Pacome ZouzouaPacome kazini
  • Kiungo Pacome Zouzoua amezaliwa 1997 ana umri wa miaka 29 ni raia wa Ivory Coast
  • Bado anacheza kikosi cha Yanga SC ni chaguo la kwanza eneo la viungo akiwa na uwezo wakufunga na kutengeneza asisti
  • Hapa tumekuletea rekodi za magoli, mechi alizocheza na asisti kitaifa na kimataifa

Anaitwa Pacome Zouzoua kiungo mshambuliaji wa Yanga SC inayoshiriki NBC Premier League. Amezaliwa 30/04/1997 ana umri wa miaka 29 yeye ni raia wa Ivory Coast anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Anauwezo wakucheza kiungo mchezeshaji, kiungo wa kati na wakati mwingine amekuwa akicheza eneo la ushambuliaji kwa umakini mkubwa.

SOMA HII: Je Pacome Zouzoua chanzo Yanga SC 0-0 Simba SC? Ali Kamwe atoa ufafanuzi

Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

SportPesa Aviator Challenge

Zijue timu ambazo amecheza Pacome Zozoua

Pacome Zouzoua
Pacome Zouzoua na tuzo ya NBC Premier League.

SOMA HII: Pacome Zouzoua yupo Yanga SC asaini miaka miwili | Magoli na rekodi zake akiwafunga Simba SC

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

23/24 ASEC Mimosas – Yanga SC
21/22 Afrika Sports- ASEC Mimosas
19/20 Africa Sports
19/20 Daugavpils
18/19 SC Gagnoa-Daugavpils
16/17 Sparta Prague B – SC Gagnoa
16/17 Williamsville – Sparta Prague B

Rekodi za Pacome CAF Champions League

2025/26 CAF Champions League ni mechi 10 amecheza alifunga magoli 2 akitumia dakika 775. Kiujumla katika CAF Champions League amecheza mechi 32 alifunga magoli 8 na ametengeneza asisti 2. CAF Confideration Cup ni mechi 15 magoli 3 asisti 1.

Rekodi za Pacome NBC Premier League

2024/25 alicheza mechi 26 za NBC Premier League akitumia dakika 1,626 alifunga magoli 12 na asisti 10. Wananchi walitwaa taji la ligi msimu uliopita. 2025/26 amefunga magoli 7 na kutoa asisti 4. Ametwaa tuzo za Man of the Match mara mbili msimu wa 2025/26. Yanga SC inapambania kutetea taji la ligi ikiwa inaongoza na pointi 60 baada ya mechi 25 na pointi 60.

SOMA HII: Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? | Wachambuzi wajibizana Edo Kumwembe vs Jemedari

Hitimisho

Pacome Zouzua ni kiungo mwenye uwezo mkubwa kutengeneza nafasi na kufunga magoli. Ni miongoni mwa wachezaji waliofika fainali CAF Confideration Cup 2023 wakati Yanga SC ikipoteza taji mbele ya USM Alger. Uwezo wake unafanya wengi kudhani mpira ni kazi nyepesi.

Share this: