Elie Mpanzu Kibisawala: Moto wa hatari NBC Premier League, Takwimu zake hizi hap ani balaa

ByJoel Thomas

October 13, 2026
Eli Mpanzu KibisawalaEli Mpanzu KibisawalaEli Mpanzu Kibisawala

 

  • Staa wa Simba SC, Elie Mpanzu Kibisawala ameendelea kuwa gumzo nchini, kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekionyesha msimu huu kwenye NBC Premier League.
  • Mpanzu ambaye wikiendi iliyopita aliteka vichwa vya Habari, hii ni baada ya kuifungia Simba SC bao la ushindi katika mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Watani zao wa jadi Yanga SC.
  • Katika mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Simba SC 2-1 Yanga SC, Mpanzu alionyesha kiwango bora kitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi.
  • Makala hii inakupitisha kwa ufupi kwenye takwimu za Mpanzu akiwa na Simba SC msimu huu wa 2026/27.

Elie Mpanzu Kibisawala, staa wa Simba raia wa DR Congo ameendelea kuwa gumzo nchini, kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekionyesha msimu huu kwenye NBC Premier League. Mpanzu wikiendi iliyopita aliteka vichwa vya abari, baada ya kuifungia Simba SC bao la ushindi katika mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Watani zao wa jadi Yanga SC.  Katika mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Simba SC 2-1 Yanga SC, Mpanzu alionyesha kiwango bora kitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi. Makala hii inakupitisha kwa ufupi kwenye takwimu za Mpanzu akiwa na Simba SC msimu huu wa 2026/27.

SOMA HII PIA: Usichokijua kuhusu usajili wa Mpanzu: Je, ni kweli Yanga SC walimpa mkataba?

Safari yake ya soka na kujiunga na Simba SC

Mpanzu
Mpanzu 

Elie Mpanzu alianza safari yake ya soka katika vilabu mbalimbali kabla ya kutua Simba SC. huku timu ambayo ilimtambulisha kwa ukubwa ikiwa ni AS Vita ya DR Congo, kiasi cha kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji. Uzoefu wake kutoka ligi tofauti umempa uwezo wa kuzoea mazingira mapya haraka na kuonyesha kiwango cha juu. Kujiunga kwake na Simba kulionekana kama nyongeza kubwa kwa kikosi hicho chenye malengo makubwa ya kutawala soka la Tanzania na Afrika.

Je, wajua? Unaweza kushinda Milioni 800 sasa, Cheza kindege ‘Aviator’ ya SportPesa upate ushind gusa hapa chini

Elie Mpanzu Kibisawala
 

Mchango wa Elie Mpanzu Kibisawala katika dabi ya kariakoo

Elie Mpanzu
Elie Mpanzu

Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC ni moja ya mechi kubwa na zenye ushindani mkubwa barani Afrika. Elie Mpanzu alipata nafasi ya kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo akifunga bao kali la ushindi na kuamua mechi kwa matokeo ya Simba SC 2-1 Yanga SC. Ukiachana na goli hilo Mpanzu alikuwa mwiba mkali akiongoza mashambulizi kiasi cha majaribio kadhaa kugonga mwamba. Mpanzu alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

SOMA HII ZAIDI: Elie Mpanzu Kibisawala ni Simba SC 2025/26/ Rekodi na magoli / Dili lake Yanga SC

Uwezo na mtindo wa uchezaji

Mpanzu anajulikana kwa uwezo wake wa kucheza kama kiungo mshambuliaji, akiwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kupiga chenga za maudhi pamoja na kufunga mabao. Mtindo wake wa uchezaji unamfanya kuwa mchezaji kamili anayeweza kuendana na mifumo mbalimbali ya makocha. Uwezo wake wa kucheza chini ya presha na kufanya maamuzi sahihi uwanjani ni sifa nyingine inayomtofautisha na wachezaji wengine na kumfanya kuwa tegemeo kubwa kwa Simba SC katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.

Takwimu za Elie Mpanzu Kibisawala

Mpanzu -
Mpanzu 

Mpanzu katika msimu huu mpya wa Ligi Kuu Bara 2026/27, Elie Mpanzu amekuwa miongoni mwa karata muhimu za Simba SC akihusika katika mabao 6 ya Simba SC akifunga mabao 4 na kuasisti mara 2. Mabao mawili kati ya hayo aliyafunga katika katika mchezo wa leo Jumanne dhidi ya Mashujaa FC ambao Simba wameibuka na ushindi wa mabao 6-1. Katika mchezo huo Mpanzu pia alifanikiwa kutoa asisti moja.

SOMA HII ZAIDI: Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC | Simba SC yatoa masharti mazito | Magoli na rekodi zake CAF

1UP, 2UP, 3UP Haina kusubiri dakika 90, chukua pesa yako mapema gusa hapa chini

Screenshot ---------- ------

Hitimisho

Kwa sasa, Elie Mpanzu Kibisawala anaendelea kuwa nguzo muhimu kwa Simba SC. Mashabiki wanatarajia kuona akiendelea kuonyesha kiwango cha juu na kuisaidia timu kufikia malengo yake ya kutwaa mataji zaidi. Mchango wake katika timu unaendelea kuwa muhimu katika kila mchezo. Kama ilivyo kwa wachezaji wengi wenye vipaji, kuna uwezekano wa kuwavutia vilabu vikubwa zaidi barani Afrika au hata nje ya bara Endelea kufutilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.