Coastal Union 1-0 Singida Black Stars: Highlights, NBC Premier League, matokeo, magoli yote, rekodi za h2h

ByJoel Thomas

October 13, 2026
Coastal Union --- Singida Black StarsCoastal Union --- Singida Black StarsCoastal Union --- Singida Black Stars

  • Ligi Kuu Bara imeendelea tena jana Jumatatu, ambapo huko Tanga matokeo yalikuwa Coastal Union 1-0 Singida Black Stars.
  • Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara, yaani NBC Premier League ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
  • Ni goli la Gradi Kiala Lassa la dakika ya 15 ndilo liliweka tofauti ya matokeo ya mchezo huo.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi matokeo, magoli na mwenendo wa mchezo huu.

Ligi Kuu Bara yaani NBC Premier League imeendelea tena jana Jumatatu, ambapo huko Tanga ubao wa matokeo wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-0 Singida Black Stars baada ya filimbi ya dakika 90. Mchezo huu ulipigwa majira ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.  Ni goli la, Gradi Kiala Lassa la dakika ya 15 ndilo liliweka tofauti ya matokeo ya mchezo huo. Hizi hapa takwimu muhimu za mchezo.

SOMA HII PIA: Ligi Kuu ya Bara fixtures

Mchezo ulivyokuwa

Coastal Union 1-0 Singida Black Stars
Coastal vs Singida

Coastal Union waionyesha dhamira ya wazi ya kushinda mchezo huo tangu dakika ya kwanza, hii ni baada ya kufanya mashambulizi mfululizo. Baada ya majaribio kadhaa Coastal walipata bao pekee la mchezo huo dakika ya 15 kupitia kwa, Gradi Kiala Lassa baada ya safu ya ulinzi ya Singida kujichanganya. Baada ya bao hilo Singida waliamka na kusaka bao la kusawazisha, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda mpaka mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili mchezo ulikuwa wa kushambuliana kwa zamu. Singida Black Stars wakisaka bao la kusawazisha, huku Coastal wakisaka bao la ziada la ushindi. Dakika 90 zilitmatika kukiwa hakuna mabadiliko ya ubao wa matokeo yaani ‘Score board’.

SOMA HII ZAIDI: Singida Black Stars FC: Matokeo, Ratiba na Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2026/27)

Habari za timu na majeraha baada ya mchezo

Kikosi cha Coastal baada ya ushindi
Kikosi cha Coastal baada ya ushindi

Hakuna taarifa rasmi za majeraha makubwa au wachezaji muhimu, baada ya mchezo huo kumalizika, zilizopatikana kwenye vyanzo vya habari. Hii ina maana makocha watakuwa na vikosi kamili kuelekea ratiba za mechi zao zijazo. Ratiba ya mechi zijazo inaonyesha Coastal Union watakuwa ugenini Oktoba 24, dhidi ya Namungo hukuSingida Black Stars wakiwa wageni wa Pamba Jiji Oktoba 29, mwaka huu.

Shinda hadi milioni 800, Paisha kindege ‘Aviator’ ya SportPesa ushinde, gusa hapa chini

Screenshot ---------- ------

Takwimu za ana kwa ana na fomu ya sasa

Mchezo ulivyokuwa
Mchezo ulivyokuwa

Historia ya michezo ya ana kwa ana kati ya Coastal Union na Singida Big Stars inaonyesha ushindani mkali. Mchezo wa jana unakuwa mchezo wa 7 kwao kukutana ambapo, Coastal wamekuwa na rekodi bora wakishinda mara 4, Singida Black Stars wameshinda mechi 2 tu. Mchezo mmoja uliosalia uliisha kwa matokeo ya sare.

SOMA HII PIA: Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27 | Kadi nyekundu | Highlights | SportPesa Blog

Hitimisho

Matokeo ya Coastal Union 1-0 Singida Black Stars yanatoa changamoto kubwa juu ya mwenendo wa kikosi cha Singida ambacho sasa kimeshuka mpaka nafasi ya 5 kwenye msimamo. Kazi kubwa inabidi kufanyika ili warejee katika nne bora, ambayo sasa ina mgeni mpya timu ya Mashujaa United. Kwa Coastal Union ushindi huu umewapeleka mpaka nafasi ya 12 ya msimamo na angalau kikosi chao kimeanza kupata matokeo ya ushindi baada ya kuanza vibaya.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.