- Usajili na malengo ya msimu wa 2026/27 kwa Simba SC ni kutwaa makombe
- Kocha Mkuu, Steve Barker abainisha mipango kamili na kinachohitajika kwenye mechi za kitaifa na kimataifa
- Kelvin Nashon, Chilambo, Doumbia wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Msimbazi
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unakaribia kuanza huku usajili na malengo ya Simba SC 2026/27 ikiwa ni kutwaa ubingwa. Baada ya misimu mitano mfululizo kuisha wakishuhidia watani wao wa jadi Yanga SC wakijenga ufalme wao. Uongozi wa Msimbazi umeamua kufanya mabadiliko makubwa, kuanzia benchi la ufundi hadi usajili wa wachezaji wapya. Mashabiki wa Simba wanatamani kuona timu yao ikitawala tena soka la Tanzania na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Wachezaji waliosajiliwa Simba SC: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini

Maandalizi ya msimu huu yamekuwa yakifuatiliwa kwa karibu na wadau wa soka nchini. Kauli za viongozi wa Simba SC zimekuwa zikisisitiza kuwa hawajengi timu mpya bali wanaongeza nguvu kwenye kikosi kilichopo, ikimaanisha wanalenga kuimarisha maeneo mahususi kwa wachezaji wenye uzoefu na vipaji. Hii inaashiria mkakati wa makini wa kuunda kikosi chenye ushindani mkubwa.
Usajili wa nguvu: Nyuso mpya Msimbazi

Ratiba ya Simba SC: Ratiba ya Simba SC mechi 10 za msimu mpya 2026/27 : Ligi Kuu NBC , Takwimu |Kukutana na Yanga SC ‘Kariakoo Dabi’ Oktoba 10, 2026 | SportPesa Blog
Simba SC imefanya usajili wa wachezaji muhimu, ikilenga kuongeza ubora katika kila idara. Moja ya majina makubwa yaliyotua Msimbazi ni beki wa kati kutoka Ivory Coast, Serge Badjo mwenye umri wa miaka 23. Mshambuliaji Ibrahim Doumbia raia wa Mali naye ni ingizo jipya.
Mbali na Badjo, Simba pia imewatambulisha rasmi wachezaji chipukizi wenye vipaji, Nathaniel Chilambo na Kelvin Nashon. Nashon kiungo mkabaji ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa unyamani. Usajili wao unaonyesha dhamira ya klabu kuwekeza katika vipaji vya ndani na kuwajengea uzoefu wa kucheza timu kubwa.
Simba SC imefanikiwa kumuongezea mkataba wa mkopo nyota Neo Maema. Huyu alitarajiwa kurejea Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini. Amerejea kuendelea na msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Malengo makuu ya msimu wa 2026/27
Malengo ya Simba SC kwa msimu wa 2026/27 yameelezwa mara kwa mara na uongozi. Kipaumbele cha kwanza ni kurejesha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao umekuwa ukichukuliwa na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, kwa misimu kadhaa. Mashabiki wanatamani kuona kombe likirudi Msimbazi. Lengo lingine muhimu ni kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, hususan Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba imekuwa na rekodi nzuri ya kufika hatua za juu katika mashindano haya hapo awali. Ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2025 dhidi ya RS Berkane. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wametinga hatua ya robo fainali mara 7 sasa wanataka kuvuka hatua hiyo na kufikia fainali au hata kutwaa ubingwa. Usajili wa wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa unalenga kuimarisha kikosi kwa ajili ya changamoto hizo.
Klabu pia inalenga kuimarisha miundo mbinu yake na kuendeleza akademi ya vijana. Hii ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha Simba inakuwa na msingi imara wa wachezaji wake wa baadaye na kupunguza utegemezi wa usajili wa gharama kubwa kutoka nje.Mchakato huu unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Benchi la ufundi na mikakati mizito
Mafanikio ya timu yanategemea benchi la ufundi na Simba SC imefanya mabadiliko muhimu katika eneo hili. Kocha Mkuu ni Steve Barke ambaye alikuwa na kikosi msimu wa 2025/26. Huyu ni kocha anayeamini katika vipaji na mbinu za kumiliki mpira zaidi kwenye mechi za ushindani.
Msisitizo utakuwa katika nidhamu ya kimbinu, utimamu wa mwili, na uwezo wa wachezaji kuelewa na kutekeleza maelekezo ya kocha. Mazoezi ya pre-season yalifanyika Rwanda. Hapo walipata muda wa kucheza mechi 3 za ushindani kwenye Kagame Cup. Ushindi mechi 1 na sare mechi 2 wakiishia nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi.
Maoni ya Steve Barker
Kocha Mkuu Barker amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo ndani ya msimu mpya. Ameongeza kwamba wachezaji watakuwa na kazi kutafuta ushindi. Maandalizi waliyofanya yatawapa nguvu kuanza msimu mpya wakiwa na kasi.
“Tumekuwa na maandalizi mazuri kuelekea msimu mpya. Kuanza kwa kupoteza mchezo wetu wa Ngao ya Jamii ni somo kwetu. Pale mbapo kuna mapungufu tutafanyia kazi kuwa bora zaidi,”.
Ushindani na matarajio ya ligi kuu
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuwa na ushindani mkali msimu huu. Yanga SC wataendelea kuwa tishio kubwa, huku timu nyingine kama Azam FC, Singida Black Stars, Fountain Gate zikiwa na hesabu yakupata matokeo chanya. Hata hivyo, Simba SC imedhamiria kurejesha hadhi yake na kuonyesha ubora wake uwanjani.Msimu uliopita iliishia nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 73 tofauti ya pointi 2 na vinara Yanga SC waliokusanya pointi 75.
Mashabiki wa Simba wana matarajio makubwa kutoka kwa kikosi chao kipya. Wanaamini kuwa usajili uliofanywa na mikakati iliyowekwa itawawezesha kutwaa mataji yote ya ndani na kufanya vizuri kimataifa. Shinikizo ni kubwa, lakini uongozi na wachezaji wameonekana kuwa tayari kukabiliana nalo.
Changamoto na fursa
Kama ilivyo kwa kila msimu, Simba SC itakabiliana na changamoto mbalimbali. Majeraha ya wachezaji muhimu, uchovu wa mechi nyingi na ushindani mkali kutoka kwa wapinzani ni baadhi ya vikwazo vinavyoweza kujitokeza. Hata hivyo, klabu ina fursa ya kutumia uzoefu wake na ubora wa kikosi chake kipana kukabiliana na changamoto hizo.
Fursa nyingine ni kuendeleza vijana kutoka akademi na kuwapa nafasi ya kucheza katika timu ya wakubwa. Hii itasaidia kujenga msingi imara wa timu kwa miaka ijayo na kuhakikisha kuna mbadala wa kutosha kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza. Usimamizi mzuri wa rasilimali fedha pia utakuwa muhimu katika kufikia malengo.
Hitimisho
Simba SC imeingia msimu wa 2026/27 ikiwa na matumaini mapya na dhamira kubwa ya kufanya vizuri. Mchezo wa Ngao ya Jamii umewapa fuzo kufanyia maboresho kwenye mapungufu. Taji ambalo wanalitetea kwa sasa ni CRDB Federation Cup walilotwaa kwa ushindi wa bao 1-0 Azam FC kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Zanzibar.

