skip to Main Content
Asian Handicap

Asian Handicap

Katika mchezo wa ubashiri, msemo Asian handicap unamaanisha aina ya ubashiri ambao hutofautisha au kutenganisha timu mbili, wakati timu moja wapo ikisadikika kuwa na ubora au uwezekano mkubwa wa kushinda kuliko mwenzake.

Handicap ni idadi ya magoli au pointi ambazo zinaongezwa katika matokeo ya mwisho ya timu iliyokuwa dhaifu, au kupunguzwa katika timu iliyokuwa bora ili kupata matokeo ya ubashiri.

Asian Handicap, SportPesa

Kwa mfano, timu A inaeleweka kuwa bora kuliko timu B, Bookmaker anaweza kuipa timu B ‘’handicap’’ ya over 1.5 ya magoli, wakimaanisha 1.5 ya magoli itajumlishwa kwenye matokeo ya mwisho ya mchezo.

Kama timu B itashinda mchezo au kupoteza kwa chini ya 1.5 kwa maana ya 0-1 au 0-1-2, ubashiri wa timu B utahesabika umeshinda.

Aina hii ya ubashiri ni maarufu pale ambapo kuna tofauti kubwa baina ya timu au wachezaji.

Na huu ni mfano wa kufurahisha;
Fikiria wewe na rafiki yako mnashindana kuona ni nani kati yenu anaweza kunywa bia kwa haraka kuliko mwenzake.

Wewe una imani unaweza kugida bia kwa haraka kuliko mwenzako, kwa hiyo unaweka ubashiri kuhusu hilo, lakini rafiki yako hana uhakika, kwa hiyo unakubali kumpa faida “handicap”kwamba yeye atangulie kugida bia yake.

 

Asian Handicap

Unaweka bia yake kwenye glass fupi, alafu unaweka bia yako kwene glass ndefu.

Kwa njia hii hata kama wewe ni mnywaji bia mzuri, rafiki yako ana nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu ya faida ya glass fupi.

Katika mfano huu ‘’handicap’’ ni tofauti ya urefu wa glass hizo mbili na imebuniwa kuweka mzani wa ushindi kati ya wewe na rafiki yako.

Kama ilivyo katika michezo ya ubashiri, ‘’handicap’’ inampa nafasi mchezaji au timu dhaifu (kwa mantiki hii) rafiki kupata nafasi ya kushinda na pia kumpa/kuipa timu bora (wewe) nafasi ya kuonyesha ukuu wako/ukubwa wako/uwezo wako.

Kwa hiyo, hata kama wewe ni nguli katika kunywa pombe, itakupasa kunywa bia yako kwa haraka sana kuliko rafiki yako ili ushinde.

Share this:
Back To Top