Ballon d’Or 2026 nani anashinda? Lamine Yamal, Harry Kane, Kylian Mbappe au Messi?
- Usiku wa kihistoria wa tuzo ya Ballon d’Or 2026 ni leo Jumatatu Oktoba 26, 2026.
- Tuzo za mwaka huu zinatarajiwa kutolewa pale London Palladium Theatre, nchini England.
- Swali kubwa ni nani atakayebeba tuzo hiyo mwaka huu? Huku majina ya Harry Kane, Lamine Yamal, na Kylian Mbappe yakitajwa kwa ukubwa.
- Makala hii inachambua maoni ya wachambuzi wa soka wa Shirika la Utangazaji la BBC
Usiku wa leo Jumatatu Oktoba 26, 2026 ni wa kihistoria wa tuzo ya Ballon d’Or 2026. Tuzo za mwaka huu zinatarajiwa kutolewa pale London Palladium Theatre, nchini England. Swali kubwa linabaki kuwa ni nani atakayebeba tuzo hiyo mwaka huu? Huku majina ya Harry Kane, Lamine Yamal, na Kylian Mbappe yakitajwa kwa ukubwa. Makala hii inachambua maoni ya wachambuzi wa soka wa Shirika la Utangazaji la BBC.
SOMA HII PIA: Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025
Kwanini Lamine Yamal anastahili kuwa mshindi wa Ballon d’Or 2026?

Msimu uliopita, Lamine Yamal alishinda ubingwa wa La Liga akiwa na Barcelona na ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Hispania. Yamal ni miongoni mwa vijana watano pekee, walioanza mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia na kufanikiwa kuibuka washindi. Mchambuzi wa soka la Ulaya, Guillem Balague anasema hakuna namna tuzo ya mwaka huu ikamkosa mchezaji wa PSG au, mchezaji wa Hispania.
Shinda zaidi ya Shilingi Milioni 800, cheza kindege ‘Aviator’ cha SportPesa sasa gusa hapa chini
Khvicha Kvaratskhelia

Kvaratskhelia ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili mfuulizo akiwa na PSG. Mtaalamu wa soka la Ulaya, Julien Laurens anasema Kvara alikuwa mchezaji bora zaidi barani Ulaya msimu uliopita, hasa kwenye Ligi ya Mabingwa, ambako alicheza kwa kiwango cha juu sana. Alisaidia kuiongoza timu yake kutwaa tena taji hilo kwa misimu miwili mfululizo. Anastahili Ballon d’Or kwa sababu alikuwa mchezaji bora duniani hadi kufikia Kombe la Dunia.
Harry Kane

Kane alifunga mabao sita katika Kombe la Dunia la mwaka 2026 akiwa na England. Alan Shearer, mshambuliaji wa zamani wa England anasema Harry Kane ndiye anayepaswa kushinda Ballon d’Or. Takwimu zake katika kipindi cha miezi 12 hadi 18 iliyopita zimekuwa za kuvutia sana akiwa na Bayern Munich na timu ya taifa ya England. Kwa sababu hiyo, anastahili kutwaa tuzo hiyo. Kane amefunga mabao 73 katika mechi 65, yakiwemo mabao 36 kwenye Bundesliga, aliiongoza Bayern Munich kutwaa mataji ya ligi na kombe la ndani, pia alifunga mabao 14 kwenye Ligi ya Mabingwa, akisaidia Bayern kufika nusu fainali.
SOMA HII ZAIDI: Dembele kushinda Ballon d’Or 2025: Hiki ndicho walichosema Messi, Mbappe, Neymar
Lionel Messi
Mshindi mara nane wa tuzo hiyo, Lionel Messi, anayeichezea Inter Miami ya Marekani na timu ya taifa ya Argentina, ni miongoni mwa mastaa wanaopewa nafasi hasa kutokana na mafanikio yake ya Kombe la Dunia. Messi alikuwa mchezaji muhimu akiisaidia Argentina kufika fainali mara mbili mfululizo ya Kombe la Dunia. Argentina ilipoteza fainali kwa Hispania kufuatia ushindi wa bao 1-0, huku Messi akiacha rekodi ya ufungaji.
Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, ni miongoni mwa majina mengine yanayotajwa kuwania tuzo hiyo. Mbappe anapewa nafasi kubwa kutokana na mafanikio makubwa binafsi, ambapo kwenye Kombe la Dunia 2026 alifunga mabao 10 na kumfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa historia ya mashindano hayo. Mbappe pia aliibuka mshindi wa ufungaji bora wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya akichangia mabao 71 kwa ujuma msimu uliopita.
SOMA HII PIA: Ronaldo, Dembele, Yamal watikisa Globe Soccer awards 2025
Hitimisho
Mchuano wa Ballon d’Or 2026 unaonekana kuwa mgumu kutokana na ukubwa wa majina na mchanganyiko wa mafanikio ya wale wanaoshindania. Je, ni Kylian Mbappe, Lamine Yamal, Kvara, Harry Kane au Lionel Messi. Fuatilia taarifa zote mpya kupitia SportPesa Blog.


