TRA United 0-0 Yanga SCKocha Yanga SCKocha Yanga SC

TRA United 0-0 Yanga SC
Mudathir vs TRA United

TRA United 0-0 Yanga SC | Highlights | Kocha Mkuu afutwa kazi | 24/10/2026

  • FT;TRA United 0-0 Yanga SC,NBC Premier League 2026/27, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. 
  • Manqoba Mngqithi afutwa kazi rasmi baada ya mchezo huo kukamilika ikiwa ni sare ya kwanza ndani ya msimu mpya.
  • Mudathir Yahya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC alionyeshwa kadi nyekundu atakosekana kwenye mechi mbili zijazo wakati Aziz Ki akirejea uwanjani.

Wababe wawili wametoshana nguvu baada ya dakika 90 kumalizika matokeo kuwa TRA United 0-0 Yanga SC NBC Premier League.Pambano hili limepigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha ukiwa ni mchezo wa mwisho wa Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi.Inakuwa ni sare ya kwanza kwa mabingwa watetezi 2026/27.

Kwenye pambano hilo kali kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mudathir Yahya alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 88.Anakuwa mchezaji wa pili kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, alianza Aziz Ki dhidi ya Geita Gold.Pointi mbili wameziacha ugenini wakigawana pointi mojamoja.

SOMA HII PIA:Presha Manqoba Mngqithi kufutwa kazi baada ya Dabi ya Kariakoo?

Bado hujashinda? Cheza na ushinde mpaka milioni 800 ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.Rubani huku mkwanja upo wakutosha unakusubiri.Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

TRA United 0-0 Yanga SC taarifa

Kipengele Maelezo
Mashindano NBC Premier League
Matokeo TRA United 0-0 Yanga SC
Uwanja Sheikh Amri Abeid
Tarehe 24/10/2026
Timu mwenyeji TRA United

Takwimu za mchezo

Yanga SC walikuwa na umiliki imara ugenini.Ni kadi nyekundu moja ilitolewa kwa upande wa mchezaji wa Yanga SC ambaye ni Mudathir.Kwa mujibu wa Sokametrics wakusanya takwimu wa ligi wameonyesha kuwa TRA United walipiga mashuti mengi yaliyolega lango zaidi ya wapinzani wao.

Kipengele TRA United Yanga SC
Mabao 0 0
Mashuti 11 12
Umiliki 45%  55%
Pasi 241 583
Mashuti yaliyolenga lango 4 2
Kadi nyekundu 0 1
Usahihi wa pasi 51% 76%

Maneno ya mwisho ya Kocha Mkuu wa Yanga SC

Manqoba Mngqithi kabla ya kufutwa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC Oktoba 24,2026 alibainisha kuwa walishindwa kumalizia nafasi ambazo walitengeneza.Kocha huyo raia wa Afrika Kusini aliongeza kuwa watafanyia kazi maboresho kwenye mechi zinazofuata.Aliwapongeza wapinzani kutokana na mchezo wa ushindani.

“Tulikuwa tumetengeneza nafasi ambazo hatukizibadili kuwa ushindi.Makosa ambayo yametokea tutafanyia kazi kuwa bora zaid.Bado kuna kazi kwenye mechi zinazofuata,”.

Msimamo wa NBC Premier League

Yanga SC inafikisha pointi 19 kwenye ligi baada ya mechi 8.TRA United nafasi ya 12 ina pointi 7 baada ya mechi 8.Vinara ni Simba SC wakiwa na pointi 24 baada ya mechi 8.

SOMA HII PIA; TRA United yaibana mbavu Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings

Hitimisho

TRA United 0-0 Yanga SC ni pambano ambalo lilikuwa na presha kubwa.Mabingwa watetezi wamesitisha mkataba wa Mngqithi muda mfupi baada ya mchezo Oktoba 24,2026.Matokeo ya mchezo uliopita wa Kariakoo Dabi, Simba SC 2-1 Yanga SC yaliongeza presha kwa kocha huyu raia wa Afrika Kusini.

Share this: