MWALIMU SIMIYU ASHINDA JACKPOT BONUS YA SPORTPESA 16,088,715
Mkazi wa Lamadi, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Shabani Salumu Forogo, ameshinda shilingi milioni 16, katika Jackpot Bonus ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12.
Akizungumza baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Shabani anasema alianza kucheza na Sportpesa mwaka jana 2021, baada ya kuona washikaji zake wakishinda.
‘’Nilianza kucheza na Sportpesa kama sikosei mwaka 2021, baada ya watu wangu wa karibu kuwa wanashinda mara kwa mara’’. Unajua watu kule wawanacheza Jackpot kwa wingi’’.
Kwa mujibu wake, Shabani ambaye pia ni mwalimu wa shule ya Msingi muungano, anasema alivutiwa sana na Sportpesa baada ya kuona na kusikia matangazo kuhusiana na Sportpesa kupitia mitandao ya kijamii na kwa watu wa karibu.
‘’Ujue nina rafiki zangu ambao wote walikuwa wanacheza Sportpesa na nilikuwa nawaona wanacheza na pia wengine walikuwa wanashinda na kunishauri nicheze, hivyo walinitamanisha na mimi kujaribu bahati yangu. Alisema Shabani.
‘’Kuna mmoja alishinda timu 10 na kushinda jackpot bonus, hivyo ilipelekea mimi kupata mshawasho mkubwa kupambania Jackpot’’.
Anaendelea kwa kusema ilibidi aamue kuwa siriazi na aanze kucheza ingawa mwanzo alikuwa anacheza na kukosa lakini hakukata tamaa. ‘’Mwaka ulipoanza niliweka nadhiri nianze kucheza kwa umakini mkubwa na hivyo mara ya kwanza nilijaribu Jackpot sikuambulia kitu na mara ya pili ambayo ni wiki ya tarehe 11 nimejaribu ndio hivyo nimeshinda’’.
Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Jackpot bonus anasema aliona mkeka wa jackpot siku ya ijumaa na kuanza kucheza papo hapo akiwa shule kwa kuwashirikisha walimu wenzake.

Mshindi wa Jackpot bonus mechi 12 Shaban Salum Fogoro akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 16,088,715. Jackpot ya SportPesa kwa sasa ni shilingi 940,850,660.
‘’Niliwashirikisha wenzangu stafu nikawaambia nahitaji kucheza Jackpot lakini zile timu nilikuwa sizielewi na kufanikiwa kutengeneza mkeka mmoja. Baada ya kurudi nyumbani nikiwa nimetulia mwenyewe nikaona nitengeneze mkeka wa kwangu mwenyewe kwa kuwa nilikuwa siwaamini wale wenzangu’’.
Anaendelea kusema baada ya kutulia na kupitia ule mkeka wa kwanza ambao alishirikiana na wenzake alitengeneza mkeka wa kwake binafsi kwa utulivu mkubwa ambao ndio huu umeshinda mechi 12.
‘’Ujue mimi baada ya kazi nilitulia nikatengeneza mkeka binafsi ambao sikufanya jitihada kubwa sana kwenye uchambuzi ila nilikuwa na Imani na ushindi, mkeka huu umeshinda’’.
Kuhusu ni kwa namna gani alipata matokeo ya mkeka ulioshinda Jackpot Shabani anasema siku ileile ya Tarehe 11 baada ya kutoka kazini alikwenda kwenye biashara yake ya boda boda, na baada ya hapo alianza kufuatilia matokeo kwa kutumia Livescore.
‘’Unajua ile ijumaa kulikuwa na mechi nane zinacheza na kwa muda ule naanza kutizama matokeo nilikuta timu saba zimeshatoa matokeo kama nilivyotaka hivyo nikawa nasubiria timu moja ambayo baadae nayo ilishinda kama nilivyoweka.
Siku ya Tarehe 12 Jumamosi niliwauliza washkaji zangu kwani ushindi wa Jackpot bonus unaanzia timu ngapi nikapewa jibu kuwa kuanzia timu kumi mpaka kumi na mbili .
Nilisubiri mpaka jioni ambapo timu zilianza kucheza tena hivyo timu zilizobaki zilishinda.
Baada ya mimi kupata timu kumi mechi zilizofuata zilikuwa za westham na Leicester city mechi hiyo niliweka droo na ilinipa presha kwani west ham alipigwa mapema tu lakini baadae alisawazisha.Ya mwisho ambayo ilikuwa timu ya kumi na mbili ilikuwa Kasimpasa ambayo nayo kama mechi iliyoisha ilipigwa goli mbili na kunichanganya sana. Namshukuru Mungu walifanikiwa kukomboa goli zote mbili na kutoa droo ya mbili mbili
Shabani anawashauri watanzania wote wasisite kucheza Jackpot ya SportPesa kwani ndio kampuni ya uhakika na haina ubabaishaji wa aina yoyote katika malipo.
Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atawekeza kwenye biashara zake na nyingine atanunua kiwanja hapa Dar es Salaam.
Kwa upande wa Sportpesa Meneja Uhusiano Sabrina Msuya alimpongeza sana Shabani kwa ushindi wake.
“Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza sana Shabani kwa kubashiri mechi 12 kwa usahihi kati 13”.
“Hii ni ishara ya kwamba kushinda hii Jackpot inawezekana, Kumbuka kuwa unaweza kuweka mkeka Zaidi ya mmoja au kubashiri kwa combination”. alimaliza
Kwa wiki hii kiwango cha Jackpot ni shilingi 940,850,660/-.