- Dembele amefanikiwa kuibuka mshindi wa Ballon d’Or 2025 baada ya kumaliza msimu na takwimu za kuvutia.
- Katika msimu uliopita, Dembele alifunga mabao 35 na kutoa asisti 16, akishinda makombe 4.
- Dembele kushinda Ballon d’Or 2025, nini Messi, Mbappe, Neymar mastaa wa soka wamesema?
Hatimaye usiku wa kuamkia leo Jumanne staa wa PSG, Ousmane Dembélé alitangazwa rasmi mshindi wa Ballon d’Or 2025. Hii ni baada ya staa huyo kuwa na msimu bora akiisaidia kushinda mataji manne. Miongoni mwa mataji hayo ni Kombe la kihistoria la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wapo waliokubali na kumpongeza na wapo waliozua mijadala mbalimbali, Makala hii inachambua hoja hizo.
SOMA HII PIA: Dembele au Yamal nani atashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025?
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Dembele kushinda Ballon d’Or 2025, mchakato ulikuwaje?
Dembele amefanikiwa kuibuka mshindi wa Ballon d’Or baada ya kumaliza msimu akiwa na takwimu za kuvutia. Katika msimu uliopita, Dembele alifunga mabao 35 na kutoa asisti 16 katika mashindano yote. Sehemu kubwa ya mabao na asisti hizo, Dembele alizitoa katika michezo mikubwa ya maamuzi. Ukiachana na takwimu hizo, bado Dembele alikuwa na mchango mkubwa ‘work rate’ uwanjani.
Mara baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Ousmane Dembélé mwenyewe aliongea maneno yaliyowagusa wengi. Katika hotuba yake ya kupokea tuzo, alishukuru kila aliyemsaidia kwenye safari yake kuanzia kwa klabu, makocha, wachezaji wenzake, na familia. Alisisitiza kuwa, ingawa ni tuzo ya mtu mmoja, lakini “inawakilisha juhudi za pamoja.”
SOMA HII ZAIDI: Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025
Kesi ya mshindani wake mkuu, Lamine Yamal

Katika vita hiyo ya Ballon d’Or, Dembele alikuwa akichuana kwa karibu na staa wa Barcelona, Lamine Yamal. Staa huyo kinda wa Barca alimaliza katika nafasi ya 2 tena akiyafanya yote hayo hata kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Yamal msimu uliopita alisaidia Barcelona kushinda Kombe la La Liga na Copa del Rey. Pamoja na hayo Yamal pia alikuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Spain katika mashindano ya kimataifa.
Baba yake Yamal akasirishwa na ushindi wa Ballon d’Or ya Dembele

Baada ya matokeo kutangazwa, baba wa Yamal alionesha kukerwa hadharani, akiuelezea uamuzi huo kama “ukaidi wa maadili” na “ajabu,” akisisitiza kwamba mtoto wake alistahili kwani alikuwa na mchango mkubwa zaidi ndani ya uwanja.
Mjadala juu ya Vigezo: Mabao vs Athari vs Mataji
Baadhi ya wakosoaji wanasema ingawa idadi ya mataji ya Dembélé na takwimu za mabao ni vya kuvutia. Vigezo kwa tuzo ya Ballon d’Or haviko wazi kila wakati, au havitumiwi kwa usawa. Wanaopingana wanaonyesha mechi ambapo athari ya Yamal, hasa kwa Barcelona na Spain katika michezo muhimu ilionekana katika ubunifu zaidi kuliko tu, kufunga goli.
SOMA HI ZAIDI: PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live: H2H, Vikosi, utabiri, habari za timu
Messi, Mbappe, Neymar watoa tamko

Kufuatia ushindi huo wa Dembele, mastaa mbalimbali wenye majina makubwa wamenukuliwa wakipongeza na kukosoa kama ifuatavyo:
Lionel Messi, aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake na mmoja wa wachezaji bora wa muda wote, alimpongeza kwa maneno ya kumtia moyo. Kupitia mitandao ya kijamii, Messi aliandika: “Ous mkubwa!!! Hongera, nimefurahi sana kwa ajili yako. Unastahili hii.” (Chanzo: The Standard)
Kylian Mbappé naye alimpongeza kwa kuchapisha tena ‘Repost’ tangazo la PSG na kuongeza ujumbe wa kuunga mkono: “Dembele, hizi ndizo hisia! Unastahili mara elfu moja.” (The Standard)
Luis Enrique, kocha wa PSG, alikuwa miongoni mwa waliomkubali tangu mwanzo. Miezi kadhaa kabla ya tuzo, alisema: “Ningempa Ballon d’Or kwa, Ousmane Dembélé. Hii ndiyo njia ya kuongoza timu. Mabao, mataji, uongozi, kuzuia, msukumo wake, Ousmane ndiye Ballon d’Or wangu. Sina shaka.” (Chanzo: Pulse Sports Nigeria)
Nasser Al‑Khelaïfi, rais wa PSG, pia alimuunga mkono Dembélé, akimwita “mchezaji wa kipekee, mtu wa ajabu” alipoulizwa kama ni miongoni mwa waliopigiwa upatu. (Chanzo: Tribuna)
Ukosoaji na Maswali Yaliyozuka

Baba wa Lamine Yamal, Mounir Nasraoui, alikuwa mkosoaji mkubwa zaidi. Baada ya mwanawe kumaliza nafasi ya pili, alieleza kuwa uamuzi huo “ulimuumiza na unaleta mswali mazito ya kimaadili.” Alisema anaamini kuwa Yamal ni “mchezaji bora zaidi duniani tena kwa mbali, si kwa sababu ni mwanangu bali kwa sababu ni bora kwa hakika.” (Chanzo: ESPN)
Aliongeza: “Kuna jambo la ajabu sana limetokea hapa,” na akasema kwa kujiamini: “Mwaka ujao Ballon d’Or itakuwa ya Mhispania.” (VnExpress International)
Neymar, pia alitoa hisia zake kali si moja kwa moja juu ya ushindi wa Dembele, bali kuhusu nafasi ya Raphinha. Raphinha, mchezaji mwingine wa Barcelona, alimaliza nafasi ya tano licha ya msimu bora. Neymar aliandika kwenye Instagram: “Raphinha nafasi ya 5! ni mzaha mkubwa.” (SPORTbible)
Hitimisho:
Kutoka kwa jumuiya ya soka kwa upana, baadhi walihisi kwamba, Mohamed Salah na wagombea wengine walipuuzwa. Na kuuliza maswali ikiwa uzito wa mataji na mafanikio ya Champions League unabadilisha mwelekeo wa kura kwa kiasi kikubwa. Hii ikiongeza je, inawaathiri wachezaji wabunifu ambao hawajashinda mataji mengi lakini wamekuwa na athari kubwa binafsi. Kwa mfano, Casemiro alieleza kuwa Salah alikuwa na hoja ya nguvu kama ya Dembele. (Planet Football)

