- Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? hili ni zaidi ya swali ambalo mashabiki wa Yanga wanajiuliza muda huu, hii ni baada ya kuwepo taarifa kuhusu uwezekano wa kuondoka kwa mastaa hao wengine wawili mwishoni mwa msimu huu.
- Baada ya kumuuza Aziz Ki kwa dola za marekani zinazokadiriwa kufikia 350k Imethibitishwa Yanga wamepokea ofa 3 zinazohitaji huduma ya Mzize, lakini mpaka sasa timu tatu zimethibitishwa ambazo ni JS Kabylie, Zamalek na Al Ittihad ya Libya huku ofa ya Zamalekh ikiwa ni kubwa kuliko.
- Kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho taarifa kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Yanga na Aucho. Ikumbukwe mkataba wa Yanga na Aucho unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? hili ni zaidi ya swali ambalo mashabiki wa Yanga wanajiuliza muda huu, hii ni baada ya kuwepo kwa taarifa kuhusu uwezekano wa kuondoka kwa mastaa hao wawili mwishoni mwa msimu huu ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Zilizothibitishwa kutoka ndani ya kikosi cha Yanga, Baada ya Aziz Ki, Mzize, Aucho wanaondoka Yanga?

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa kikosi cha Zamalek kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Misri wanakaribia kukamilisha usajili wa straika, Clement Mzize kutoka Yanga. Imeelezwa kuwa mazungumzo ya vilabu vyote viwili yamefanyika na yako kwenye hatua za mwisho kabisa.
Imethibitishwa kuwa Yanga wamepokea ofa kadhaa kutoka klabu zinazohitaji huduma ya Mzize, lakini mpaka sasa timu tatu zimethibitishwa ambazo ni JS Kabylie, Zamalek na Al Ittihad ya Libya huku ofa ya Zamalekh ikiwa ni kubwa kuliko ya JS Kabylie na Al-Ittihad ya Libya.
Lolote linaweza kutokea katika dili hili na huenda uongozi wa Yanga ukatoa taarifa rasmi ya kumuaga Mzize hivi karibuni, akiwa ni staa wa pili baada ya hivi karibuni kuagana na Mbukinabe, Aziz Ki aliyetimkia Wydad Casablanca.
Kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho taarifa kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Yanga na Aucho. Ikumbukwe mkataba wa Yanga na Aucho unaisha mwishoni mwa msimu huu na kuna uwezekano Aucho kuondoka Yanga.
SOMA HII PIA: Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Tetesi usajili bongo, ulaya
Pacome, Maxi kimeeleweka Yanga, Simba wanamtaka Job

Kwa mujibu wa mchambuzi, Hans Raphael amesema tayari Yanga wamemalizana na viungo, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli na wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na nahodha wao, Dickson Job ambaye pia anawindwa na Simba kwa mara nyingine tena.
“Yanga wamefanya mazungumzo na Dickson Job ili kusaini mkataba mpya, mkataba wa Job na Yanga unamalizika rasmi mwishoni mwa msimu huu na Job ametaja ofa yake na Yanga wameomba muda wa kuichakata kabla ya maamuzi ya mwisho kufanyika.
“Yanga wanamuona Job kama mchezaji muhimu kwenye kikosi chao na Job anaiheshimu Yanga na kuipa kipaumbele cha kwanza. Siku kadhaa zilizopita Simba waliulizia upatikanaji wake na wakaahidi kupeleka ofa yao ya kwanza baada ya fainali ya CAF, inatajwa Fadlu ni shabiki mkubwa wa Job.
“Hii sio mara ya kwanza kwa Simba kuulizia huduma ya Job na kama Job atasaini mkataba mpya na Yanga, basi ataungana na Pacome na Maxi ambao tayari wameongeza miaka miwili kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo,” amesema Hans.
SOMA HII PIA: Aziz Ki ameanza kazi Wydad Casablanca, Yanga SC ameacha rekodi
Je, Diakite ni mrithi sahihi wa Aucho Yanga?

Kufuatia uwezekano wa kuachana na Aucho, mchambuzi Hans ameendelea kusema Yanga wanaiwinda saini ya kiungo wa ulinzi wa Djoliba AC, Daba Diakite raia wa Mali.
“Yanga wamejitosa kwenye vita nzito ya kuinasa saini ya kiungo wa chini (holding Midfielder) wa Djoliba AC,Daba Benoit Diakite (21) raia wa Mali. Diakite ni bidhaa ya moto kwa sasa Africa na Yanga wanamuona ni mrithi sahihi wa Khalid Aucho.
“Kiungo huyo amebakiza mkataba wa mwezi mmoja na Djoliba, hivyo mwezi ujao huenda akaondoka kama mchezaji huru. Msimu uliopita Manchester Utd walituma scout wao kumtazama Diakite, Benfica Lisbon nao walifanya hivyo na huku Africa Kaizer Chiefs na De Tunis wanamtaka kiungo huyo.
“Diakite anawataka Yanga kuweka kipengele cha kumuuza mara moja endapo atapata ofa nzuri ya Ulaya. Wakala wa Diakite anajuana sana na viongozi wa Yanga na kwa miaka ya hivi karibuni Yanga walisajili wachezaji wake wanne tofauti.”
SOMA HII PIA: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki, sababu zatajwa
Kwa kuwa dirisha kubwa la usajili lipo karibu kufunguliwa kila kitu kuhusu tetesi hizi za usajili zitathibitishwa.

