Ngao ya Jamii: Yanga SC vs Simba SC ni leo New Amaan Complex | Odds | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

August 12, 2026
Ratiba ya Yanga SCYanga SC ZanzibarYanga SC Zanzibar
  • Yanga SC vs Simba SC ni leo Ngao ya Jamii, Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:30 usiku
  • Seleman Mwalimu hatihati kuukosa mchezo huu dhidi ya mabosi wake wa zamani
  • Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema kuwa ana uzoefu wa miaka 25 na mechi ngumu hana presha
  • Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema anatambua ubora wa wapinzani wataingia kwa tahadhari

Yanga SC vs Simba SC ni leo Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:30 usiku mchezo huu mkali unatarajiwa kuchezwa. Ni mabingwa wa NBC Premier League 2025/26 Yanga SC vs Simba SC, mabingwa wa CRDB Federation Cup 2025/26.Mwanzo wa mchezo huu ni ishara ya ufunguzi pazia la ligi kwa msimu wa 2026/27.

Taarifa muhimu kuhusu Kariakoo Dabi: Yanga SC vs Simba SC Ngao ya Jamii: Kariakoo Derby, Matokeo, Ratiba, h2h, Habari za timu

Je, unataka kushinda na SportPesa?

Ni zamu yako kushinda leo Agosti 12,2026 kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC. SportPesa kuna odds ambazo zinakupa ushindi. Bashiri kwa ustaarabu.

Yanga SC vs Simba SC
Yanga SC vs Simba SC

Ngao ya Jamii: Yanga SC vs Simba SC ni leo Agosti 12,2026, maoni ya makocha

Yanga SC vs Simba SC ni leo
Clatous Chota Chama kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC ni leo Agosti 12,2026 katika visiwa vya Zanzibar. Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema licha ya kutokuwa na maandalizi ya kutosha kwa msimu mpya anaamini timu yake ina ubora wa kushinda mchezo dhidi ya Simba.

“Mashabiki watafurahi na watarajie soka safi kwa kuwa nina amini katika ubora wa wachezaji na mazoezi ambayo tumefanya. Kikubwa ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri na kushinda Ngao ya Jamii. Nina miaka 25 katika ukocha, sijawahi kusumbuliwa na presha ya mechi za aina hii, nina uzoefu wa kuhimili presha. Kikubwa ni soka safi na kupata matokeo mazuri,” amesema Mngqithi

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo dhidi ya Yanga SC. Steve ameongeza kuwa malengo ni kupata ushindi na kutwaa taji ya Ngao ya Jamii.

“Tunafahamu ubora wa Yanga, hivyo maandalizi yamejikita katika maeneo ya kiufundi, kimwili na kisaikolojia ili kuwa tayari kwa ushindani wa mchezo ujao ambao ni mgumu. Tunahitaji kuanza vizuri na kupata ushindi ili kutwaa Ngao ya Jamii. Wachezaji wapo tayari kuelekea kwenye mchezo wetu mgumu,”.

Seleman Mwalimu hatihati kuukosa mchezo

Selemani Mwalimu
Selemani Mwalimu, mshambuliaji wa Yanga SC

Soma hapa kuhusu Mwalimu: Ngao ya Jamii Yanga SC vs Simba SC: Selemani Mwalimu atua Zanzibar aanza mazoezi na Shalulile, Kariakoo Derby, Matokeo, Ratiba, h2h, Habari za timu

Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Seleman Mwalimu kuna hatihati kuukosa mchezo wa leo. Hii inatokana na kutokuwa na timu kweye maandalizi mwanzo wa msimu. Mwalimu ambaye yupo hapo kwa mkopo wa mwaka mmoja alianza mazoezi na Simba SC.

Licha ya Simba SC kumtambulisha kwenye Simba Day, Uwanja wa Uhuru Agosti 8,2026 hajajiunga na timu hiyo. Agosti 11,2026 alitambulishwa Yanga SC. Yupo hapo kwa mkopo akitokea Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Tayari ameshajiunga na Yanga SC kambini Zanzibar mapema Agosti 11,2026. Kuna uwezekano mdogo kuanza kikosi cha kwanza kwa sababu hakuwa na kikosi cha Yanga SC katika maandalizi. Hivyo kuanza ama kutokuanza itategemea maamuzi ya benchi la ufundi.

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC ni leo kwa wababe hawa kuanza hesabu kuusaka ubingwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 14. Katika mchezo uliopita 2025 walipokutana ni Wananchi walitwaa taji ya Ngao ya Jamii. Hawa wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kutetea taji lao.

.

Share this: