Simba SC vs Mashujaa FC: Ratiba NBC Premier League, Live score, h2h, Habari za timu  

ByJoel Thomas

October 12, 2026
Simba SC ratibaChama- Oura na MpanzuChama- Oura na Mpanzu

 

  • Baada ya kumalizika kwa kelele za Kariakoo Dabi, Ligi Kuu Bara yaani NBC Premier League inaendelea ambapo kesho Jumanne kuna ratiba ya mechi ya Simba SC vs Mashujaa FC.
  • Mchezo huu Unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuanzia saa 1 usiku.
  • Simba itaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu bora baada ya matokeo ya ushindi ya Simba SC 2-1 Yanga SC.
  • Hii ni mara ya kwanza kwa Simba SC na mashujaa kukutana msimu huu, na Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za mchezo huu.

Baada ya kumchapa mtani wake juzi Jumamosi, Mnyama kesho Jumanne atashuka Uwanjani katika ratiba ya mechi ya Simba SC vs Mashujaa FC. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuanzia saa 1 usiku. Simba itaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu bora baada ya matokeo ya ushindi ya Simba SC 2-1 Yanga SC siku ya Jumamosi. Hii ni mara ya kwanza kwa Simba SC na mashujaa kukutana msimu huu, na Makala hii inachambua kwa ufupi mambo muhimu kuhusu mchezo huu.

SOMA HII PIA: Mashujaa FC (0) vs Simba SC (3) NBC Premier League | Highlights, goal, h2h | SportPesa Blog

Weka mkeka wako wa mechi hii ya Simba SC vs Mashujaa FC moja kwa moja kwa kugusa odds hizi hapa chini

Screenshot ---------- ------

Msimamo

Msimamo wa ligi
Msimamo wa ligi

Timu hizi zinauelekea mchezo huu zikiwa katika maeneo tofauti katika msimamo wa ligi, Simba SC wanaongoza msimamo wa ligi na pointi zao 21 walizokusanya katika michezo yao 7 ya kwanza. Mashujaa FC wao wanaingia katika mchezo huu wakiwa nafasi ya nne baada ya kukusanya pointi 12 katika michezo 7. Nafasi zao kwenye msimamo zinaakisi mchezo mgumu ambao unatarajiwa.

Maandalizi ya vikosi

Simba SC vs Mashujaa FC
Mazoezi ya Mashujaa FC

Timu zote mbili zimekamilisha maandalizi yao ya mwisho kuelekea mchezo huu, maandalizi hayo yamefanyika katika uwanja wa Uhuru na Simba MO Complex. katika vipindi tofauti. Kila timu imeonekana kuwa tayari kwa mchezo huu.

SOMA HII ZAIDI: Mashujaa FC vs Simba SC NBC Premier League | H2H, takwimu, msimamo | SportPesa Blog

Historia ya mikutano yao H2H

Timu hizi zimekutana katika michezo 6, ambapo Simba SC wamekuwa na rekodi ya asilimia 100 ya kuwafunga Mashujaa FC. Wababe bao kutoka ziwa Tanganyika bado hawajafanikiwa kupata angalau hata sare mbele ya Simba SC. Hivyo matokeo ya mchezo huu yatakuwa muhimu kujua ushindani baina yao unaelekea wapi.

Shinda milioni 800 ya SportPesa sasa, cheza kindege ‘aviator’ kwa kugusa hapa chini

Screenshot ---------- ------

Kauli za makocha na wachezaji

Simba SC

Simba SC vs Yanga SC
Steve Barker

Kocha wa Simba SC, Steve Barker amesema maandalizi waliyofanya kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga SC yalikuwa ya ujumla kwa ajili ya mechi zote 2.  Barker pia amesema anatamani kuona wanaendeleza wimbi la ushindi.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha ya mchezo huu, maandalizi yetu yanatuweka katika nafasi nzuri ya kupata ushindi. Mashujaa ni timu ngumu, hivyo tunatarajia mchezo mgumu. Licha ya hayo yote malengo yetu ni kushinda,” amesema Barker.

Kwa upande wa wachezaji nyota, Anthony Mrigo kwa niaba ya wachezaji wenzake malengo yao ni kushinda mchezo huo. Amesema kila pointi ni muhimu kwao katika vita ya bingwa.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC 2-0 Mashujaa FC Ligi Kuu Bara NBC: Mnyama afufuka! Highlits,Matokeo, Ratiba

Mashujaa FC

Simba SC 2-1 Yanga SC NBC Premier League
Kocha wa Mashujaa FC, Aman Josiah amesema mchezo wa NBC Premier League dhidi ya Simba SC utakuwa fursa kwa timu yake kupima mambo mbalimbali. Kwa upande wake, mchezaji Jonas Mkude amesema wanautazama mchezo huo kama michezo mingine. Mkude ameendelea kusema wanawapa heshima mpinzani wao na kujiandaa kukabiliana na changamoto watakayokutana nayo uwanjani.

Hitimisho

Kuelekea mchezo huo wa Simba SC vs Mashujaa FC, wenyeji wa mchezo kupitia kwa Semaji lao, Ahmed Ally ametangaza rasmi viingilio vya mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa. Ahmed pia amewahimiza mashabiki wa Simba SC kujitokeza kwa wingi uwanjani, ili kutoa sapoti kwa wachezaji wao katika mchezo huo. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.