- Pazia la mashindanio ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake WAFCON 2026 linakaribia mwishoni.
- Mashindano hayo kwa sasa yameingia katika hatua ya Nusu Fainali, ambapo timu 4 tayari zimefuzu kuisaka Fainali.
- Mataifa 4 ambayo yamefuzu hatua hiyo baada ya mechi za Robo Fainali, na kutengeneza vita ya nusu fainali ni Morocco vs Cameroon na Algeria vs Malawi.
- Makala hii inakupa uchambuzi mfupi kuhusu mechi hizo 2 za hatua ya Nusu Fainali.
WAFCON 2026 imeingia hatua ya Nusu Fainali, ambapo timu nne zimefuzu kusaka nafasi ya kucheza fainali. Mataifa 4 ambayo yamefuzu hatua hiyo baada ya mechi za robo fainali ni: Morocco, Algeria, Malawi na Cameroon. Katika hatua ya Nusu Fainali mechi zinatarajiwa kuwa Morocco vs Cameroon na Algeria vs Malawi.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Cheza Aviator na upate nafasi ya kushinda hadi TZS milioni 800 kwa raundi.
Kuhusu Muhtasari wa WAFCON 2026 hatua ya Nusu Fainali

Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake WAFCON 2026 imekamilika, na mechi za Nusu Fainali zimepangwa. Mechi zote za Nusu Fainali zinatarajiwa kupigwa leo Jumatano Agosti 12, 2026. Mechi mbili za kusisimua zinasubiriwa katika mashindano hayo ya bara, ambayo pia yanatumika kama mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA Brazil 2027. Ikumbukwe timu hizi 4 tayari zimefuzu moja kwa moja Kombe la Dunia la mwaka ujao.
Mabingwa watetezi Nigeria walishindwa kuifungua ngome ya Cameroon kwenye Robo Fainali, huku Malawi ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza, wakitoka nyuma na kuifunga Ghana. Morocco wamefika nusu fainali kwa mara ya tatu mfululizo, huku Atlas Lionesses wakikaribia kutwaa taji lao kubwa la kwanza endapo watafanikiwa kwenda mpaka mwisho. Wameungana na Algeria, ambao nao wameweka historia kwa kufikia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mashindano haya.
Nusu Fainali ya Kwanza: Morocco vs Cameroon
Kuna motisha kubwa kwa Morocco ambao wanacheza nyumbani, licha ya kwamba wamewahi kupoteza fainali mara mbili. Timu hiyo iliyo na nafasi ya juu zaidi kwenye viwango kati ya timu zilizobaki, wanaamini wanaweza kuvunja kile kinachoonekana kama laana yao ya kutotwaa taji. Kwa upande mwingine, kati ya mwaka 2002 na 2018, Cameroon ilifika katika kila hatua ya nusu fainali ya WAFCON. Safari hii, Indomitable Lionesses wamerudi katika mazingira waliyoyazoea na sasa ni miongoni mwa timu nne zilizofika nusu fainali.
Nusu Fainali ya Pili: Algeria vs Malawi
Algeria wamekuwa wakishiriki WAFCON mara kwa mara kwa miaka mingi, wakicheza katika matoleo matano kabla ya mwaka 2024. Katika toleo la mwaka 2025, walifanikiwa kuvuka hatua ya awali kwa mara ya kwanza lakini wakaishia robo fainali. Safari hii wameenda hatua moja zaidi kwa kufuzu nusu fainali, beki na kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali, Marine Dafeur, amekuwa mhimili muhimu wa timu hiyo.
Malawi wanashiriki WAFCON kwa mara ya kwanza katika historia yao. Kufika hatua hii kunamaanisha pia wamejihakikishia nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake kwa mara ya kwanza mwaka 2027, kama ilivyo kwa wapinzani wao wa nusu fainali. Aidha, wana nafasi halisi ya kuwania taji kubwa la Afrika.
Hitimisho

Mashindano ya WAFCON 2026 yamezidi kuonyesha nguvu ya uwekezaji na maandalizi ya vipaji barani Afrika. Timu 4 ambazo ni; Cameroon, Morocco, Malawi na Algeria zitavaana kusaka mbabe. Je ni timu zipi 2 zitakazofuzu hatua ya Fainali? Dakika 90 zitaamua, Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

