ChilamboChilamboChilambo

Nathaniel Chilambo: Usajili mpya Simba SC unaowavuruga watu Ligi Kuu ya NBC

  • Kama utaambiwa utaje majina ya walinzi wa kulia bora kwenye Ligi Kuu ya NBC kwa sasa, basi huwezi kuacha kulitaja jina la Nathaniel Chilambo.
  • Chilambo ambaye amejiunga na Simba SC akitokea ndani ya kikosi cha Azam FC amekuwa akiwavuruga wapinzani kutokana na maeneo anayocheza, ambapo mara nyingi anaonekana eneo la kushambulia.
  • Tangu kuanza kuitumikia Simba SC, mashabiki wa timu hiyo wameacha hofu ya kumkosa nahodha wao, Shomari Kapombe pale anapopata majeraha.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi wasifu na rekodi za Chilambo.

Nathaniel Chilambo amewaka ndivyo unavyoweza kusema, kumhusu nyota huyu wa Simba SC aliyejiunga nao akitokea ndani ya kikosi cha Azam FC. Kwa sasa kama utaambiwa utaje majina ya walinzi wa kulia bora kwenye Ligi Kuu ya NBC, basi huwezi kuacha kulitaja jina la Nathaniel Chilambo. Mlinzi huyo amekuwa akiwavuruga wapinzani kutokana na maeneo anayocheza, ambapo mara nyingi anaonekana eneo la kushambulia, licha ya kwamba ni mlinzi. Tangu kuanza kuitumikia Simba SC, mashabiki wa timu hiyo wameacha hofu ya kumkosa nahodha wao, Shomari Kapombe pale anapopata majeraha.

SOMA HII PIA: Matokeo ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27 | Man of The Match | Maxi Nzengeli | Nathaniel Chilambo | Msimamo| SportPesa Blog

Safari yake ya soka kabla ya Simba SC

Nathaniel Chilambo
Chilambo akiwa Azam

Kabla ya kutua Msimbazi, Nathaniel Chilambo alikuwa akicheza nafasi ya beki wa kulia katika klabu ya Azam FC. Akiwa na Azam, Chilambo alijijengea jina kama mmoja wa mabeki bora nchini, akionyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kupanda kusaidia mashambulizi. Uzoefu wake na Azam FC ulimpa fursa ya kucheza mechi nyingi za Ligi Kuu na mashindano mengine, na kumfanya kuwa mchezaji anayeaminika. Ni sifa hizi zilizovutia macho ya vigogo wa soka la Tanzania, Simba SC, ambao waliona umuhimu wa kumleta katika kikosi chao.

SOMA HII PIA: Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog

Usajili wake Simba SC

Chilambo X Kipre
Chilambo X Kipre

Usajili wa Nathaniel Chilambo kwenda Simba SC ulithibitishwa rasmi, na kuleta shangwe kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo Julai 20, 2026. Kuwasili kwake kumeongeza nguvu na ushindani katika safu ya ulinzi ya Simba SC, hasa katika nafasi ya beki wa kulia. Klabu hiyo inalenga kurejesha mataji na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa, na wachezaji wenye uzoefu na uwezo kama Chilambo wanaonekana kuwa muhimu katika kufikia malengo hayo. Mashabiki wanatarajia kumuona akiendelea kuonyesha kiwango chake bora na kusaidia timu kufikia malengo yao.

Shinda mpaka Milioni 800 muda huu, cheza Aviator ya SportPesa gusa hapa chini

image

Mchango wake kwa Simba SC na ligi kuu

Chilambo X Oura
Chilambo X Oura

Nathaniel Chilambo amekuwa na mchango mkubwa kwa Simba SC, si tu katika ulinzi bali pia katika kuanzisha mashambulizi. Uwezo wake wa kupanda na kushuka uwanjani unampa kocha chaguo zaidi za kimbinu. Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, uwepo wake hasa katika kipindi ambacho, Shomari Kapombe alikuwa majeruhi umezidi kuwafanya Simba kuwa imara.

SOMA HII PIA: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog

Hitimisho

Nathaniel Chilambo ni nyongeza muhimu kwa Simba SC na mi miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi hicho. Kwa uwezo wake wa kiufundi na uzoefu, ameleta mabadiliko chanya na kusaidia Simba SC kufikia malengo yao ya msimu huu. Safari yake ya soka inaendelea kuwa ya kuvutia, na mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni mafanikio gani makubwa ataipa Simba SC.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.