- Ni Azam FC iliyo nafasi ya 3 kwenye msimamo dhidi ya Simba SC iliyo nafasi ya pili NBC Premier League leo Septemba 16, 2026 Uwanja wa Azam Complex
- Mchezo huu wakukata na shoka utapigwa saa 1:00 usiku kwa Afrika Mashariki katika Mzizima Dabi.
- Fuatilia mchezo huu stats, livescores, lineups kupitia SportPesa Score
Mchezo mkali unatarajiwa kuchezwa leo Septemba 16, 2026 Uwanja wa Azam Complex, Azam FC vs Simba SC NBC Premier League 2026/27. Timu zote mbili zina wachezaji imara wenye takwimu bora. Azam FC imejumuisha wachezaji hatari akiwemo Idd Nado, Feisal Salum na Mubiru. Mnyama amejumuisha wachezaji bora akiwemo Clatous Chama, Oura na Libasse Gueye.
Zitambue taarifa muhimu Azam FC vs Simba SC NBC Premier League

H2H: Azam FC vs Simba SC: Azam FC vs Simba SC NBC Premier League | H2H | Livescores | SportPesa Blog
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindenge
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Makocha wa pande zote mbili wamebainisha ugumu wa mchezo huu mkubwa. Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema wamefanya maandalizi mazuri. Ameongeza kuwa hakuna mchezo mwepesi unaowakutanisha wapinzani hawa wawili uwanjani.
“Mchezo wetu dhidi ya Simba SC sio mwepesi inatokana na ubora wa mpinzani wetu. Kila tunavyokutana unakuwa ni mchezo wenye utofauti na mbinu tofauti.Ninamshukuru Mungu tumepata muda wa maandalizi hivyo mchezo wetu muhimu tutatumia nafasi kutafuta ushindi,”.
Kwa upanda wa Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker ameweka wazi wanakibarua kigumu ugenini. Kocha huyo ameongeza wametoka kucheza mchezo mgumu wanakutana na timu ngumu. Aliongeza kwamba wapo tayari kwa ushindani lengo ni kupata matokeo mazuri.
“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Azam FC. Tumeona ni wapinzani wagumu na ukizingatia tumetoka kucheza mchezo mgumu. Tupo tayari kwa mchezo malengo ni kupata pointi tatu ugenini,”.
Takwimu za wachezaji wakuchungwa Azam FC vs Simba SC
| Jina la mchezaji | Timu | Dakika alizocheza | Mabao | Nafasi alizotengeneza | Asisists |
| Nado | Azam FC | 411 | 1 | 13 | 1 |
| Oura | Simba SC | 377 | 1 | 11 | 1 |
| Mubiru | Azam FC | 275 | 1 | 11 | 2 |
| Libasse | Simba SC | 360 | 1 | 32 | 5 |
Msimamo wa NBC Premier League
Simba SC ni nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 5. Azam FC ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo. Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 18.

Azam FC vs Simba SC team fomu: Azam FC vs Simba SC NBC Premier League | H2H | Livescores | SportPesa Blog
Hitimisho
Ni Azam FC vs Simba SC NBC Premier League Mzizima Dabi. Mchezo wa kukata na shoka kwa wababe hawa wawili. Matajiri wa Dar watakuwa nyumbani wakimkaribisha Mnyama.Timu zote mbili hazijapoteza mchezo hivyo kila mmoja atakuwa kazini kusaka rekodi kupata ushindi mara ya kwanza. 2025/26, Azam FC alipata ushindi mchezo wa mzunguko wa kwanza na kuwa timu pekee iliyoifunga Simba SC.

