Uwanja mpya wa Yanga SC kwanini haujaanza kujengwa? Unaanza lini? | Injinia Hersi Said atoa tamko zito, sasa mambo safi GSM 50/50 Wananchi, Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)

Uwanja mpya wa Yanga SCUwanja mpya wa Yanga SCUwanja mpya wa Yanga SC

Uwanja mpya wa Yanga SC kwanini haujaanza kujengwa? Unaanza lini? | Injinia Hersi Said atoa tamko zito, sasa mambo safi GSM 50/50 Wananchi

  • Uwanja mpya wa Yanga SC umekuwa mjadala mkubwa kwenye vijiwe vya michezo kwa muda mrefu sasa, huku maswali ya kwanini hauanzi kujengwa yakipasua kichwa
  • Hali hii imemlazimu Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said kutoka hadharani kueleza sababu nzito za uwanja huo kuchelewa kuanza.
  • Injinia Hersi pia amethibitisha kuwa sasa mambo yamekamilika na wanakaribia kuanza ujenzi, huku makubaliano yakiwa ni wa umiliki wa asilimia 50 kwa mwekezaji GSM na 50 kwa wanachama Yanga SC.
  • Makala hii inachambua mambo muhimu katika taarifa hiyo ya Injinia Hersi Said.

Sakata la Uwanja mpya wa Yanga SC limekuwa mjadala mkubwa kwenye medani ya soka hapa nchini, huku maswali ya kwanini hauanzi kujengwa yakipasua kichwa. Hali hii imemlazimu Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said kutoka hadharani kueleza sababu nzito za uwanja huo kuchelewa kuanza kujengwa. Injinia Hersi pia amethibitisha kuwa sasa mambo yamekamilika na wanakaribia kuanza ujenzi, huku makubaliano yakiwa ni wa umiliki wa asilimia 50 kwa mwekezaji GSM na 50 kwa wanachama Yanga SC.

SOMA HII PIA: Uwanja mpya wa Yanga SC huu hapa | GSM 50/50 Wananchi, Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)

Ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC

Hersi Said
Hersi Said

Katika taarifa ya Injinia Hersi Said,  Yanga SC imesisitiza kuwa mradi wa ujenzi wa uwanja unaendelea kama ilivyopangwa. Klabu imefafanua kuwa hatua za awali za upimaji na usanifu zimekamilika, na sasa wanajiandaa kwa awamu inayofuata ya utekelezaji. Taarifa hiyo pia imewataka mashabiki na wanachama kupuuza uvumi wowote unaoenezwa na vyanzo visivyo rasmi, klabu imeahidi kutoa taarifa za mara kwa mara kupitia njia zake rasmi pindi tu kutakapokuwa na maendeleo mapya.

SOMA HII PIA: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog

Nini kimechelewesha ujenzi kuanza? Na je, unaanza lini?

Muonekano Uwanja mpya wa Yanga SC
Muonekano Uwanja mpya wa Yanga SC

Klabu imethibitisha kuwa tayari wameshakamilisha taratibu za kisheria na kimipango zinazohusiana na eneo la ujenzi. Hii inajumuisha vibali muhimu na makubaliano na wadau husika. Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amefafanua kuwa kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa uwanja mpya eneo la Jangwani kunatokana na klabu hiyo kufuata taratibu za kisheria na mwongozo wa Serikali.

Hersi amesema tangu makubaliano ya ujenzi yasainiwe (Mei 15, 2026), uongozi umekuwa na mawasiliano ya karibu na Serikali ili kuhakikisha kila hatua inafuata kanuni na taratibu salama kwa pande zote. Yanga wamekutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali 2 Novemba 2026, ambapo walipewa machaguo kadhaa ya namna bora ya kutekeleza mradi huo.

Hersi amesema klabu ilipokea rasmi mwongozo wa mwisho wa utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali siku ya Jumanne, Novemba 17, 2026. Uwanja huo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na mgawanyo wa Umiliki (50/50). Yanga itamiliki asilimia 50 ya hisa kwa kuchangia ardhi ya Jangwani, huku mwekezaji (Kampuni ya GSM) akimiliki asilimia 50 kwa kugharamia uwekezaji wa kifedha wa ujenzi huo. Hatua inayofuata itahusisha kuanza kwa kazi za ujenzi halisi, ambazo zitajumuisha uwekaji wa miundombinu ya msingi.

Shinda mpaka Milioni 800 sasa, cheza kindege cha SportPesa ushinde kwa kubonyeza hapa chini

Hitimisho

Uwanja mpya wa Yanga SC

Ujenzi wa uwanja mpya wa Yanga unatazamiwa kuleta mapinduzi makubwa kwa klabu hiyo, si tu kwa upande wa michezo bali pia kiuchumi. Utatoa fursa ya kukuza mapato na kuboresha mazingira ya mashabiki kufurahia michezo. Pia, uwanja huo utakuwa kituo cha maendeleo ya vijana na michezo mingine, ukichangia katika ukuaji wa soka nchini Tanzania. Yanga SC inaamini kuwa mradi huu utaiweka klabu katika ramani ya kimataifa. Endelea kufuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2026/27; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari mbalimbali za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.