- Je Tuzo ya kiungo bora NBC Premier League 2024/25 nani kuitwaa? Majibu yatajulikana Arusha.
- Viungo bora wanawania tuzo hii Clatous Chama, Allen Okello, Pacome, Maxi na Fei Toto.
- Okello kwa sasa hayupo katika NBC Premier League wengine waliotajwa wanaendelea na maisha katika timu za Bongo

Swali kubwa kwa sasa ni kuhusu Tuzo ya kiungo bora NBC Premier League 2024/25 nani kuitwaa? Hii inatokana na ubora na uimara wa wachezaji wanaoshindanishwa katika eneo hilo.Ikumbukwe kwamba Novemba 11, 2026 taarifa rasmi ilitolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Cliford Ndimbo ikitaja tarehe na wachezaji wanaowania tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) za msimu wa 2025/2026 zitafanyika Disemba 12, 2026 Jijini Arusha Tanzania.Tuzo hizo zimejumuisha vipengele vitano ambapo jumla kategori zitakazotoa tuzo ni 38 na jumla watunukiwa ni 61.Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 tuzo hizo hazikufanyika hivyo zinarejea kwa mara nyingine tena.
SOMA HII PIA:Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) za msimu wa 2025/2026 | Orodha ya wachezaji | MVP
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1
Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

Je Tuzo ya kiungo bora NBC Premier League 2024/25 nani kuitwaa?
Kutokana na kila timu kuwa na viungo bora huku eneo hili likiwa msingi wa ushindi kila mmoja anasubiri kuona shujaa atakuwa nani.Kipengele hiki kinajumuisha wachezaji watano watatu wanatoka Yanga SC, Simba SC imetoa mchezaji mmoja sawa na Azam FC.Mzawa katika kipengele hiki ni Feisal Salum mali ya Azam FC.
Wanaowania tuzo ya kiungo bora
| Jina la Kiungo | Klabu | |
|---|---|---|
| 1 | Allan Okello | Yanga SC |
| 2 | Clatous Chama | Simba SC |
| 3 | Feisal Salum | Azam FC |
| 4 | Max Nzengeli | Yanga SC |
| 5 | Pacome Zouzua | Yanga SC |
Allan Okello raia wa Uganda anakumbukwa kwa umuhimu wake katika kufunga na kutengeneza nafasi za mwisho.Clatous Chama raia wa Zambia kwenye eneo la kiungo ni bora.Mazi Nzengeli na Pacome Zouzua hawa kutoka DR Congo katika kutuliza na kufunga wapo imara.Ubora wa kila mchezaji unaongeza ugumu wa kujua nani atatwaa tuzo katika eneo hili.
SOMA HII PIA:Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 mfululizo | Takwimu, matokeo | SportPesa Blog
Hitimisho
Tuzo ya kiungo bora NBC Premier League 2024/25 nani kuitwaa?Majibu yatakuwa wazi Jijini Arusha siku ya kilele cha tuzo.Wapo wachezaji ambao wanaendelea na maisha katika timu zao akiwemo Chama, Pacome,Maxi na Feisal huku Okello akiwa kwenye changamoto mpya.

