Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FCMhiluMhilu

Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC
Geita Gold FC vs Fountain Gate FC

Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC : NBC Premier League 2026/27 | Highlights

  • FT:Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC,NBC Premier League 2026/27 Uwanja wa Bukombe, Oktoba 25,2026.
  • Yusuph Mhilu mfungaji wa bao la kusawazisha katika mchezo huo amechaguliwa kuwa Man of The Match.
  • Geita Gold FC kwenye msimamo ipo nafasi ya12 na pointi 8,Fountain Gate FC nafasi ya 16 na pointi 6.

Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC  haya ni matokeo rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Oktoba 25, 2026.Wageni walianza kupachika bao dakika ya 42 kupitia kwa Chukwunanye Macdonald kwa mkwaju wa penati.Wachimba madini walisawazisha dakika ya 63 kupitia kwa Yusuph Mhilu, Uwanja wa Bukombe,Geita.

Fountain Gate kwenye msimamo inaburuza mkia ikiwa na pointi 6 baada ya mechi 9.Geita Gold ipo nafasi ya 12 ina pointi 8 baada ya mechi 9.Vinara ni Simba SC wakiwa na pointi 24 wanafuatiwa na mabingwa watetezi Yanga SC nafasi ya pili na pointi 19.

SOMA HII PIA:Tanzania Premier League 2026/27: Fixtures, Results, Standings and Teams

image

Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC taarifa

Kipengele Maelezo
Mashindano NBC Premier League
Matokeo Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC
Uwanja Bukombe,Geita.
Tarehe 25/10/2026
Timu mwenyeji Geita Gold

Takwimu

Wamegawana pointi mojamoja wababe hawa wawili katika mchezo wa NBC Premier League.Kwa upande wa wenyeji walikuwa imara katika eneo la umiliki huku wageni wakipiga kona nyingi zaidi.Hizi hapa takwimu za wababe hawa ndani ya dakika 90 kwa mujibu wa Sokametrics wakusanya data za ligi:-

Kipengele Geita Gold FC Fountain Gate FC
Mabao 1 1
Mashuti 8 8
Umiliki 57%  43%
Pasi 469 411
Usahihi wa pasi 67% 62%
Pasi sahihi 316 256
Kona 2 5

Yusuph Mhilu nyota wa mchezo

Nahodha wa Geita Gold FC, Yusuph Mhilu amebeba tuzo ya mchezaji bora kwenye pambano hilo.Mhilu alifunga bao la usawa kipindi cha pili akitimiza majukumu kwenye eneo la ushambuliaji.Alitumia dakika 89 akifunga bao moja la muhimu, alipiga krosi 2 na mashuti 4 akiwa uwanjani.

SOMA HII PIA:Fountain Gate FC: Ngome Inayochipukia ya Soka Tanzania – Ratiba, Wachezaji na Maelezo Muhimu ya Klabu

Hitimisho

Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC ulikuwa mchezo wa moto uliopigwa Bukombe.Mchezo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kupigwa Desemba 30,2026.Felix Minziro hajawa kwenye mwendo mzuri na kikosi cha Fountain Gate katika mechi za msimu wa 2026/27.

Share this: