skip to Main Content
HUKU GHANA VS ANGOLA, KULE RAJA VS SIMBA
Ghana

HUKU GHANA VS ANGOLA, KULE RAJA VS SIMBA

Mechi za kimataifa ndio hivyo zimerudi tena. Kuanzia siku ya Jumatano wiki hii, mpaka mwisho wa mwezi huu, viwanja vingi vya mpira vitakuwa vinashughuli za kimechezo za mechi za kimataifa kwenye hatua ya kufuzu iwe Africa ama Ulaya.

Leo tunakuangazia baadhi ya mechi ambazo zitachezwa kuanzia kesho kutwa. Mechi ya kwanza ambayo ninafikiri inahitaji kutupiwa jicho la karibu ni mechi kati ya Ghana dhidi ya Angola.

Timu hizi mbili, moja kutoka ukanda wa Magharibi wa bara la Afrika na nyingine inatoka katika ukanda wa kusini mwa Afrika.

Timu zote mbili zinajaribu kufanya vyema katika kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, huku Ghana ikipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu wao, katika ushiriki wa mashindano ya kimataifa.

Ghana inaingia kucheza mechi ya kimataifa ya kwanza baada ya kutoka katika mashindano ya kombe la Dunia Desemba 2022, ambapo timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi ikifanikiwa kushinda mechi moja dhidi ya Jamhuri ya Korea na kufungwa mechi mbili dhidi ya Ureno na Uruguay.

Kwa upande wa Angola wao wanaingia kwenye mechi hii wakiwa hawajacheza mechi za kiushindani kama Ghana lakini wakiwa walicheza mechi za kufuzu kucheza kombe la shirikisho la mpira wa miguu la Africa CHAN, ambalo ni maalum, kwa ajili ya wachezaji wanaocheza mechi za ligi ya nyumbani.

Kwa namna ambavyo ukitazama mwenendo wa matokeo waliyoyapata timu hii ya Taifa ya Angola, utaona kwamba, kwa mechi walizocheza tangu mwaka jana mwezi wa tisa dhidi ya Afrika Kusini ndio mechi yao kubwa ya ki ushindani waliyofanikiwa kuwa na matokeo ya kuridhisha wakiichapa Bafana Bafana magoli manne.

Mechi nyingine tatu walizocheza baada ya hapo zote ilikuwa ni za kufuzu kombe la CHAN kwa wachezaji wa ndani ambapo walishinda mechi moja tu dhidi ya Botswana, na kutoa sare mechi mbili, ambazo walicheza dhidi ya Mali na kupata sare ya (3-3) na mechi dhidi ya Mauritania ambayo walitoa sare ya bila bila.

Kwa namna uchambuzi huu unavyoonyesha itakuwa bahati kwa Angola kupata matokeo mazuri, ingawaje kwenye mpira chochote kinaweza kutokea.

Tukirudi kwenye mashindano ya CAF ngazi ya klabu, timu ya Simba ya Tanzania, yenyewe imeshafanikiwa kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa Africa, baada ya kuichapa timu ya Horoya kutoka Guinea kwa magoli (7-0).

Simba imelipa kisasi cha kufungwa na timu ya Horoya siku ya Jumamosi, baada ya kufungwa goli moja bila, Tarehe 24 Mwezi Februari 2023, katika mji mkuu wa Guinea, Conakry. Bao hilo lilifungwa na Pape Ndiaye (18) kwa kichwa, baada ya kucheza mpira wa kona uliopigwa na Amadou Wankoye.

Kwa matokeo hayo Simba, ambayo ipo kundi C, pamoja na Vipers, Raja na Horoya, sasa imesalia nafasi ya pili, ikiwa na pointi 9, nafasi ambayo ilikuwepo kabla ya mechi dhidi ya Horoya, na sasa imebakiza mechi moja ya kukamilisha ratiba dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa Tarehe 31 Machi 2023.

Raja kwa upande wao watamaliza mechi yao ya mwisho dhidi ya Simba, wakiwa tayari wanapointi 13, wakiongoza kundi baada ya kutoka sare na timu Vipers ya Uganda siku ya Jumamosi usiku, katika uwanja wa St marry’s Kitende.

Kwa ufupi mechi zinazoenda kuchezwa kuanzia siku ya Jumatano, nazungumzia Ghana VS Angola na Raja Casablanca VS Simba zitaonyesha ni kwa namna gani timu ya Angola, pamoja na Simba ambazo zote mbili zinaingia kwenye mechi zao kama vibonde (underdog) ukilinganisha na wapinzani wao zinavyoweza kubadili upepo wa ushindi kwa kuishangaza Africa na matokeo ya ushindi dhidi ya wapinzania wao.

Mechi hizi, yaani ya Ghana VS Angola, Raja Casablanca VS simba SC, na nyinginezo nyingi za ligi ambazo zitakuwa bado zinacheza katika nchi mbali mbali, zinatarajiwa kuwamo katika tovuti yetu kwa ajili ya wateja wetu kuzibashiria.

Kujisajili na kucheza tembelea Sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this:
Back To Top