Bet Mpira wa miguu Ligue 1 – SportPesa imekuwekea timu bora nchini Ufaransa
SportPesa inakuletea timu bora kwa ubashiri wa mpira wa miguu wa Ligue 1, ikiwa utachagua kubeti kwenye mchezo mmoja. Tutembelee kwenye tovuti yetu.
Kati ya timu zote zenye ubora wa hali ya juu huko Uropa, Ufaransa imekuwa taifa ambalo kila mtu anataka kulishinda. Stade de France ni moja ya ukumbi wa michezo nchini humo, na wakati taifa liliposhinda Kombe la Dunia kwa mara ya pili mnamo 2018, ilithibitisha kuwa hii ni nchi ambayo timu yake inaweza kuchukua ubingwa sio Ulaya tu, lakini dunia nzima.
Kama timu yoyote kubwa ya kitaifa, mafanikio ya Ufaransa yamejengwa juu ya ubora wa mashindano yake ya ndani. Ligue 1 inawakilisha ubora zaidi, unaweza kubashiri juu ya Paris St Germain na zingine hapa SportPesa. Tunayo orodha kamili ya msimu mzima na mechi moja moja.
Kuanzishwa kwa Ligue 1
Ligi ya daraja la juu la Ufaransa inafuata muundo ule ule ambao unaonekana Uropa, kwa mfano, Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza. Hushindaniwa kati ya timu 20 bora nchini Ufaransa, kila moja ikicheza michezo 38. Kwa hivyo, kila timu inacheza na timu nyingine mara mbili, mara moja nyumbani na mara ya pili ugenini. Ligi hiyo inaendesha mfumo wa kukuza na kushuka daraja Ligue 2, tatu juu na tatu chini mwishoni mwa kila msimu.
Ligue 1 ilizinduliwa mnamo 1932, na kuifanya kuwa moja ya ligi za kihistoria ya mpira wa miguu Uropa yote. Kumekuwa na mabadiliko madogo ya mifumo kwa wakati huo wote, na kilichoingilia kati ni vita vya pili vya dunia mwaka 1939 na 1945.
Kwa miaka iliyopita, Ligue 1 imeonyesha vipaji vikubwa zaidi katika mpira wa miguu, historia za wachezaji kama Zinedine Zidane, Michel Platini, Zlatan Ibrahimovi, Thierry Henry na Neymar, kutaja wachache tu. Lakini ni timu gani zimetawala zaidi miaka na miaka? Jibu linaweza lisiwe wazi kama unavyofikiria.
Umaarufu wa PSG
Uliza watu 10 wataje timu ya Ligue 1, Tisa kati yao watasema Paris St Germain. Sio kilabu maarufu tu nchini Ufaransa, Iko katika nafasi za juu na Bayern Munich, Real Madrid na Manchester United kama moja ya timu bora katika mpira wa miguu wa Uropa.
PSG ni timu ambayo kila mtu anaiogopa sana katika Ligue 1, na imeshinda mara saba katika miaka nane iliyopita. Lakini unaweza kushangaa kujua kwamba kuna timu nyingine ambayo ina rekodi ya mafanikio zaidi Ligue 1.
Saint-Étienne alitawala ligi hiyo mnamo miaka ya 1960 na 70, na amekusanya jumla ya mataji 10, ikilinganishwa na tisa ya PSG. Kwa kuzingatia imekuwa miaka 40 tangu Saint-Étienne kuchukua ushindi. hata hivyo, labda ni suala la muda tu kabla hawajapitwa.
Uwekezaji nchini Paris.
PSG imepataje utawala kama huo baada ya miaka mingi kuwa chini? Ni muhimu kutambua kwamba timu ilianza tu mnamo 1970, kwa hivyo ni mpya ikilinganishwa na nyingi ambazo zina historia za miaka ya 1800. Timu hii ya kisasa ilichukua njia za kisasa na ikifuata mfano ulioletwa na Bayern Munich katika Bundesliga mapema miaka ya 1980. Wanaendesha kilabu kama biashara inayosimamiwa vizuri, wakipata pesa kupitia udhamini mzuri na mikataba ya utangazaji ili waweze kuzitumia kwa wachezaji bora zaidi.
Rekodi yao ya kumsaini Neymar kutoka Barcelona kwa Euro M222 mnamo 2017 ndiyo rekodi iliyosikika sana ulimwenguni, lakini huo si mkataba pekee wa pesa kubwa. Kylian Mbappe alisainiwa akiwa bado kijana kwa gharama ya Euro M135, wakati washambuliaji Edinson Cavani na Mauro Icardi, pamoja na winga Angel Di Maria kila mmoja alikuwa na bei zaidi ya € 50 milioni.
Swali kubwa katika Ligue 1 tunapoangalia kwa siku zijazo ni ikiwa PSG inaweza kuendelea kutumia kwa njia hii, ikizingatiwa hali ngumu timu zote za mpira wa miguu zimekuwa zikikabiliwa na miezi ya hivi karibuni. Maoni yako juu ya hiyo hakika itakuwa sababu katika uchaguzi wako wa kubashiri Ligue 1.
Kubeti mpira wa miguu Ligue 1.
SportPesa tunakupa wigo mpana wa kubashiri kwenye Ligue 1 ambayo utapata mahali popote. Mashabiki wengi wanapenda kuweka dau la haraka kwa timu moja au nyingine kushinda mchezo maalum, na ikiwa hiyo ni chaguo lako la kuchagua, unaweza kuelekea kuangalia mechi za Ligue 1 na uamue ni nani wa kumpa ushindi.
Mwishowe, hakikisha ujaribu mchezo wetu wa Ligue 1 katika michezo ya kubashiri. Hii ni aina ya ubunifu wa kubashiri mpira wa miguu, ambayo unaweza kuweka dau wakati mchezo unaendelea. Mashabiki wa mpira wa miguu wanavutiwa kuona jinsi pointi hubadilika wakati bao linafungwa, au mchezaji anatolewa nje. Mwisho, kuna tuzo kubwa za kupata ikiwa unaweza kuona mabadiliko na kuweka dau lako kabla ya pointi kubadilika.
Aina yoyote ya dau unalopendelea, utapata chaguo bora zaidi hapa SportPesa, iwe kwenye tovuti ama aplikesheni yetu.