- Aishi Manula ni suala la muda kuondoka ndani ya kikosi cha Simba SC ambapo mabosi wa Azam FC wanatajwa kuonyesha nia kuhitaji huduma yake.
- Fei Toto anagombaniwa na matajiri wa mitaa ya Kariakoo, Simba SC na Yanga SC ambao wanatajwa kupeleka ofa nono.
- Jonathan Sowah mshambuliaji wa Singida Black Stars jina lake limeongezeka thamani kutokana na kazi yake kubwa kwenye miguu yake.
Aishi Manula anaondoka Simba SC kwa kuwa inaelezwa yupo kwenye rada za Azam FC kipa huyo. Ikiwa dili lake litajibu huenda akaondoka bure ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Sababu kubwa ya Manula kuondoka bure ni mkataba wake aliongeza 2022 kutarajiwa kufika tamati mwisho wa msimu wa 2024/25 hivyo atakuwa ni mchezaji huru.
Azam FC wanatajwa kwa ukaribu kuwa kwenye mpango mkubwa wa kuinasa saini ya kipa huyo mwenye uzoefu kwenye mechi za kitaifa na kimataifa alipokuwa chaguo la kwanza Simba SC walitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Nafasi ya Air Manula Simba SC
Kwa sasa nafasi ya Air Manula ndani ya kikosi cha Simba SC kwa msimu wa 2024/25 imekuwa finyu. Sababu kubwa ilikuwa inaelezwa kuwa ni kutokuwa fiti kwa kuwa bado hajaimarika vizuri.
Kwenye mechi za ligi ambazo Simba SC imeshuka uwanjani msimu wa 2024/25 zote chaguo la kwanza alikuwa ni Moussa Camara na mara nyingi benchi alikuwa anakaa Ally Salim.
Mchezo mmoja alipata nafasi kucheza ulikuwa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal baada yah apo hakuonekana uwanjani jambo linalotoa nafasi kwake kuondoka.
Anga la kimataifa ndani ya Simba SC
Simba SC kwenye anga la kimataifa msimu wa 2024/25 imegotea nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Mech izote kuanzia hatua ya awali, makundi mpaka fainali ni Camara alianza langoni.
Alikuwa kwenye msafara wa kikosi kilichokuwa Zanzibar kwenye fainali ya pili dhidi ya RS Berkane lakini hakupata nafasi yakucheza.

Kwenye usajili wa dirisha dogo tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa Azam FC walipeleka ofa kwa Simba SC kuomba kupata saini ya Air Manula ila uongozi wa Simba SC uligomea kumuachia.
Feisal Salum wa Azam FC anagombaniwa
Kiungo mshambuliaji Feisal Salum wa Azam FC anatajwa kugombaniwa na wababe wawili ambao wanavutana kwa ajili ya kupata saini yake kwa sasa.

2023/24 Feisal Fei alifunga jumla ya mabao 19 alikuwa ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi. Msimu wa 2024/25 katupia mabao manne.
Simba SC na Yanga SC zinatajwa kuwania saini ya kiungo huyo mali ya matajiri wa Dar, Azam FC.
Clement Mzize anatajwa na Zamaleki FC
Kwenye eneo la ushambuliaji Clement Mzize anafanya kazi kubwa akiwa kafunga mabao 13. Anatajwa kuwa kwenye hesabu za Zamaleki FC ya Misri.

Inahusiana na hii:Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo
Ellie Mpanzu anatajwa Yanga SC
Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye dirisha dogo, Ellie Mpanzu anatajwa kuwa kwenye rada za watani wa jadi wa Simba SC, ambao ni Yanga SC inayohitaji saini ya winga huyo mwenye spidi akiwa uwanjani na uwezo wa kutumia mguu wake wa kulia.
Mpanzu ni chaguo la kwanza la Fadlu ni miongoni mwa wachezaji wanaoingia kwenye orodha ya waliopiga mashuti mengi kwenda lango la wapinzani katika mashindano ya kimataifa.
Mpanzu ni nafasi ya tatu kwa nyota waliopiga mashuti mengi kwenda kwa wapinzani akiwa amefikisha mashuti 31 na kinara ni Jean Ahoua ambaye alipiga mashuti 35.
Jonathan Sowah rasta wa Singida Black Stars
Mtambo wa mabao ndani ya kikosi cha Singida Black Stars Jonathan Sowah akiwa kafunga jumla ya mabao 11 msimu wa 2024/25. Kwenye mabao ambayo amefunga Sowah 11 moja alifanikiwa kumfunga kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Singida Black Stars, pointi tatu zilibaki kwa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi. Anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC na Simba SC.
Maxi Nzengeli anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba SC ambao wanahitaji saini yake kwa ajili ya kuwa naye katika kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Taarifa zinaeleza kuwa Maxi amekuwa akitumiwa meseji na watani wa jadi wa Yanga SC ambao ni Simba SC wakihitaji kupata huduma yake.
Kuelekea msimu wa 2025/26 ni usajili wa mchezaji mmoja pekee kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara umekamilika ni ule wa Aziz Ki aliyenunuliwa na Wydad Casablanca ya Morocco.
Soma na hii:Aziz Ki ameanza kazi Wydad Casablanca, ameacha rekodi Yanga SC

