skip to Main Content
Simba, Raja Nani Kuonyesha Ubabe?
Raja-VS-Simba

Simba, Raja nani kuonyesha ubabe?

JE SIMBA KULIPA KISASI KWA RAJA KESHO?

Kikosi cha timu ya soka ya Simba, kutoka Tanzania, tayari kimeshatua nchini Morocco kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya timu ya Raja Casablanca.

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa, siku ya kesho Machi 31-2023, kwenye Uwanja wa Mohamed V, jijini Casablanca.

Tayari inaeleweka mchezo huu ni wa kukamilisha ratiba, kwani timu zote mbili, tayari zimeshafuzu katika Kundi, C, huku Raja Casablanca, wakiongoza kama vinara wa kundi, wakiwa na pointi 13, Simba 9, Horoya 5 na Vipers 1.

Mchezo huu ni kipimo sahihi kwa Simba, kwani wanaingia uwanjani wakiwa na hasira za kutaka kulipa kisasi dhidi ya Raja Casablanca, ambao waliwafunga mabao 3-0 kwenye Uwanja mkuu wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba iliondoka Dar-Es-Salaam, juzi baada ya kumaliza kufanya mazoezi yake ya mwisho, kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju, kabla ya kuanza safari hiyo siku ya Jumanne jioni.

Wakati msafara huo ukiondoka, juzi jioni, nyota wake waliokuwepo katika kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichovaana na Uganda, wenyewe wameshaungana na wenzao   Jumatano huko Morocco.

Wachezaji hao ni pamoja na Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yasini, Mohammed Hussein na Shomari Kapombe ambao wamemaliza majukumu yao kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliocheza dhidi ya Uganda na kushindwa..

Wachezaji wengine wa kigeni wanaoicheza timu ya Simba, nazungumzia kina Clatous Chama, Peter Banda, Pape Osmane Sakho na Henock Inonga, tayari wameshajumuika na wenzao kutokea katika timu za mataifa mengine ya ki Afrika baada ya kumaliza majukumu yao.

Kuelekea mchezo huu, Simba inatarajiwa kuwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali ikwemo majeraha na kadi za njano.

Wachezaji hao ni pamoja na Mohamed Hussein (kadi njano), Jonas Mkude, Mohamed Mussa, Augustine Okrah, Jimmyson Mwanuke, na Ismail Sawadogo (majeruhi) na Mohamed Ouattara (mechi fitness).

Akizungumzia mchezo huu wa kesho, kiungo mshambuliaji wa Simba Mzambia Clatous Chama anasema kuwa licha ya kucheza vizuri na kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya, bado wana kiu ya kulipa kisasi baada ya kuchapwa goli tatu jijini Dar-es-Salaam.

‘’Mimi pamoja na wachezaji wenzangu tunahitaji kufanya vizuri zaidi dhidi ya Raja Casablanca, ili kwanza kurudisha heshima na pia kufikia malengo ya pointi na magoli tuliyojiwekea wakati tunaanza mashindano’’ Alisema Chama.

Simba SCAnaendelea kwa kusema kuwa anaamini katika michezo inayofuata, akimaanisha wa robo fainali,  timu ya Simba itakuwa imeimarika zaidi katika maeneo mbali mbali ikiwemo safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Kiungo huyo anaendelea kwa kusema kuwa walianza vibaya michuano hiyo, katika michezo ya hatua za awali, lakini kwa sasa kikosi chao kimebadilika, na kinacheza kitimu ikiwemo kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

“Kwa hatua tuliyofikia hivi sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano haya, malengo yetu yakiwa ni kucheza fainali.

“Nafikiri uliona mchezo wetu dhidi ya Horoya ulivyoenda, sasa hivi akili na nguvu zetu zote tunazielekeza kwenye mechi na mechi nyingine inayofuata. Kipekee naomba niwapongeze wapenzi na mashabiki wa Simba kwa mchango wao mkubwa, katika kutupa hamasa.

“Tunawaahidi kuwa kama wachezaji tutatimiza majukumu yetu ya kuipambania timu, ili tutimize malengo yetu ya kucheza nusu fainali au fainali,”.

Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Oliviera Roberto ‘Robertinho’ anaungumzia mchezo wa kesho kwa kusema kuwa “Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa timu ya Simba, licha ya kufuzu hatua ya robo fainali.

“Umuhimu wake ni kuutumia kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa robo fainali, hivyo tumepanga kuingia na kucheza kwa ari na mali ili kupata ushindi wa ki historia.

“Nitawatumia wachezaji wangu wote tegemeo katika mchezo wa kesho, licha ya kufuzu kwani bado tuna uhitaji wa pointi tatu,” anasema Robertinho.

Simba huenda ikakutana na timu hizi katika robo fainali ambazo ni JS Kabylie, Mamelodi Sundowns au Esperance ambazo zinaongoza katika makundi yao yenyewe ikiwa nafasi ya pili.

Mechi hii kati ya Raja VS Simba tayari ipo kwenye tovuti ya SportPesa.

Kucheza na kujiunga tembelea tovuti yetu Sportpesa.co.tz au piga*150*187#.

Share this:
Back To Top