- FT: Yanga SC 1-0 Geita Gold NBC Premier League Septemba 15, 2026 Uwanja wa KMC Complex
- Bao la ushindi limefungwa na Oumar Kamara akitumia asisti ya Maxi Nzengeli ambaye ni Man of The Match
- Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz Ki ameonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 18 kwa kumchezea faulo Datius Peter
Mchezo wa mzunguko wa 6, Yanga SC 1-0 Geita Gold ni matokeo halisi kwa wababe hawa wawili. Bao ka ushindi limefungwa na Oumar Kamara dakika ya 55 kwa pasi ya Maxi Nzengeli. Kiungo mshambuliaji Aziz Ki alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 18 baada ya kumchezea faulo Datius Peter. Mabingwa hao watetezi walilazimika kucheza wakiwa pungufu mpaka mwisho wa mchezo, Uwanja wa KMC Complex.
Takwimu muhimu Yanga SC 1-0 Geita Gold, KMC Complex

Mechi 5 zijazo za Yanga SC: Ratiba ya Yanga SC mechi 5 zijazo NBC Premier League | Matokeo | SportPesa Blog

Wananchi wameendelea na rekodi ya ushindi ndani ya uwanja. Takwimu muhimu tumekuletea hapa zilizotokana na mchezo huo. Huu unakuwa ni mchezo wa 6 Yanga SC kushuka uwanjani wakishinda mechi zote.
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Kadi nyekundu | Aziz Ki wa Yanga SC dakika ya 18 |
| Bao la ushindi | Oumar Kamara dakika ya 55 |
| Asisti | Maxi Nzengeli |
| Man of The Match | Maxi Nzengeli |
| Matokeo | Yanga SC 1-0 Geita Gold |
| Uwanja | KMC Complex |
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Yanga SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 18. Geita Gold inasalia na pointi 7 nafasi ya 9 kwenye msimamo. Pamba Jiji FC inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.

H2H: Yanga SC vs Geita Gold: Yanga SC vs Geita Gold ni leo NBC Premier League | H2H | Livescore | Prediction |SportPesa Blog
Hitimisho
Ni Yanga SC 1-0 Geita Gold matokeo ambayo yameendelea kuwaketisha katika utawala wa namba moja mabingwa watetezi. Ushindi huo muhimu ulipatikana kipindi cha pili dakika ya 45. Yanga SC inaendelea kuonyesha umwamba kwenye eneo la kusaka pointi tatu katika mechi ngumu.

