- Usiku wa Jumapili ya Desemba 28, huko Falme za kiarabu ulibaki kuwa wa kihistoria
- Hii ni baada ya kutolewa kwa tuzo za Globe Soccer awards 2025.
- Tuzo hizo huandaliwa na Baraza la Michezo la Dubai na kama ilivyotarajiwa, baadhi ya mastaa kama Cristiano Ronaldo, Ousmane Dembele na Lamine Yamal waliibuka kidedea kwa kuzoa tuzo tofauti.
Jana Jumapili, Desemba 28, Tuzo za Globe Soccer awards 2025 zilitolewa kwa mara nyingine tena. Tuzo hizo ambazo huandaliwa na Baraza la Michezo la Dubai, zilifanyika huko Umoja wa Falme za Kiarabu. Kama ilivyotarajiwa, baadhi ya mastaa kama Cristiano Ronaldo, Ousmane Dembele na Lamine Yamal waliibuka kidedea kwa kuzoa tuzo tofauti.
SOMA HII PIA: Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025
Je, hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu mchakato wa Globe soccer awards 2025

Tuzo hizi hutolewa kila mwaka na ziliasisiwa rasmi mwaka 2010. Lengo kuu la kutolewa kwa tuzo hizi ni, kukumbuka na kupongeza jitihada binafsi za wachezaji na timu zilizofanya vizuri zaidi katika msimu husika. Tuzo hizi huleta pamoja majina makubwa ya soka, kutoka Ulaya, Mashariki ya Kati na mashirikisho mengine.
Katika tuzo hizo tuzo zilitolewa kwa Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka, Mchezaji Bora wa Wanawake wa Mwaka. Klabu Bora ya Mwaka, Kocha Bora wa Mwaka, pamoja na tuzo mbalimbali za kibinafsi zinazohusu kila kipengele cha mchezo. Barcelona ikishuhudiwa ikitawala Tuzo za LaLiga 2025
Katika kipengele hicho cha La Liga, Barcelona ilitajwa kuwa Klabu Bora ya LaLiga, huku Hansi Flick akipokea tuzo ya Kocha Bora. Utambulisho wa mtu binafsi ulifuata, huku Jan Oblak akitunukiwa kama Kipa Bora, Raphinha alitawazwa Mchezaji Bora wa LaLiga, na Lamine Yamal aliyetajwa Mchezaji Bora wa U-23.
Cristiano Ronaldo aiteka Mashariki ya Kati, Dembele hashikiki

Kupitia tuzo hizo nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Mashariki ya Kati. Staa wa PSG Dembélé naye ametajwa kuwa mchezaji bora zaidi duniani mwaka wa 2025. Tuzo hiyo inabaki kuwa ya hadhi ya juu kuzidi zote. Dembele aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wapinzani wake, Kylian Mbappé, Raphinha, Vitinha na Lamine Yamal.
SOMA HII ZAIDI: Dembele au Yamal nani atashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025?
Aitana Bonmatí mchezaji bora kwa wanawake
Katika kipengele cha wanawake staa wa Barcelona na timu ya Taifa ya Spain, Aitana Bonmatí alitajwa kuwa mchezaji Bora wa Mwaka wa Wanawake. Nyota huyo aliwashinda: Mariona Caldeney, Melchie Dumornay, Alexia Putellas na Alessia Russo.
Diogo Jota apewa heshima

Moja ya wakati wa kusisimua zaidi wa sherehe za utoaji wa Tuzo hizo ni pale zilipotolewa heshima maalum kwa aliyekuwa staa wa Liverpool na Ureno, Diogo Jota. Nyota huyo aliyefariki dunia Julai 3 mwaka huu kwa ajali ya gari akiwa na mdogo wake nchini Spain. Katika hali ya kihisia, wazazi wa André na Diogo Jota walipokea heshima hiyo, na kuunda mojawapo ya matukio ya usiku yenye kuhuzunisha.
Hii hapa orodha kamili ya washindi wa Globe Soccer awards 2025

Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume: Ousmane Dembélé
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wanawake: Aitana Bonmatí
Klabu Bora ya Mwaka ya Wanaume: PSG
Klabu Bora ya Mwaka ya Wanawake: Barcelona
Kocha bora wa mwaka: Luis Enrique (PSG)
Kiungo bora: Vitinha (PSG)
Mshambulizi Bora: Lamine Yamal (Barcelona)
Mchezaji anayechipukia: Désiré Doué (PSG)
Wakala Bora: Jorge Mendes
Mkurugenzi Bora wa Michezo: Luis Campos (PSG)
Rais Bora wa Klabu: Nasser Al-Khelaïfi (PSG)
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Mashariki ya Kati: Cristiano Ronaldo
Muumbaji Bora wa Maudhui: Bilal Halal
Chuo Bora: Haki ya Ndoto
Tuzo la Mafanikio ya Kazi: Hidetoshi Nakata na Andrés Iniesta
Chapa Bora: Klabu ya Soka ya Los Angeles
Kocha Bora wa Akili: Nicoletta Romanazzi
Timu Bora ya Taifa: Ureno
Aliyerejea Bora: Paul Pogba
Tuzo la Maradona: Lamine Yamal
Hitimisho
Globe soccer awards 2025 zimekuja kuendelea kuielezea taswira ya soka kwa sasa. Timu za Barcelona na PSG zimeonekana kuwa na utawala na ushawishi mkubwa, kutokana na mafanikio makubwa waliyopata msimu uliopita. Mastaa wat imu hizi wameendelea kufurahia matunda ya kuwa na msimu bora wa 2024/25. Hii pia inawafanya kuwa na deni kubwa katika kuutekeleza msimu mpya wa 2025/26.

