Peter Shalulile ‘Shasha man’ ashtua NBC Premier League: Takwimu, matokeo, ratiba
- Mshambuliaji wa Yanga SC, Peter Shalulile ameendelea kushtua kwenye Ligi Kuu ya NBC 2026/27.
- Hii ni baada ya kufikisha mabao 6, bao moja tu kabla ya kumfikia kinara wa ufungaji kwenye ligi.
- Shalulile sasa anazidiwa goli moja tu na straika wa Polisi Tanzania, Anuary Jabir mwenye mabao 7.
- Shalulile sasa amehusika kwenye mabao 7 ya Yanga SC msimu huu akifunga mabao 6. Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu zake msimu huu.
Straika mpya wa Yanga SC, Peter Shalulile ‘Shasha man’ anaendelea kuitikisa Ligi Kuu ya NBC kwa rekodi ya kutupia mabao. Shalulile alijiunga na Yanga SC kwenye dirisha kubwa la usajili 2026/27 kutokea Mamelodi Sundowns kwa ada inayokadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 1.8 za kitanzania. Mara tu baada ya kuanza majukumu yake staa huyo amekuwa hacheki na wowote, akifunga karibu katika kila mchezo. Mpaka sasa amehusika kwenye mabao 7 ya Yanga SC akifunga mabao 6 na kuasisti bao 1, Makala hii inaangazia takwimu zake.
SOMA HII PIA: Peter Shalulile wamoto mechi 9 magoli 6: Takwimu zake Ligi Kuu ya NBC, hizi hapa
Historia ya soka ya Peter Shalulile

Peter Shalulile alianza safari yake ya soka nchini Namibia katika klabu ya Tura Magic, kabla ya kuhamia Afrika Kusini, ambako aling’ara zaidi. Nchini Afrika Kusini Shasha man alijiunga na timu ya Highlands Park. Huko ndiko alikoanza kuonyesha uwezo wake wa kipekee wa kufunga mabao, na kuvutia macho ya klabu kubwa. Uhamisho wake kwenda Mamelodi Sundowns ulikuwa stori kubwa nchini Afrika Kusini, na alipojiunga nao alifanikiwa kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Afrika, akishinda mataji mengi ya ligi na ya Afrika na kuwa mfungaji bora mara kadhaa.
SOMA HII PIA: Peter Shalulile atikisa usajili Yanga SC 2026/27: Atua Jangwani na mabao 136, asisti 35 hizi hapa rekodi zake
Zaidi ya Shilingi Milioni 800 inatoka muda huu, cheza kindege cha SportPesa, gusa hapa chini

Rekodi ya mabao na mafanikio barani afrika

Shalulile ameacha rekodi kali katika soka la vilabu barani Afrika. Akiwa na Mamelodi Sundowns, alikuwa nguzo muhimu katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa kama Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Uwezo wake wa kufunga mabao muhimu umemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki na mchezaji anayeheshimika na wapinzani. Ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini akiwa na zaidi ya mabao 100.
Ameshinda tuzo kadhaa za mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (DStv Premiership), na alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Sundowns kwa ufanisi mkubwa. Rekodi yake ya kufunga mabao katika CAF Champions League pia inamweka katika orodha ya washambuliaji bora wa kizazi chake. Kwa mujibu wa rekodi za Tranfermarket akiwa na jezi ya klabu tatu alizozichezea kabla ya kutua Yanga SC, Shalulile ameandika rekodi ya kipekee akifanikiwa kufunga mabao 136 katika mechi 313 alizocheza.
Atua Yanga SC kwa kishindo

Mara baada ya kumaliza maisha yake na timu ya Mamelodi, Peter Shalulile ametua Yanga SC kama mchezaji huru. Uhamisho wake ulianza kama tetesi, kabla ya taarifa rasmi kuthibitisha amekamilisha usajili. Usajili wake ulikuwa stori kubwa zaidi ya usajili kwenye dirisha kubwa la usajili ukikadiriwa kuwa nba thamani ya fedha za kitanzania Bilioni 1.8.
Hitimisho
Peter Shalulile ‘Shasha man’ ameendelea kujitambulisha kuwa ni mshambuliaji mwenye kipaji cha kipekee, ambaye anathibitisha uwezo wake barani Afrika. Msimu huu mpaka sasa anashika nafasi ya tatu kwenye listi ya wafungaji bora, lakini kuna kila uwezekano akawa anataka kubeba kiatu cha dhahabu kama ataendelea na kasi yake. Endelea kufuatilia SporPesa blog kwa taarifa zaidi.

