skip to Main Content
Daktari Mwanza Ashinda Tsh.49,041,581 Jackpot Bonus Ya SportPesa.
Mshindi wa Jackpot bonus mechi 12 kutoka Mwanza Ancet Clavery Macheta. akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 49,041,581. Jackpot ya SportPesa kwa sasa ni shilingi 1,089,062,84.

Daktari Mwanza ashinda Tsh.49,041,581 Jackpot Bonus Ya SportPesa.

Mkazi wa Buhongwa, wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, Anicet Clavery Macheta ameshinda shilingi 49,041,581 katika Jackpot Bonus ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13.

Akizungumza baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Anicet anasema alianza kucheza na Sportpesa kuanzia mwaka 2018, baada ya kuona matangazo na washkaji wengine wakishinda.

‘Mimi ni mpenzi wa mchezo wa mpira. Hivyo wakati bado ni mwanafunzi wa udaktari pale Muhimbili, wakati naishi hosteli maeneo ya chole Oysterbay nilikuwa napenda kwenda kuangalia mpira.

Mshindi wa Jackpot bonus mechi 12 kutoka Mwanza Ancet Clavery Macheta. akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 49,041,581. Jackpot ya SportPesa kwa sasa ni shilingi 1,089,062,84.

Siku moja wakati tunaangalia mpira alitokea kijana mmoja ameshika karatasi anashangilia kwa furaha. Nilipomuuliza vipi mwenzetu akasema ameshinda fedha kwenye mechi zilizotoka kuisha kuangalia’’.

Anasema kitendo kile cha yule kijana kilimvutia kumuuliza maswali zaidi namna ya kucheza hivyo baada ya hapo mwaka 2015 alianza rasmi kucheza. ‘’ Ilipita  miaka 3

Ndipo niliwasikia washkaji zangu wakiongelea Sportpesa na namna walivyo na odds kubwa na malipo ya haraka.

‘’Nilifuatilia namna ambavyo nilisikia kwa vijana wenzangu na kugundua kupitia sms na mitandao matokeo ya Jackpot yalikuwa yanaonyesha viwango vya ushindi kwa waliopata mechi 10, 11 na 12. Hilo lilinishawishi kuanza kucheza nao’’.

Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Jackpot bonus anasema aliweka mkeka wake siku ya Ijumaa baada ya kuichambua na kufanyia utafiti mechi kwa siku zaidi ya tatu.

‘Staili yangu mimi huwa siweki mikeka mingi ya Jackpot. Huwa naweka mkeka mmoja kwa dau lililoshiba kama ishara ya kujiamini, nikicheza zaidi dabo kombinesheni’’.

Anaendelea kueleza kuwa siku ya Jumamosi hakufuatilia mechi kwa kuziangalia moja kwa moja ila alienda mazoezi ya kukimbia ili aondoe hofu ya kupoteza ushindi wa mikeka yake. ‘’ Nilimaliza mazoezi muda ambao mechi zilikuwa zimeisha na nilipocheki matokeo nikakuta nimepata timu 9 kati ya 10 za siku hiyo’’.

Anicet anasema siku ya jumapili nayo ilikuwa ngumu kidogo kwani kila alipofikiria mikeka yake alipata shauku na hofu kwa kuwa zilikuwa zimebaki mechi chache, hivyo muda wa mechi ulipofika alijipa shughuli iliyomweka mbali na taarifa za matokeo ya mechi zilizosalia.

‘’Baada ya zile mechi kuisha nilienda kufungua kompyuta yangu na kuangalia matokeo mnamo majira ya saa moja usiku na dakika tano. Nilikuta nishinda mechi 12 kati ya 13 na hivyo kupata sms ya ushindi wa bonus ya timu 12 dakika tano baadae.

Anicet anawashauri watanzania wacheze bila kuchoka kwani Jackpot ya Sportpesa imeiva na itapata mshindi muda wowote. ‘’Mimi najitahidi kucheza kadiri niwezavyo naipigania hii bilioni moja kwa nguvu zote’’.

Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kwenye biashara zake na nyingine kwenye mipango yake ya baadae.

Kutoka Sportpesa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya aliongeza kwa kuwahamasisha watanzania kucheza Jackpot ya Sportpesa hasa katika kipindi hiki ambapo ligi mbalimbali zimerudi kama EPL, Championship, Laliga na Bundesliga ili kujishindia zawadi mbalimbali kwenye promosheni inayoendelea ya Bet Bonanza kama elfu 20 kila siku, mmilioni 1 kila wiki na tarehe 12/04 zawadi kubwa ya shilingi 15,888,000 zitatolewa kwa mshindi wa kufungia promosheni hii.

Kwa wiki hii kiwango cha Jackpot ni Tsh. 1,089,062,84.

Share this:
Back To Top