skip to Main Content
ABDULAZIZ AKABIDHIWA SHILINGI 521,471,360/= NA SPORTPESA.

ABDULAZIZ AKABIDHIWA SHILINGI 521,471,360/= NA SPORTPESA.

1-Mshindi wa Jackpot ya SportPesa Abdulazizi Mussa Ibrahim akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360/- na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot. Jackpot ya SportPesa ni shilingi 218,361,140/-  kwa wiki hii.

2-Picha ya pamoja ya mshindi wa Jackpot ya SportPesa Abdulazizi Mussa Ibrahim akishikilia mfano wa hundi ya shilingi521,471,360/-pamojana wachezaji wa klabu ya Simba (Miraji Athumani).Jackpot ya SportPesa ni shilingi 218,361,140/-kwa wiki hii.

3-Mshindi wa Jackpot ya SportPesa Abdulazizi Mussa Ibrahim akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360/- na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas na wachezaji ya klabu ya Simba na Yanga baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot. Jackpot ya SportPesa ni shilingi 218,361,140/-kwa wiki hii.

4-Mshindi wa Jackpot ya SportPesa Abdulazizi Mussa Ibrahim akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360/- na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas na wachezaji ya klabu ya Simba na Yanga baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot. Jackpot ya SportPesa ni shilingi 218,361,140/-kwa wiki hii.

5-Picha ya pamoja ya mshindi wa Jackpot ya SportPesa Abdulazizi Mussa Ibrahim akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360/-pamojana wachezaji wa klabu ya Yanga(Farid Mussa, Bakari Mohammed na Carlinos ).Jackpot ya SportPesa ni shilingi 218,361,140/-kwa wiki hii.

 

NI BAADA YA KUBASHIRI KWA USAHIHI MECHI ZOTE 13.

Ijumaa, 09 Aprili 2021.Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa imemkabidhi rasmi mshindi wa awamu ya sita wa Jackpot mfano wa hundi ikiwa ishara ya kutimiza wajibu kama kampuni kwa washindi wake.

Mkazi wa Tabora-Sikonge Abdulaziz M. Ibrahim(24) ambaye pia ni mwajiriwa wa duka la dawa na maabara amekabidhiwa na SportPesa pesa aliyoshinda Jackpot ya mechi 13. Wakati wa makabidhiano katika ofisi za SportPesa Abdulaziz alisema “Nafurahi sana kwani baada ya kusubiri kwa kipindi kilichopangwa leo nimekabidhiwa rasmi fedha zangu”

Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza maana nilishajaribu mara kadhaa lakini sikufanikiwa.

Siku niliyoshinda niliweka mikeka kumi na kila mmoja shilingi elfu 2, katika mikeka yote 10 mkeka namba 7 ndio niliofanikiwa kushinda kwa mechi zote”

Mimi ni shabiki mkubwa wa Manchester United na kwa hapa Tanzania nashabikia Young Africans. Siku niliyoweka mikeka yangu niliikosesha ushindi Man U ambayo ilikuwa inacheza na Leister City kupelekea kufanikisha vizuri ushindi wangu.

Kwa upande wa SportPesa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas alianza kwa kuwashukuru waandishi wa habari kwa kuhudhuria tukio hilo muhimu la kumkabidhi mshindi mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360/-“

Leo ni siku ambayo tulikuwa tunaingojea kwa hamu sana maana tumeweza kukamilisha hili zoezi, huyu mshindi alipatikana tangu tarehe 22/03 lakini ilibidi tusubiri kipindi hiki cha maombolezo kimalizike ndipo tuendelee na sherehe ya kumkabidhi”

Katika ushindi wake Abdulaziz ameweza kubaki na shilingi 417,177,488/- huku akitoa shilingi 104,293,872/- kama malipo ya kodi ya zuio.“

Lengo letu ni kuendelea kuwainua vijana wa kitanzania na kuhakikisha tunabadilisha maisha yao, kwa kucheza jackpot tumeweza kuona jinsi Abdulaziz anavyoenda kubadili maisha yake”

Kila siku tunaendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha tunaboresha huduma na kuwafanya wateja wetu wazidi kufurahia kucheza na SportPesa”

Hivi sasa Jackpot yetu imepanda upya na kufikia kiasi cha shilingi TZS 218,361,140/- ambapo kwa atakayebashiri kwa usahihi mechi 13 ataibuka mshindi na kwa watakaobarishi kwa usahihi kuanzia mechi 10 hadi 12 watapata bonasi ya wiki”

Endapo Jackpot haitopata mshindi kwa wiki hiyo huongezwa mpaka pale mshindi atakapopatikana”

Mwisho.

Share this:
Back To Top