Mkazi wa mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Mbinga Mchopa. A. Mgaya amejishindia Tshs 18,004,468 kama bonus ya Jackpot ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.
Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Mchopa anasema alianza kucheza na Sportpesa zaidi ya miaka minne iliyopita . ‘’Nilianza kucheza na Sportpesa miaka minne iliyopita, na katika kipindi chote hiko nimefanikiwa kushinda kiasi tofauti kama Milioni 22, milioni 17 na kiasi cha mwisho ni hiki ambacho nimebahatika wiki iliyopita ambacho ni zaidi ya milioni 18 ambazo zote nimeshinda kwenye Jackpot ya mechi 13.

SportPesa nimeifahamu muda mrefu, kwa mara ya kwanza niliona tangazo kwenye ITV na baada ya hapo nilishawishika kuanza kucheza.na tokea hapo ndipo nilipoanza kujifunza kucheza pia Jackpot, pia SportPesa ni kampuni ambayo haina longo longo kwenye ulipaji pale ambapo unakuwa umeshinda.
Akiongelea kuhusu mkeka alioshinda, Mchopa anasema huwa anachukua muda mwingi sana kuanzia siku tatu hadi nne kuzikagua timu na kujua timu ipi ataipa ushindi.
‘’Mimi napenda ktumia muda mwingi sana kuangalia kwanza timu na kuzichambua kabla sijaweka mkeka wangu, na huwa natumia siku tatu hadi nne kupangilia mkeka wangu Mara nyingi huwa naweka mikeka 7
Akiongelea kuhusu ushindi alioupata, Mchopa alisema niliweka mikeka 7, na kati ya hiyo mmoja ndio uliotoa ushindi.
Anaendelea kusema wakati anasubiri matokeo hakuwa na uwoga kwa sababu yeye ni mzoefu kwenye kubeti na aliamini kuwa lazima apate ushindi.
Nakumbuka mechi ya mwisho ilikuwa ni ya Man United Vs Aston Villa ndio kidogo ilinipa hofu baada ya kukuta Man United ameshafungwa magoli 2 kipindi cha kwanza, nikaamua kwenda kulal, baadae nilivyoamka nilikuta Man United anaongoza magoli 3 na hapo hapo meseji iliingia, kwakweli nilifurahi sana.Alisema Mchopa.
Mchopa anawashauri watanzania wasisite kucheza kwa wingi kwani Jackpot ya Sportpesa ni halali na kama hawawezi hata mimi niko tayari kuwafundisha,kwa mtu yoyote anayehitaji kujuakucheza anaweza kunifwata pale Wilaya Mbinga ili na wao waweze kupata ushindi kama wangu. ‘’Nawaomba muitumie fursa hii kwani ndio njia ya uhakika kulamba mkwanja kama mimi’’.
Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kwenye biashara zake makazi yake ambayo anajenga na pia kidogo kitakachobaki ataongezea mtaji kwenye biashara yake..
Akiongelea ushindi alioupata Mchopa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sportpesa, Sabrina Msuya alisema, inafurahisha kuona sisi kama SportPesa tunaendelea kubadilisha maisha ya watu kila siku, ushindi huu wa Mchopa uwape hamasa hata wale ambao hawaamini kuwa watu wanaweza kushinda hela nyingi kuwa inawezekana, pia ningependa kumwambia Mchopa aendelee kucheza kwani nina amini atakuja kuwa mshindi wa Jackpot yote.
