- FT:Pamba Jiji FC 2-2 Namungo FC NBC Premier League 27/11/2026
- Pambano hili lakukata na shoka limepigwa Uwanja wa CCM Kirumba wababe wakigawana pointi mojamoja.
- Pamba Jiji FC kwenye msimamo nafasi ya 14 ina pointi 10, Namungo FC nafasi ya 7 pointi 17.

Matokeo rasmi ni Pamba Jiji FC 2-2 Namungo FC NBC Premier League 2026/27.Wenyeji wamefunga kupitia Rogers Freddy alijifunga dakika ya 60 na Natanael Iga dakika ya 86. Nassoro Kapama dakika ya 52 kwa mkwaju wa penati na Herbert Lukindo dakika ya 77 hawa ni wafungaji kwa upande wa Namungo FC.Pambano hili limepigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
SOMA HII PIA:Namungo FC—Muhtasari, Kikosi, Ratiba, Matokeo, Takwimu, Tuzo na Habari Mpya
Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Taarifa Pamba Jiji FC 2-2 Namungo FC NBC Premier League
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Matokeo | Pamba Jiji FC 2-2 Namungo FC |
| Uwanja | CCM Kirumba |
| Tarehe | 27/11/2026 |
| Timu mwenyeji | Pamba Jiji FC |
Wachezaji bora uwanjani
Herbert Lukindo
Nyota wa Namungo FC alikuwa katika ubora ndani ya dakika 90.Alifunga bao moja alipiga shuti moja ambalo lililenga lango na alitengeneza nafasi 2.
Nassor Kapama
Huyu ni staa wa Namungo FC kwenye eneo la kiungo alitumia dakika 90.Alifunga bao moja na lipiga shuti moja ambalo lililenga lango.Aligusa mpira mara mbili ndani ya box.
Ndwangou Iga
Ni nyota wa wenyeji Pamba Jiji FC chini ya Kocha Mkuu,Francis Baraza.Huyu alianzia benchi na alitumia dakika 15 pekee kwenye mchezo huu muhimu. Alifunga bao la kusawazisha kwa shuti moja ambalo lililenga lango. Kwa mujibu wa takwimu za Sokametrics.
SOMA HII PIA:Pamba Jiji FC vs Namungo FC NBC Premier League 2026/27 | SportPesa Blog
Hitimisho
Pamba Jiji FC 2-2 Namungo FC matokeo rasmi kwenye pambano la ligi.Wababe hawa wamegawana pointi mojamoja baada ya dakika 90 kukamilika.Namungo FC inafikisha pointi 17 ikiwa nafasi ya 7 huku Pamba Jiji FC ikifikisha pointi 10 nafasi ya 14.

