- Vita ya ubingwa inazidi kuwaka ndani ya NBC Premier League. Jumamosi hii ni zamu ya Yanga SC vs Tanzania Prisons. Mchezo huu muhimu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
- Diarra ‘out’, Damaro kimeeleweka; Pigo kubwa kwa Yanga SC kuelekea mchezo huu ni kumkosa kipa wao Djigui Diarra, huku Damaro jambo lake likimalizwa.
Vita ya ubingwa inazidi kuwaka ndani ya NBC Premier League. Baada ya Simba SC kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, Jumamosi hii ni zamu ya Yanga SC vs Tanzania Prisons. Mchezo huu muhimu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam. Pigo kubwa kwa Yanga SC kuelekea mchezo huu ni kumkosa kipa wao Djigui Diarra, huku Damaro jambo lake likimalizwa.
SOMA HII PIA: NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili | Azam FC vs Simba SC | Yanga SC vs Prisons | Msimamo
Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC vs Tanzania Prisons h2h

Rekodi zinaonyesha Yanga SC na Tanzania Prisons zimekutana katika michezo 28, ya mashindano tofauti. Yanga SC wamekuwa na rekodi bora dhidi ya wapinzani wao, hii ni baada ya kufanikiwa kuandikisha ushindi mara 20. Tanzania Prisons hawajawahi kuibuka na ushindi mbele ya Yanga SC, ambapo mechi 8 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare.
Kikosi cha Yanga SC kinachotarajia kuanza mchezo huu
Kuelekea katika mchezo huu Yanga SC itaendelea kukosa baadhi ya mastaa wao walio majeruhi. Pamoja na wachezaji walio majeruhi, wapo pia wanaotumikia adhabu za kadi na kufungiwa akiwemo kipa namba moja, Djigui Diarra. Kuendana na mazoezi ya mwisho ya leo Ijumaa Yanga SC wanatarajia kuanza na kikosi hiki;
Kipa: Hussein Masaranga
Walinzi: Mwenda, Baka, Mwamnyeto, Mohammed Hussein
Viungo: Duke, Pacome, Maxi, Damaro na Okello
Mshambuliaji: Depu
SOMA HII ZAIDI: Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, goal, statics
Taarifa ya benchi la ufundi Yanga SC kuhusu wachezaji walio majeruhi

Kuelekea mchezo huo, kocha mkuu wa Yanga Pedro amesema: “Tumekuwa na mazoezi mazuri ya kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons, akili zetu zinawaza kufanya vizuri tu. Tunajua nini tunataka, ni wazi kesho tunacheza na timu ngumu, tunakumbuka ugumu tuliopata katika kushinda mechi ya mzunguko wa kwanza.Licha ya hali hiyo, lakini tupo hapa kwaajili ya alama tatu na tuna imani tutazipata.
“Bado tunachangamoto kubwa ya majeruhi ya wachezaji wetu muhimu, mfano Job, Mzize na wengine, lakini timu nzima ina lengo la kupata matokeo mazuri. Hivyo kila mtu anafanya jitihada kubwa kutimiza malengo ya klabu. Tunawashukuru sana Wananchi kwa kuwa nasi katika kila hali, hasa baada ya ratiba yetu ngumu. Licha ya kuwa na matokeo ya kusuasua katika mechi kadhaa zilizopita, lakini mashabiki wetu hawajawahi kuwa nyuma, wanakuja kutupa sapoti.
“Licha ya majeruhi tulionao, tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa sana lakini wanaopaswa kuanza ni 11 pekee. Nafurahi kuwa wachezaji wote wana uelewa mkubwa kuhusu mawazo yetu na mbinu tunazowapa. Naamini kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuisaidia timu, naamini kesho itakuwa siku ngumu lakini nzuri kwasababu tumekuja kusaka ushindi”
Ishu ya Diarra na Damaro

Ikumbukwe, Diarra kupitia Kamati ya masaa 72 alikutwa na hatia ya utovu wa nidhamu mara baada ya mchezo wao na Mtibwa Sugar, ambapo kufuatia vitendo hivyo amefungiwa mechi 3 na kutozwa faini ya Shilingi Milioni 4 za Kitanzania. Hivyo kwake huu ni mchezo wa kwanza ambao atatumikia adhabu hiyo. Na ni wazi hili linatarajia kuwa pigo kubwa kwa Yanga SC kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akionyesha staa huyo.
Kuhusu Nyota wao mwingine Damaro yeye jambo lake limeisha vizuri kwa upande wake na Yanga, Taarifa iliyotolewa na TFF imethibitisha usajili wake na anatarajiwa kutumika bila changamoto nyingine. Hii ni baada ya kuwepo kwa shauri lililofunguliwa na Simba SC juu ya matumizi yake na ukamilifu wa vibali, mpaka kupelekea Yanga SC kuuita mchezo wao dhidi ya Simba Damaro Day. Nyota huyo ambaye alibadili uraia kutoka kuwa Mguinea kuwa Mtanzania, anatarajia kuanza kikosi cha kwanza.
SOMA HII PIA: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo, Takwimu na historia
Hitimisho na utabiri
Yanga SC vs Tanzania Prisons ni miongoni mwa michezo migumu ambayo haijawahi kutabirika, licha ya utawala wa muda mrefu wa Yanga SC kwenye matokeo. Mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao Yanga SC ilipata goli la dakika za mwisho unadhihirisha ushindani huu. Hata hivyo kukosekana kwa baadhi ya mastaa wa Yanga SC akiwemo kipa wao, Diarra inatarajiwa kuwa changamoto kubwa kwa Wananchi. Tusubiri dakika 90 zitatupa majibu, lakini ni wazi Yanga SC wana nafasi kubwa ya kushinda.

