Simba SC vs Orlando Pirates Uwanja wa UhuruUwanja wa UhuruUwanja wa Uhuru

Simba SC vs Orlando Pirates Uwanja wa Uhuru
Simba SC vs Orlando Pirates kupigwa Uwanja wa Uhuru

Simba SC vs Orlando Pirates Uwanja wa Uhuru tiketi zina madaraja matatu

  • Kuelekea Simba SC vs Orlando Pirates  Uwanja wa Uhuru tiketi zina madaraja matatu na tayari zimeanza kuuzwa mtandaani.
  • Kampeni za hamasa kwa mashabiki zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 26, 2026 na mchezo utapigwa Jumapili Novemba 29,2026.
  • Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC amewaomba mashabiki kushambulia kwa wingi tiketi ili wakashuhudie mchezo wa kwanza kwa Kundi C.

Kuelekea pambano la Simba SC vs Orlando Pirates Uwanja wa Uhuru tiketi zina madaraja matatu kuwapa nafasi mashabiki kujitokeza kwa wingi.Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC amebainisha madaraja hayo kuwa ni mzunguko, VIP na Platinum.Pambano hili la hatua ya makundi CAF Champions League litapigwa saa 10:00, Novemba 28, 2026.

SOMA HII PIA:Ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27 | Kundi C | Msimamo | SportPesa Blog

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1

Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

image
 

Taarifa za tiketi na madaraja

Ahmed amesema ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huu kutokana na umuhimu wake. Amewaomba kuzishambulia tiketi mapema ambazo zinauzwa mtandaoni.Aidha ameongeza kuwa wachezaji wapo tayari kuanza safari kusaka tiketi ya kufuzu robo fainali.

“Tuna madaraja matatu kwenye tiketi hizi na malengo ni kuona kila Mwanasimba anapata fursa yakuja uwanjani.Mzunguko 7,000, VIP 40,000, Platinum ni 200,000.Tiketi zote zinapatikana mtandaoni,”.

Namna yakuzipata kupitia : https://simbasc.wanaut.com

SOMA HII PIA:Simba SC vs Orlando Pirates CAF Champions League 2026/27 | H2H | Live score

Umuhimu wa mchezo dhidi ya Orlando Pirates

Mchezo huu dhidi ya Orlando Pirates ni muhimu sana kwa Simba SC katika kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ushindi nyumbani utawapa Wekundu wa Msimbazi nafasi nzuri ya kuanza vizuri hatua ya makundi na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Uwepo wa mashabiki wengi uwanjani unaweza kuwa chachu kubwa kwa wachezaji wa Simba SC, na kuwapa nguvu ya ziada ya kupambana na wapinzani wao kutoka Afrika Kusini.

Hitimisho

Simba SC vs Orlando Pirates Uwanja wa Uhuru tiketi zina madaraja matatu na tayari zimeanza kuuzwa.Kwa atakayenunua tiketi ya Platinum atapewa jezi mpya ya Simba SC, chakula na vinywaji, tiketi ya VIP A usafiri kutoka Serena.Novemba 26, 2026 uzinduzi wa hamasa unatarajiwa kufanyika tawi la Simba, Jangwani Mafuso.

Share this: