- FT: Yanga SC 1-0 Simba SC Ngao ya Jamii 2026, Uwanja wa New Amaan Complex
- Albert Kangwanda mfungaji wa bao la ushindi dakika ya 32 akitumia pasi ya Boka
- Ibrahim Jabaari wa Simba SC, Clatous Chama, Ellie Mpanzu washindwa kufua dafu
Ni Yanga SC 1-0 Simba SC Ngao ya Jamii 2026 mchezo wa ufunguzi pazia la NBC Premier League 2026/27. Wababe hawa walikuwa na dakika 90 bora zilizovuta hisia za wengi. Bao la ushindi lilifungwa na nyota Albert Kangwanda dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Taarifa kuhusu Seleman Mwalimu: Ngao ya Jamii Yanga SC vs Simba SC: Selemani Mwalimu atua Zanzibar aanza mazoezi na Shalulile, Kariakoo Derby, Matokeo, Ratiba, h2h, Habari za timu
Je, unataka kushinda mamilioni ya SportPesa?
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi, kwa kubonyeza picha hapo chini.

Yanga SC 1-0 Simba SC Ngao ya Jamii 2026, Uwanja wa New Amaan Complex

Rekodi ya Kariakoo Dabi: Simba SC 2-2 Yanga SC: Matukio 6 ya ajabu yaliyotokea, NBC Premier League, matokeo na Takwimu | SportPesa Blog
Hatimaye mchezo wa Kariakoo Dabi umeandika rekodi ubao uliposoma Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii 2026. Katika mchezo huo dakika 20 za mwanzo mnyama alianza kwa kasi kulisakama lango la Wananchi. Jitihada zao hazikuwapa matunda mpaka walipofungwa bao dakika ya 32.
Nyota mpya wa Yanga SC, alisubiri kufanya majaribio mawili illipofika dakika ya 30. Alianza dakika ya 30 shuti lake lilikwenda nje ya lango na jaribio la pili ilikuwa dakika ya 32 alipofunga bao la ushindi. Pasi hiyo ilitoka kwa beki wa pembeni Boka aliyekuwa kwenye ubora kazini.
Ibrahim Jabaari, Clatous Chama, Ellie Mpanzu washindwa kufua dafu
Nyota wa kikosi cha Simba SC,kinachonolewa na Kocha Mkuu Steve Barker kilikwama kufua dafu dhidi ya Yanga SC. Licha ya uwepo wa nyota wenye majina akiwemo Clatous Chama, Ellie Mpanzu, Ibrahim Jabaari bado matokeo hayakupatikana. Mnyama alianza kwa kasi dakika 20 za mwanzo jambo lililowapa presha Yanga SC.
Wakati zikiwa zimesalia dakika 15 mpira kukamilisha dakika 45 za mwanzo hapo upepo ulibadilika. Bao la dakika ya 32 lilibadilisha ile kasi ya Simba SC. Licha ya mabadiliko kipindi cha pili bado Yanga SC walikuwa imara kulinda ushindi na mwisho wakatwaa taji ya Ngao ya Jamii.

