skip to Main Content
HOROYA AC Vs VIPER’S -MECHI YA HESHIMA

HOROYA AC vs VIPER’S -MECHI YA HESHIMA

HOROYA AC ya nchini Guinea na Vipers ya Uganda zinatarajiwa kuvaana siku ya kesho, Ijumaa, Tarehe 31, Machi 2023, katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo wa kesho, unatafsiriwa kama wa kukamilisha ratiba, huku kukiwa na timu mbili za Raja Casablanca na Simba SC, ambazo ki msingi zimeshafuzu kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika, kwa ngazi ya klabu.

Timu ya Horoya na Vipers zote zipo katika Kundi, C ambalo Raja Casablanca wanaongoza katika msimamo wa kundi, wakiwa na pointi 13, Simba 9, Horoya 4 na Vipers 2.

Katika mchezo wa awali, uliochezwa wiki kadhaa zilizopita, matokeo yalimalizika kwa timu hizo mbili kutoka suluhu ya bila kufungana, Jijini Kampala na SportPesa wamekupa mechi hiyo ili uibashiri.

Mchezo huu wa marudiano unaopigwa kesho unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja Stade du 26 Mars, Bamako nchini Mali.

Michezo iliyopita- Horoya AC na Vipers.

Hapa tunakuwekea matokeo ya michezo mitano mfululizo waliyocheza Horoya katika hatua hii ya makundi, yapo hivi Simba 7-0 Horoya, Horoya 1-3 Raja Casablanca, Raja Casablanca 2-0 Horoya, Vipers 0-0 Horoya, Simba 0-1 Horoya.

Na michezo mitano ya Vipers waliyocheza katika hatua ya makundi ni pamoja na Vipers 1-1 Raja Casablanca, Vipers 0-1 Simba, Vipers 0-0 Horoya, Raja Casablanca 5-0 Vipers.

Katika mchezo wa kesho, timu zote mbili, yaani Horoya na Vipers zitataka kumaliza mechi za makundi, zikiwa zimeondoka na heshima, kwani inaeleweka ni namna gani timu zote zilikuwa na upinzani mkubwa katika mechi za ligi ya klabu bingwa msimu huu.

Horoya ACTimu zote mbili hazina cha kupoteza katika mchezo wa kesho, bali kwa kila timu kukamilisha ratiba, kwani Raja Casablanca na Simba tayari zimeshafuzu.

Kibarua kigumu zaidi kinatarajiwa kuwepo katika mchezo kati ya Raja Casablanca dhidi ya Simba ambazo zote tayari zimeshafuzu kundi hilo.

Katika mchezo huo, Simba watakuwa ugenini nchini Morocco, wakiingia uwanjani wakiwa na lengo moja pekee la kutaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar-Es-Salaam.

Kueleke mchezo huo, Horoya wenyewe wataingia uwanjani wakiwa na hasira ya kutoka kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Hivyo wataingia uwanjani kwa lengo moja la kurejesha imani ya mashabiki wao kufuatia kipigo cha mabao 7-0 walichokipata dhidi ya Simba.

Katika mchezo huo, Vipers wanatakiwa waingie kwa tahadhari kubwa, hasa hasa katika safu yao ya ulinzi kutokana na ubora wa safu ya ushambuliaji wa Horoya.

Vipers si wageni kwa Horoya, kazi ambayo wanaijua kwa ufanisi, ni ya kuwachunga viungo wawili wa Horoya ambao ndio tishio kwenye timu hiyo.

Viungo hao washambuliaji ni Pape Abdou Ndiaye, Sory Traore, Pape Abdou Ndiaye, Yakhouba Gnagna Barry, Daouda Camara, Alseny Soumah, Sekou Keita na Ocansey Mandela.

Wakati uimara na ubora wa safu ya kiungo na ushambuliaji wa Horoya unaeleweka, safu yao ya ulinzi itaongozwa na Ibrahima Doumbouya, Boubacar Samassekou, M´Bemba Camara, Lamine Fofana, Abou Mangué, Ibrahima Condé na Abou Mangué.

 Mabeki hao wote wana miili mikubwa ya kupambana na washambuliaji wa Vipers ambao wana fiziki huku wakicheza kwa kutumia nguvu nyingi, lakini ni watulivu wakiwa ndani ya 18.

Kwa upande wa Vipers wenyewe huenda wakamtumia mshambuliaji wao tegemeo, Milton Karisa ambaye yeye amekosa michezo kadhaa ya hatua ya makundi baada ya kupata maumivu ya misuli katika mchezo wa kwanza dhidi ya Simba uliochezwa Uganda ambaye alishindwa kumalizia pambano hilo.

Karisa ndiye mchezaji hatari wa kuchungwa kwa Vipers, hivyo mabeki wa Horoya hawatakiwi kufanya makosa ya kizembe mbele ya mshambuliaji huyo.

Pia Horoya wanatakiwa wamchunge mshambuliaji wa Vipers ambaye ni Yunus Sentamu mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti akiwa anakokota mpira akiwa anaelekea uelekeo wa goli la wapinzani.

SportPesa tayari imeshakuwekea mechi hii kwa ajili yako wewe mchezaji wetu kubashiri na kushinda mkwanja.

Share this:
Back To Top