Manqoba MngqithiManqoba (-)Manqoba (-)

Manqoba Mngqithi
Ellie Mpanzu nyota wa Simba SC vs Yanga SC, Kariakoo Dabi
  • Manqoba Mngqithi kufutwa kazi baada ya kupoteza mchezo wa Kariakoo Dabi?
  • Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amebainisha kinachofuata kuhusu benchi la ufundi.
  •  CFFA FC vs Yanga SC ni mechi inayofuata katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya dabi ya Kariakoo, macho yote yameelekezwa kwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini. Presha imekuwa ikiongezeka, huku tetesi zikieleza kuwa amepewa mechi chache akishindwa atafutwa kazi.Ikumbukwe kwamba huyu alianza kazi rasmi Julai 23, 2026 mara baada ya kutambulishwa na uongozi wa Yanga SC.

Mngqithi, raia wa Afrika Kusini, alichukua jukumu la kuiongoza Yanga SC katika msimu huu.Oktoba 10,2026 ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Simba SC 2-1 Yanga SC jambo linalotajwa kuongeza presha kwake kukaa kwenye benchi la ufundi mechi zijazo. Mngqithi sasa anahitaji kudhihirisha uwezo wake wa kukabiliana na changamoto kubwa na mchezo ujao ni Ligi ya Mabingwa Afrika CAF itakuwa ni CFFA FC vs Yanga SC, mechi ya kwanza raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA HII PIA:Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog

Bado hujashinda? Cheza na ushinde mpaka milioni 800 ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.Rubani huku mkwanja upo wakutosha unakusubiri.Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Screenshot ---------- ------
 

Manqoba Mngqithi anasemaje kuhusu matokeo ya Kariakoo Dabi?

“Tulianza kupata bao la kuongoza katika mchezo wetu muhimu dhidi ya Simba SC. Mabadiliko ya lazima yalibadili namna nzima ya mchezo. Unaona Duke Abuya alipata maumivu na huyu ni mchezaji muhimu yeye ni X Factor. Kuhusu Mudathir Yahya kumfanyia mabadiliko alikuwa amechoka hivyo kulikuwa na sababu ya kuingiza nguvu mpya,”.

Namna Yanga SC ilivyoanza mechi za NBC Premier League 2026/27

Yanga SC ilianza msimu wa 2026/27 wa NBC Premier League kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Namungo FC. Pia walishinda Coastal Union kwa mabao 4-1, ikionyesha uwezo wao wa kufunga magoli na kutawala michezo. Mwanzo huu imara uliweka matumaini makubwa kwa mashabiki wa Jangwani.

Licha ya mwanzo huu mzuri, dabi ya Kariakoo daima hubeba uzito wake. Matokeo yake yanaweza kuathiri morali wa timu na imani ya mashabiki. Kwa Mngqithi, ni muhimu kuhakikisha timu inarejea kwenye mstari wa ushindi haraka iwezekanavyo ili kutuliza presha.

Nini kinatarajiwa kutoka kwa Yanga SC?

Kikosi cha Yanga SC kimerejea kambini, Avic Town kwa maandalizi ya mechi zinazofuata.Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amebainisha kuwa wachezaji wamerejea kambini.Tayari maandalizi yanaendelea.

“Tayari wachezaji wetu wote wamerejea kambini kwa maandalizi ya mechi zinazofuata. Ni Duke Abuya pekee huyu hajarejea kambini kwa kuwa alipata maumivu katika mchezo wa Kariakoo Dabi. Jeraha lile ilikuwa ukiliangalia unaweza kusema ni dogo ila kwa sasa yupo kwenye uangalizi maalumu na jopo la madaktari,” amesema Kamwe.

Je kuhusu Mngqithi tetesi za kufutwa kazi zipoje?

Kuhusu benchi la ufundi Kamwe amefafanua kwa kubainisha: “Nitoe mfano kutoka katika msimu uliopita. Tulitoka kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Chamazi na kupoteza. Hali hiyo iliongeza presha kwa timu na uongozi na baadaye maamuzi yakafanyika kuhusu benchi la ufundi. Matokeo mabaya katika ligi hayapaswi kuamua hatima ya timu katika mashindano mengine. Timu inaweza kupitia kipindi kigumu, lakini ikiwa itajipanga vizuri na kurejesha umakini wake, inaweza kupata matokeo mazuri.

“Hata hivyo, ni lazima tutambue kwamba wapinzani wetu katika CAF Champions League hufuatilia kwa karibu hali za timu wanazokutana nazo. Huchunguza matokeo ya hivi karibuni, hali ya wachezaji, presha iliyopo ndani ya timu na mambo mengine yanayoweza kuwapa nafasi ya kupata ushindi.Kwa hiyo, hatupaswi kuwapa wapinzani wetu nafasi ya kutumia changamoto tuliyopitia baada ya Kariakoo Derby kama faida dhidi yetu.”

SOMA HII PIA:Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog

Hitimisho

Manqoba Mngqithi presha ya kufutwa kazi inazidi kupamba moto kutokana na matokeo ya Kariakoo Dabi. Yanga SC mara baada ya mechi 8 imepoteza mchezo mmoja kwenye ligi, Oktoba 10, 2026 ilipofungwa 2-1 dhidi ya Simba SC.Kuna mechi nyingine zinafuata huku kibarua cha kocha huyo raia wa Afrika Kusini kikitajwa kuwa mashakani.

 

Share this: