Aziz WydadAziz Wydad
  • Aziz Ki aliwatesa makipa Bongo kwa mabao yake yalikuwa yanaleta gumzo kutokana na mashuti yake kudhaniwa kuwa yalikuwa ni mepesi.
  • Faroukh Shikalo wa Mtibwa Sugar alipotunguliwa na Aziz Ki hakumaliza msimu ndani ya timu hiyo aliomba kuondoka.
  • Aishi Manula wa Simba SC hakuwa na bahati kabisa mbele ya Aziz Ki hasa mguu wake wa kushoto ambao ulikuwa unatoa adhabu.

Aziz Ki ameanza kazi Wydad Casablanca akiwa ni kiungo mpya kwenye timu yake hiyo mpya mara baada ya usajili wake kukamilika akitokea Yanga SC ambapo huko ameacha rekodi.

Ki
Ki akitambulishwa kwenye timu yake mpya ya Wydad. Source: Wydad.

Ki Mei 25 alitambulishwa ndani ya Wydad Casablanca na Mei 26 2025 alianza mazoezi na timu yake hiyo mpya. Akiwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni ligi namba nne kwa ubora alifanya kazi yake kwa umakini.

Alitambulishwa Yanga SC akitokea Klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast msimu wa 2022/23 alitupia mabao 9 kibindoni. Kazi yake iliendelea kuwa miongoni mwa wachezaji amba oni chaguo la kwanza kwenye benchi la ufundi.

Aziz
Aziz ki kiungo wa zamani wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Ikumbukwe kwamba 2022/23 alitupia mabao 9 baada ya kucheza mechi 24 alikomba dakika 1,486 na alitoa pasi tano za mabao. Mabao yake yote alifunga kwa mguu wa kushoto.

Nyota huyo kwa sasa hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC kwa kuwa tayari ameshatambulishwa ndani ya timu mpya ya Wydad Casablanca.

Isome na hii: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki

Tuzo zake 2023/24

Aziz Top
Aziz Ki kwenye usiku wa tuzo za 2023/24. Source: Yanga SC.

Msimu wa 2023/24 alitwaa tuzo ya ufungaji bora alipofunga jumla ya mabao 21. Jina lake lilikuwa kwenye kikosi bora na alitwaa tuzo ya mchezaji bora. (MVP).

Msimu wa 2024/25 kwa Aziz Ki

Aziz Ki mpaka anasepa Yanga SC msimu wa 2024/25 rekodi zinaonyesha amecheza mechi 25 za ligi, dakika 1,676 amefunga mabao 9 na pasi 7 za mabao ametoa.

Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa amefunga mabao 8 na bao moja alifunga kwa pigo la kichwa.

Mkali wa mapigo huru

AzizĀ KIĀ ni miongoni mwa wachezaji ambao ni wakali kwenye kufunga mabao ya mapigo huru akitumia mguu wake wa kushoto kufunga akiwa nje ya 18.

2023/24 alifunga bao lake la 10 ilikuwa mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ilikuwa dakika ya 21. Timu nyingine aliyoitungua kwa pigo huru ni JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Inahusiana na hii:Aziz Ki anaondoka Yanga SC kusaini Wydad AC, Simba SC yatajwa

Makipa hawa wana rekodi naye ikiwa ni Shikalo na Makaka wa Mtibwa Sugar

Septemba 13, 2022 Uwanja wa Mkapa dakika ya 90 alimtungua Faroukh Shikalo aliyekuwa langoni akiwa nje ya 18. Mwendo wa kipa huyo haukuwa mzuri aliomba kuondoka ndani ya Mtibwa Sugar. Hili lilikuwa ni bao la kwanza la Aziz ndani ya ardhi ya Tanzania kwenye ligi.

Kwenye mchezo wa msimu wa 2023/24 alipokutana na Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Desemba 16 2023 aliwafunga mabao mawili dakika ya 45 kwa pigo la penalti na bao la pili alifunga dakika ya 65.

Langoni alianza Mohamed Makaka aliyetunguliwa jumla ya mabao manne kwenye mchezo huo pointi tatu zikawa za Yanga SC.

Air Manula wa Simba SC

Air Manula
Aishi Manula, kipa wa Simba SC. Source: Rabi Hume.

Oktoba 23, kipa wa Simba, Aishi Manula, Air Manula alitunguliwa na Aziz KI kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 dakika ya 45 na kufanya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 1-1 Simba.

Baada ya kuwa nje kwa muda Manula alirejea tena uwanjani kwenye mchezo wa ligi ilikuwa Novemba 5 2023 alitunguliwa na Aziz KI dakika ya 73 bao moja na mwisho ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Haule Benedict

Ilikuwa Mei 4 alimtungua Benedick Haule wa Singida Big Stars ambayo baadaye iliitwa Singida Fountain Gate na sasa inaitwa Singida Black Stars kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18.

 2023/24 bao lake la kwanza kufunga ilikuwa Uwanja wa Azam Complex alipowatungua KMC Agosti 28 kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18 na kutibua rekodi yake ya mguu wa kushoto kuhusika kwenye kufunga mabao mengi.

Maseke Wilbol wa KMC

Ni Wilbol Maseke kipa wa KMC alitunguliwa bao moja na Ki kwenye mchezo wa kwanza wa ligi. Mwisho ubao ulisoma Yanga 5-0 KMC. Dakika ya 58 Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Agosti 23 2023 akitumia mguu wake wa kulia

Abdulai wa Azam FC

Alifunga hat trick yake ya kwanza msimu wa 2023/24 ilikuwa dhidi ya Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 23 dakika ya 8, 69 na 71. Langoni alikuwa kipa mwili jumba Idrisu Abdulai.

2024/25 mechi yake ya mwisho

Aziz Ki
Aziz Ki kwenye mazoezi na timu yake ya zamani: Source: Yanga SC.

Msimu wa 2024/25 Aziz Ki mechi yake ya mwisho ilikuwa mbele ya JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Katika mchezo huo Aziz anayevaa jezi namba 10 alivishwa kitambaa cha unahodha ikiwa ni ishara ya kumuaga kiungo huyo ambaye alishuhudia ubao ukisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Aziz Ki anakuwa ni mchezaji wa kwanza kupewa Thank You ndani ya kikosi cha Yanga SC ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.

Share this: