Ijumaa ya Tarehe 24, majira ya saa 4: 45 usiku, timu ya taifa ya Ufaransa itawakaribisha Uholanzi kwenye Uwanja wa The Stade De France, jijini Paris.
Ufaransa watakuwa nyumbani, kama wenyeji katika mchezo huo, wakiwakaribisha Uholanzi katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Euro 2024, ambao ni muhimu kwa timu kupata ushindi ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kufuzu, mashindano haya ya timu za taifa za Ulaya..
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wenye ushindani na wakuvutia, baina ya timu hizi, kutokana na kila timu kuwa na wachezaji wake wote nyota na tegemeo wanaong’ara katika klabu mbali mbali, barani ulaya.
Kumbukumbu zinaonyesha, mara ya mwisho kwa ufaransa kucheza mechi za kiushindani, ilikuwa mwaka jana wakati wa kombe la dunia, ambapo timu hiyo ilifanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika jumla ya michezo mitatu, mmoja ikitoa sare na mwingine mmoja wakifungwa dhidi ya Tunisia.
Michezo hiyo waliyocheza ni pamoja na mechi dhihi ya Argentina (3-3), France VS Morocco (2-0), England VS France (1-2), France VS Poland (3-1) na Tunisia v France.(1-0)
Uholanzi kwa upande wao, katika michezo mitano ambayo wamecheza, nao wameshinda mechi tatu pekee huku wakitoa sare michezo miwili wakiwa hawajapoteza hata mchezo mmoja.
Na kesho wataingia uwanjani kuvaana dhidi ya Ufaransa wakiwa na rekodi nzuri ya kutofungwa katika siku za hivi karibuni. Hivyo yoyote kati ya mafahari hawa wawili ana nafasi ya kushinda katika mchezo huo.
Na michezo mitano ya Uholanzi waliyocheza hivi karibuni matokeo yalikuwa hivi; Uholanzi VS Argentina (2-2), Uholanzi VS Marekani (3-2), Uholanzi VS Qatar (3-2), Uholanzi VS Ecuador (1-1) na Senegal VS Uholanzi (0-2)
Kuelekea mchezo huo, mabeki wa Uholanzi watakuwa na kibarua kigumu mbele ya mshambuliaji hatari na tishio wa Ufaransa Kylian Mbappe ambaye amepewa unahodha hivi sasa na kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps.
Ingawa hakufanikiwa kutwaa kombe la dunia, kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamp, ameaminiwa tena na shirikisho la soka la Ufaransa mwezi Januari 2023, kwa kuongezewa mkataba wa kuinoa timu hiyo ya taifa mpaka mwaka 2026.
Akizungumza siku ya kutambulishwa rasmi kocha Didier alisema Ufaransa ina kazi kubwa ya kulinda heshima yake ya soka katika bara la Ulaya kwani ina mechi mbili muhimu za kufuzu kucheza kombe la Euro 2024 dhidi ya Uholanzi na dhidi ya Ireland.
Kwa upande wa kocha wa Uholanzi Ronald Koeman, yeye amerudishwa katika kibarua cha kuifundisha timu ya Taifa kuanzia Tarehe 1, Januari 2023, baada ya kocha Louis Van Gaal kutofanya vizuri wakati wa kombe la Dunia 2022, kule Qatar.
Kocha Koeman anarudi katika nafasi hiyo, baada ya kuiacha miaka miwili iliyopita akitimkia Barcelona ambapo alikuwa kocha mkuu mpaka. Akizungumza kurudi kwake katika nafasi ya kocha mkuu wa taifa Koeman alisema
‘’Nafikiri nimerudi sehemu ambayo sikuiacha ikiwa na hali mbaya. Nimerudi wakati timu hii inahitaji mtu ambaye ataivusha kutoka hapa ilipo na kuipatia mafanikio ya kisoka. Ni jukumu langu na pia nadhani wasaidizi wote pamoja na wachezaji wetu kuibeba nchi yetu katika mafanikio ya mpira wa miguu barani Ulaya. Mkataba wa Ronald Koeman utampeleka mpaka mwaka 2026 wakati wa Kombe la Dunia linalofuata.
Tukirudi Ufaransa, mchezaji machachari wa Ufaransa Kylian Mbappe, amepewa unahodha wa timu ya taifa akichukua nafasi ya nahodha mstaafu Hugo Lloris, aliyejihudhuru mara baada ya kumalizika kwa mashindano Kombe la Dunia nchini Qatar.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka, 24 anayekipiga klabu ya Paris Saint-Germain amekubali kupewa unahodha huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kocha wake Deschamps.
Staa huyo wa Ufaransa kwa mara ya kwanza ataiongoza timu hiyo, akiwa kama nahodha watakapovaana dhidi ya Uholanzi.
Wakati Mbappe akiwa nahodha mkuu, msaidizi wake ni kiungo mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann akimrithi beki wa kati wa Manchester United, Raphael Varane.
Mbappe ndiye mchezaji hatari kwa upande wa Uholanzi ambaye yupo katika kiwango bora katika kikosi cha Ufaransa ambaye alipiga hat-trick katika Fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika huko Qatar walipocheza dhidi ya Argentina.
Akiwa katika kiwango hicho bora Mbappe, lakini mshambuliaji huyo atakutana na safu ngumu ya vulinzi ya Uholanzi itakayoongozwa na beki tegemeo wa Liverpool, Virgil van Dijk.
Pia wapo mabeki wengine wenye kiwango bora watakaompunguza makali Mbappe ambao ni Nathan Benjamin Aké (Manchester City), Daley Blind (Bayern Munich), Denzel Dumfries na Stefan de Vrij (Inter Millan).
Wakati Uholanzi wakiwa na safu hiyo nzuri ya ulinzi, washambuliaji wataongozwa na staa wa Atletico Madrid, Memphis Depay, Luuk de Jong (Eredivisie club PSV Eindhoven).
Wengine ni Steven Bergwijn (Ajax), Wout Weghorst (Manchester United) na Vincent Janssen (Royal Antwerp F.C).
Kwetu SportPesa tukiwa kama wadau nguli wa ubashiri tumeshakuwekea mechi hizi ili uweze kuzibashiria.
Hivyo mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kila timu, kikubwa wote wanatakiwa kucheza kwa nidhamu, ikiwemo kushambulia kwa nidhamu.

