanja wa Wembley.

Kitendo cha kuchukua kombe la ulaya, na baadae kuchukua kombe la La Liga mara mbili kilipelekea timu ya Barcelona kubatizwa jina la Dream Team. Utawala huu uliendelea, mpaka pale kocha Johan Cruyf alipoondoka Barcelona na ufalme kurudi Real Madrid, wakiongozwa na mchezaji Raul Gonzalez. Raul alichezea Real Madrid kwa mara ya kwanza mwaka 1994, na ilipofika mwaka 1997, Raul aliiongoza Madrid kutwaa taji la saba la Ulaya, ambalo kwa wakati huo lilianza kuitwa Champions League.

Real Madrid walirudia kupata mafanikio hayo katika msimu wa mwaka 1999/2000, kwa kutwaa taji la nane la Champions League.

Nitawarudisha nyuma kidogo katika historia ya mechi hizi za El Classico, katika msimu wa 1993/94 na 1994/95, mchezo wa El Classico baina ya mafahari hawa mawili, Barcleona aliitandika Real Madrid 5-0, katika uwanja wa Nou Camp.

Mchezo wao uliofuata ndio uliotoa tafsiri sahihi ya upinzani wao, na kwa nini mechi ya mafahari hawa ni El Classico. Real Madrid alilipa kisasi na kushinda 5-0, katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Historia kubwa zaidi ilitengenezwa kwenye msimu ya mwaka 2000. Mchezaji Luis Figo, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Barcelona, alipohamia Real Madrid, akisajiliwa na Rais wa wakati huo wa Real Madrid Florentino Perez, ambaye alitimiza ahadi yake wakati akifanya kampeni za kushika kiti cha urais wa timu ya Real Madrid.

Kwa msimu mmoja na nusu baada ya Luis Figo kusajiliwa na baadae David Beckham kujiunga na klabu hiyo, timu ya Real Madrid ilikuwa ya moto sana ikiwa pamoja nao Roberto Carlos na Zinedine Zidane, almaarufu kama Zizzou.

Ujio wa mchezaji Ronaldinho,  katika timu ya Barcelona, ulisambaratisha kwa muda ufalme wa Real Madrid, katika mashindano yote waliyoshiriki pamoja. Kwa kifupi dabi ya El Classico, imekuwa ikikolezwa na nyakati, kutegemeana na aina ya uongozi wa klabu, kocha na wachezaji.

Mathalani, baada ya kocha Pep Gurdiola, Lionel Messi, Iniesta, Xavi kuanza kuitumikia Barcelona kuanzia msimu wa mwaka 2008, ufalme wa soka ulihamia Barcelona.

Kifupi dabi ya El Classico baina ya mafahari hao ina historia ndefu, yenye mambo mengi naya kusisimua.

Ukiangalia vikosi vya timu zote mbili tukianza na Barcelona wao

Mechi nyingine zinazocheza siku ya kesho ni pamoja na 

Share this: