- Aziz Ki atarejea Yanga SC kuendelea na majukumu yake msimu wa 2025/26 ikiwa atakutana na Thank You Wydad Casablanca.
- Kocha Mkuu wa Wydad Casablanca, Mohammed Amin atajwa kutoridhishwa na uwezo wake.
- Clatous Chama kwenye orodha ya wachezaji watakaoongezewa mkataba Yanga SC.
Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Wydad Casablanca atarejea ndani ya Yanga SC ikiwa atapewa Thank You ndani ya Wydad Casablanca. Kiungo huyo alipata dili la kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco. Benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mohammed Amin Benhashem wa Wydad linatajwa kutoridhishwa na kiwango chake.


Soma hii: Aziz Ki, Chama Watikisa Dirisha la usajili Bongo
Huyu hapa Ofisa Habari Yanga SC kuhusu Aziz Ki
Ally Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC 2024/25 amefungukia suala la Ki kurudi ndani ya timu hiyo. Kamwe alibainisha kuwa kila kitu kipo kwenye makubaliaono. Alieleza kuwa Ki mkataba wake ulikuwa na vipengele muhimu.
“Kwa mujibu wa makubaliano ilikuwa hadi kufikia Julai 10 Wydad wawe wameshawasiliana na Yanga SC. Kama Wydad watakuwa wanaongeza maana yake wamalizie kiasi ambacho tulikubaliana ila kama watasema arudi sawa arudi aje awashone. Bado amebaki na mwaka mmoja,” amesema Kamwe.
Vuna mamilioni sasa na Aviator
Ni muda wakuvuna mamilioni sasa hivi. Unapaisha ndege na unapata mamilioni. Muda ni sasa mamilioni yanakusubiri.
Mbali na Aziz Ki kutajwa kurejea Yanga SC kuna wachezaji wengine ambao wataondoka. Wengine wataongezewa mikataba kwa sasa baada ya ligi kugota mwisho. Kumekuwa na tetesi nyingi kwa sasa. Hawa wengine wanatajwa namna hii:-
Clatous Chama
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anatajwa kuitwa mezani na mabosi wa timu hiyo kumuongezea mkataba. Chama kandarasi yake inagota mwisho ndani ya Yanga SC. Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Yanga SC, msimu wa 2024/25 alitambulishwa akitokea ndani ya Simba SC ambapo alikuwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kugota mwisho.
Dickson Job beki wa kazi
Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa kuitwa mezani kuzungumza kuhusu suala la kuongeza mkataba. Job mkataba wake unakaribia kugota mwisho hivi karibuni. Job alitambulishwa ndani ya Yanga SC akitokea Mtibwa Sugar.
Feisal Salum anatajwa Yanga SC

Soma hii: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo
Feisal Salum, kiungo mshambuliaji wa Azam FC anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Feisal ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho. Msimu wa 2024/25 katengeneza pasi 13 na kufunga mabao manne.
Nyota huyu mzawa amekuwa kwenye mwendelezo wa ubora. Msimu wa 2023/24 alifunga mabao 19 akiwa ni mzawa namba moja kufunga mabao mengi. Feisal aliweka wazi kuwa yupo tayari kurejea ndani ya Yanga SC ikiwa kutakuwa na makubaliano mazuri.
Ibrahim Keita wa TP Mazembe anatajwa Yanga SC
Ibrahim Keita ni mlinzi wa kulia ambaye mkataba wake na timu ya TP Mazembe unakaribia kufika mwisho na inaelezwa kuwa hayupo tayari kuongeza kandarasi nyingine. Yanga SC wanahitaji kufanya maboresho kwenye timu hiyo. Kuna uwezekano wakampata ndani ya timu hiyo kuelekea msimu wa 2025/26.
Singida Black Stars walianza kuulizia saini ya nyota huyo. Yanga SC wakafuata kuulizia ili kuinasa saini yake. Hivyo mabosi haw awa timu mbili wanaipambania saini ya nyota huyo.
Elvis Rupia anatajwa Yanga SC
Mkali kwenye kucheka na nyavu ambaye yupo Singida Black Stars, Elvis Rupia anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Jangwani Yanga SC. Yanga SC wanahitaji mshambuliaji ambaye atashirikiana na Prince Dube kwenye eneo la ushambuliaji. Ikiwa watampata Rupia itaongeza nguvu kwenye eneo hilo ambalo ni namba moja kwa Yanga SC.
Inaelezwa kuwa kwenye dirisha dogo Yanga SC walikuwa wanahitaji kuinasa saini yake. Walipishana naye baada ya kumchukua Israel Mwenda ambaye alikuwa ndani ya Singida Black Stars. Hivyo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya saini ya nyota huyo.
Jonathan Sowah- Yanga SC

Soma hii: Baada ya Mayele, Pyramids wanamtaja Aziz Ki 2024
Jonathan Sowah mshambuliaji wa Singida Black Stars anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Mshambuliaji huyo aliyeingia dirisha dgo anaingia kwenye orodha ya nyota waliowafunga makipa wote wa Simba SC na Yanga SC. Sowah alimfunga Djigui Diarra wa Yanga SC kwenye Ligi Kuu Bara ya NBC na alimfunga Moussa Camara wa Simba SC kwenye CRDB Federation Cup.
Huenda Sowah akatambulishwa ndani ya Yanga SC. Nyota huyo ana uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kulia akiwa uwanjani. Kwenye fainali dhidi ya Yanga SC mchezo wa CRDB Federation Cup alianza kikosi cha kwanza na alionyeshwa kadi mbili za njano na kuonyeshwa kadi nyekudu wakati Yanga SC wakitwaa ubingwa.
Kuna orodha kubwa ya wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC. Mabingwa hao wa NBC 2024/25 wanafanya maboresho kwa ajili ya timu hiyo kuendelea kuwa kwenye ubora. Yanga SC itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika jambo ambalo linawafanya wajiboreshe zaidi.


