Mzee Mpili shabiki wa Yanga SC afariki dunia

ByLunyamadizo Mlyuka

September 28, 2026
Mzee MpiliMpiliMpili
  • Mzee Mpili alifariki dunia usiku wa kuamkia Septemba 27, 2026, katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri (Rufiji) mkoani Pwani alipokuwa akipatiwa matibabu.
  • Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Msikiti Mkuu uliopo Ikwiriri, mkoani Pwani.
  • Hatuchezi ni moja ya kauli maarufu aliyozungumza enzi za uhai wake

Shabiki maarufu wa Klabu ya Yanga SC, Haji Omari Ramadhani Mpili maarufu kwa jina la Mzee Mpili, amefariki dunia usikuwa Septemba 27,2026. Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga SC imeeleza  Mzee Mpili, amefariki katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu. Shabiki huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matatizo ya mgongo, kiuno na magonjwa ya uzee. Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, majira ya saa 10:00 jioni, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Rufiji, Mkoa wa Pwani.

SOMA HII PIA: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Screenshot ---------- ------
Screenshot ———- ——

Yanga SC yamlilia Mzee Mpili

Mzee Mpili
Mzee Mpili enzi za uhai wake.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu ya Yanga SC imeeleza kuwa mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, amefariki dunia usiku wa Septemba 27, 2026, katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika saa 10:00 jioni, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Rufiji, Mkoa wa Pwani.Mpili atakumbukwa kutokana na ujasiri wake katika matukio mbalimbali. Hatuchezihatuchezi ilikuwa ni kauli yake maarufu wakati alipokuwa hai.

Hitimisho

Mwanachama na shabiki maarufu wa Yanga SC, Mzee Mpili amefariki dunia. Mpili ameumaliza mwendo huku akiacha alama kwenye uliwengu wa mpira. Atakumbukwa kwa ucheshi wake na kauli zake kuuchangamsha mpira wa Tanzania.

Share this: