skip to Main Content
Mkazi Shinyanga Alamba Jackpot Bonus Tshs 5,362,400/.
Mshindi wa Jackpot bonus Paul Method Dotto kutoka Kahama, Shinyanga akishikilia mfano wa hundi ya shillingi 5,362,400 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 kwenye Jackpot ya SportPesa wiki iliyopita. Jackpot kuwa ya SportPesa kwa wiki hii ni shilingi 1,031,243,893.

Mkazi Shinyanga Alamba Jackpot Bonus Tshs 5,362,400/.

Mkazi wa Shinyanga, wilaya ya Kahama, eneo la Chona Paulo Method Dotto, ameshinda Tshs 5,362,400 kama bonus ya Jackpot ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Paulo anasema alianza kucheza na Sportpesa miaka minne iliyopita. ‘’Nilianza kucheza na Sportpesa mwaka 2018 baada ya aliyekuwa mwalimu wangu kunifundisha kucheza.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Rafiki yake aitwaye Leonard ambaye ni wakala wa Airtel Money, Halopesa na Mpesa, alivutiwa na Sportpesa, baada ya kuona kiwango cha bonasi za Sportpesa ni kikubwa kuliko makampuni mengine.

Mshindi wa Jackpot bonus Paul Method Dotto kutoka Kahama, Shinyanga akishikilia mfano wa hundi ya shillingi 5,362,400 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 kwenye Jackpot ya SportPesa wiki iliyopita. Jackpot kuwa ya SportPesa kwa wiki hii ni shilingi 1,031,243,893.

‘’Mimi nilikuwa napenda kucheza hii michezo ya tusua mapene.Sasa siku moja nilikutana na mwalimu aliyenifundisha kuanzia form one mpaka form four. Sasa aliponiona ninaweka pesa kwa ajili ya michezo hiyo akaniambia mdogo wangu kwa nini hauchezi na Sportpesa. Nilimwambia sijui ndipo alipoanza kunifundisha.

 Kwa ufupi mwanzo ulikuwa mgumu kidogo, namshukuru mungu baada ya muda niliweza kucheza mwenyewe kwa urahisi na bahati nzuri niliwahi kushinda sh milioni 10 kwenye Jackpot bonus ya timu 13

Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Supa Jackpot bonus anasema aliweka mkeka wake siku ya Ijumaa na baadae kusubiria matokeo kuanzia Jumamosi ambapo timu zote alizozibetia zilimpa matokeo.

Mimi nilicheza Supa Jackpot ya mechi 13 ambayo niliona naiweza. Nilibahatika kupata mechi zote za Jumamosi na kukosa mechi moja tu siku ya Jumapili ambayo ilikuwa Arsenal ambayo ilifungwa na Manchester United’’. Alisema Paulo.

Paulo anawashauri watanzania wasisite kucheza kwa wingi kwani Supa Jackpot ya Sportpesa imeboreshwa na kukupa unafuu katika uchaguzi ucheze Jackpot yenye timu ngapi. ‘’Nawaomba muitumie fursa hii kwani ndio njia ya uhakika kulamba mkwanja kama mimi’’.

Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kwenye makazi yake ambayo anajenga na pia kidogo kitakachobaki ataongezea mtaji kwenye biashara yake..

Naye meneja uhusiano na Mawasiliano Sportpesa Sabrina Msuya alimpongeza Paulo kwa ushindi wake na kuwaasa watanzania waendelee kuiamini na kucheza na Sportpesa kwani wanaweza kushinda kama Paulo. ‘’Niwakumbushe tu watanzania Supa Jackpot kwa wiki hii ni 1,031,243,893/ endeleeni  kucheza mshinde kama Paulo.

Share this:
Back To Top