Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5 Zilizoacha Gumzo | Ellie Mpanzu nyota wa mchezo

Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5Kagoma vs MudathirKagoma vs Mudathir

Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5
Mpanzu vs Bacca Kariakoo Dabi
  • Kariakoo Dabi Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5 zilizoacha gumzo Uwanja wa Uhuru, Oktoba 10,2026
  • Ellie Mpanzu nyota wa mchezo akifunga bao la ushindi dakika ya 71 mbele ya Ibrahim Bacca na Bakari Nondo.
  • Mnyama amevunja uteja wakutoshinda mbele ya Yanga SC baada yakupita miaka mitatu, mara ya mwisho kushinda ilikuwa 16/04/2023
  • Manqoba Mnqithi mbinu zake zakwama mbele ya Steve Barker, Duke Abuya atumia dakika 25

Kariakoo Dabi, pambano la jadi kati ya Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5 ziliacha gumzo mwisho wa mchezo.Katika mchezo wa Oktoba 10,2026  mnyama alivunja uteja mbele ya mtani wake wa jadi.Rekodi kadhaa ziliwekwa na nyingine kuvunjwa, zikiacha gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki.

Ushindi huu muhimu haukuwa tu wa pointi tatu kwa Simba SC, bali pia uliweka mazingira ya kipekee kwa rekodi mbalimbali. Hapa tumekuletea rekodi tano muhimu zilizojitokeza baada ya mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na athari zake.

SOMA HII PIA:Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog

Screenshot ---------- ------
 

Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5 hizi hapa: Ushindi wa kwanza baada ya miaka 3

Mara ya mwisho Simba SC kupata ushindi dhidi ya Yanga SC ilikuwa 16/04/2023, Simba SC 2-0 Yanga SC.Baada ya hapo mechi zilizofuata mnyama hakupata ushindi. Mchezo wa mzunguko wa pili 2025/26 walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.Hivyo wamepata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu kupita.

Uteja wakutofungwa na Yanga SC umevunjwa rasmi. Utawala mpya unajengwa kwa sasa kutokana na watani hawa wa jadi kuwa na upinzani mkubwa.05/11/2023, Simba SC 1-5 Yanga SC ni kipigo kikubwa walichopokea wakiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa ligi.

Ibrahim Doumbia kupata nafasi Uwanja wa Uhuru

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia alipata nafasi kucheza dhidi ya Yanga SC. Nyota huyu raia wa Mali amekuwa akiimbwa na mashabiki wa timu zote kutokana na uwezo wake. Simba SC wamekuwa na matumaini naye kuwa atafunga mabao mengi huku wale wa Yanga SC wakiwa hawana imani naye.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC ameweka wazi aliomba dua kwa Mungu Doumbia asifunge. Kamwe alibainisha walikuwa wanatambua wamepoteza mchezo lakini hakutaka wafungwe mabao mengi.

“Tulipokuwa tumefungwa mabao 2-1 nilianza kuomba dua tusifungwe bao jingine. Kubwa zaidi niliomba Mungu Doumbia asifunge. Yaani hajafunga mechi zilizopita aje atufunge sisi ingekuwa ni ngumu mno,”.

Rekodi ya tatu: Ellie Mpanzu nyota wa mchezo

Nyota wa Simba SC, Ellie Mpanzu nyota wa mchezo baada ya kiwango bora na alifunga bao la ushindi dakika ya 71.Bao la kuweka usawa lilifungwa na Neo Maema dakika ya 68.Ndani ya dakika 4, Simba SC ilifunga mabao mawili mbele ya watani zao wa jadi, Yanga SC.

Mpanzu aliyekuwa bora tangu mwanzo wa mchezo alifanya majaribio manne, matatu yalikwenda nje ya lango. Ushangiliaji wake ulizua gumzo kwa kuwa aliandika chini ya uwanja.Kwa mujibu wa uongozi wa Simba SC uliweka wazi kuwa aliandika ‘Thank You God” ikiwa na maana Asante Mungu.

Rekodi ya nne: Athari kwa msimamo wa ligi

Ushindi huu wa Simba SC ulikuwa na athari kubwa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mnyama amefikisha pointi 21 baada ya mechi 7. Ni nafasi ya kwanza kwenye msimamo huku mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili.Simba SC ilipanda kutoka nafasi ya pili mpaka nafasi ya kwanza ikijenga utawala wake nafasi ya kwanza.

Rekodi ya tano: Mbinu za makocha na mabadiliko

Mchezo huu pia uliweka rekodi ya jinsi makocha walivyoweza kubadilisha mbinu zao na kufanya mabadiliko yaliyoweza kuleta matokeo. Ushindi wa 2-1 unaweza kuashiria ufanisi wa mbinu za Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker na jinsi alivyoweza kuwasoma wapinzani wake.Kocha Mkuu wa Yanga SC Manqoba Mnqithi akilazimika kutafakari upya mikakati yake.

Mabadiliko ya kiufundi alipotoka Clatous Chama nafasi yake aliingia Kalesto dakika ya 62Kiungo huyu alitoa pasi ya ushindi kwa Mpanzu dakika ya 71.Ibrhim Jabaar aliingia dakika ya 84 akichukua nafasi ya Anicet Oura na Neo Maema alitoka dakika ya 90 nafasi yake ilichukuliwa na Morice Abraham.Kila mchezaji alionyesha ufundi wake na kucheza kwa juhudi.

Kwa upande wa Yanga SC, mabadiliko yalibadili aina ya uchezaji, Duke Abuya alipata maumivu dakika ya 25. Kuingia kwa Ngoma kuliongeza presha kipindi cha kwanza na kile cha pili. Alipotoka Mudathir Yahya baada ya mchoko timu ilianza kujilinda zaidi.

SOMA HII PIA:Simba SC vs Yanga SC 10/10/2026: Steve Barker uso kwa uso na Manqoba Mngqithi, moto utawaka vita ya makocha

Hitimisho

Ukiweka kando matokeo ya Simba SC 2-1 Yanga SC rekodi 5 zimeandikwa kwa wababe hawa wawili. Mbinu za Steve Barker ambaye ni raia wa Afrika Kusini ziliwapa ushindi.Mnyama anaongoza ligi akiwa hajapoteza mchezo mpaka sasa msimu wa 2026/27.

Share this: