Mbeya City vs Simba SC NBC Premier League kupigwa mchanaEllie Mpanzu
  • Uwanja wa Sokoine, Mbeya City vs Simba SC kupigwa saa 8 mchana NBC Premier League 2025/26 Juni 17.
  • Mbeya City amekutana na Simba SC mara moja kwenye ligi msimu huu Desemba 4,2025.
  • Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC amesema kuna mshtuko mkubwa kuhusu mabadiliko ya muda

Mchezo wa Mbeya City vs Simba SC kupigwa saa 8 mchana, NBC Premier League Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Awali mchezo huu ulitarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, umefanyiwa mabadiliko na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). Sababu kubwa imeelezwa kuwa ni masuala ya kiutendaji. Hivyo Juni 17, 2026 mnyama atakuwa ugenini kwa mara ya kwanza kwenye msimu akicheza mchana.

SOMA HII: Kikosi cha Simba SC kimerejea kambini rasmi | NBC Premier League na CRDB Federation Cup | SportPesa Blog

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Mbeya City vs Simba SC kupigwa saa 8 mchana mzunguko wa pili NBC Premier League

Mbeya City vs Simba SC NBC Premier League kupigwa saa 8
Mwalimu Seleman.

SOMA HII: Ratiba ya Simba SC mwezi huu wa 6, 2026 | Ligi Kuu NBC na CRDB Federation Cup, Takwimu |Mechi 6 za kufa na kupona | SportPesa Blog

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Ni Mbeya City vs Simba SC kupigwa saa 8 mchana kwenye mzunguko wa pili. Mchezo uliopita walipokutana Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo matokeo ilikuwa Simba SC 3-0 Mbeya City. Je ugenini wenyeji watakubali kupigwa na mnyama ama watalipa kisasi? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo ya hivi punde.

Msimamo wa Mbeya City na Simba SC

TimuNafasiMechiUshindiSareVipigoPointiMagoli KufungaMagoli Kufungwa
Simba SC2251771584510
Mbeya City14255713222039

Simba SC imekuwa na safu imara ya ulinzi ikifungwa magoli machache ambayo ni 10. Wenyeji Mbeya City wameruhusu jumla ya magoli 39 baada ya mechi 25. Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana walipoteza pointi 3 kwa kufungwa magoli 3.

H2H Mbeya City vs Simba SC

TareheTimu NyumbaniTimu WageniMatokeo
04/12/2025Simba SCMbeya City3-0
18/01/2023Simba SCMbeya City3-2
23/11/2022Mbeya CitySimba SC1-1
16/06/2022Simba SCMbeya City3-0
17/01/2022Mbeya CitySimba SC1-0
22/06/2021Simba SCMbeya City4-1
13/12/2020Mbeya CitySimba SC0-1
24/06/2020Mbeya CitySimba SC0-2

Mnayama ameandika rekodi bora mbele ya Mbeya City kwenye eneo la ufungaji wa magoli akifikisha 19. Mbeya City amefunga magoli 6. Ushindi mara 6, sare 1 na ikipoteza mara 1. Je mchezo ujao nani atakuwa mbabe?

Maoni ya Ahmed Ally kuhusu mechi ya saa 8 mchana

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema mara baada ya mabadiliko hayo kumekuwa na mshtuko. Ahmed ameongeza kuwa mashabiki wengi hawajazoea hali hiyo jambo linalowapa wasiwasi kuelekea kwenye mchezo huo. Amewaomba mashabiki wasiwe na mashaka kwa kuwa ni muda mzuri.

“Mara baada ya mabadiliko ya muda kwa kuwa awali mchezo ulitarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni kumekuwa na mshtuko kwa mashabiki. Ninawaomba mashabiki wasiwe na presha huu ni muda mzuri na mabadiliko tumeyapokea. Mbeya saa 8:00 hakuna jua kali na ukizingatia kwa sasa tunaingia msimu wa baridi.

“Ukienda Mbeya saa 8:00 kunakuwa hakuna jua kali. Mazingira yanaruhusu na tunafanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo. Hakuna sababu yakupata mshtuko, tunaamini tutakwenda kufanya kazi yetu kwa umakini mkubwa ukizingatia huu ni mzunguko wa pili,”.

SOMA HII: Ratiba na matokeo ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 | Takwimu, msimamo| SportPesa Blog

Hitimisho

Rekodi inakwenda kuandikwa Mbeya City vs Simba SC kupigwa saa 8 mchana 2025/26. Mnyama ratiba yake ilikuwa ni saa 10:00, saa 1:00 usiku, je atapata matokeo ya aina gani ugenini? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo ya hivi punde.

Share this: