- Spain vs Belgium FIFA Kombe la Dunia 2026, ni mchezo mkali wa Robo Fainali unaotarajiwa kupigwa 10 July 2026, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Los Angles, huko nchini Marekani.
- Spain inayoongozwa na mastaa Lamine Yamal na Mikel Oyarzabal watavaana na Belgium ya Romelo Lukaku na Jeremy Doku katika vita ya kuisaka Nusu Fainali.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Baada ya kuiondosha timu ngumu ya Portugal katika hatua ya 16 bora, kikosi cha Spain kitashuka tena usiku wa kesho Ijumaa, kuvaana na Belgium katika mchezo mkali wa robo fainali ya FIFA Kombe la Dunia 2026. Mechi hii itapigwa saa nne usiku wa kesho Ijumaa 10 July 2026, katika Uwanja wa Los Angeles nchini Marekani. Huu ni miongoni mwa mechi zinazokutanisha mastaa wakubwa kama, Kelvin De Bryne na Jeremy Doku, Lamine Yamal na Mikel Oyarzabal. Hapa tunachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Spain vs Belgium
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Mchezo huu ni wa hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Ni mechi ya mtoano ambapo hakuna nafasi ya kurekebisha makosa; mshindi atajihakikishia tiketi ya kucheza Nusu Fainali, huku timu itakayoshindwa ikimaliza safari yake kwenye mashindano. |
| Tarehe na Muda | Pambano hili litachezwa Ijumaa, 10 Julai 2026, kuanzia saa 4:00 usiku (EAT). |
| Uwanja | Mechi itafanyika katika Uwanja wa Los Angeles, nchini Marekani. Uwanja huu ni miongoni mwa viwanja vinavyotumika kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2026, ukiwa na miundombinu ya kisasa na uwezo wa kuandaa mechi za kiwango cha juu za kimataifa. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 4 ZA HATUA YA ROBO FAINALI, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 Robo Fainali | Mechi zote 4 | Utabiri | Odds kubwa | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa Spain vs Belgium FIFA Kombe la Dunia 2026

Spain watakutana na Ubelgiji katika robo fainali ya pili ya Kombe la Dunia 2026, itakayochezwa Ijumaa jijini Los Angeles kwenye Uwanja wa Los Angeles. Mshindi wa mchezo huu atafuzu nusu fainali, ambako atakutana na mshindi kati ya Ufaransa na Morocco. Mpaka sasa kwenye mashindano haya, kikosi cha Luis de la Fuente kiliongoza Kundi H kabla ya kuifunga Austria kirahisi katika hatua ya 32 Bora, kisha kikaiondoa Ureno katika hatua ya 16 Bora.
Nguvu kubwa ya Hispania imekuwa safu yake ya ulinzi. Hadi sasa ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu bao lolote katika michuano hii. Wameweka rekodi ya kucheza mechi sita mfululizo za Kombe la Dunia bila kuruhusu bao, sawa na zaidi ya saa 10 za mchezo. Historia inaibeba Hispania, kwani tangu walipopoteza dhidi ya Ubelgiji kwenye Euro 1980, La Roja wameshinda mechi tisa kati ya 11 walizokutana na Belgium.
Kwa Ubelgiji katika mashindano haya, waliongoza Kundi G licha ya kutocheza kwa kiwango cha kuvutia sana, kabla ya kuiondoa Senegal kwa ushindi wa mabao 3-2 katika hatua ya 32 Bora. Licha ya Kocha Rudi Garcia, kukosolewa sana kwa kufanya uamuzi wa kushangaza wa kuwaanzisha benchi Kevin De Bruyne, Jeremy Doku na mfungaji bora wa muda wote wa Ubelgiji Romelu Lukaku dhidi ya Marekani. Timu hiyo ilifanikiwa kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 4-1.
Habari za timu na majeruhi
Kwa Spain, Nico Williams bado hajarejea katika kiwango chake bora baada ya kuuguza jeraha la msuli wa paja, hivyo anatarajiwa kuanza benchi. Kwa upande wa Ubelgiji, imepata pigo baada ya Amadou Onana kupata jeraha la ACL litakalomuweka nje ya mashindano. Romelu Lukaku anatarajiwa kuendelea kuanzia benchi licha ya kufunga bao lake la 93 akiwa na timu ya taifa katika mchezo uliopita.
Vikosi Vinavyotarajiwa
Hispania:
| Nafasi | Mchezaji | Maelezo |
|---|---|---|
| Kipa | Unai Simón | Kipa namba moja wa Hispania anayejulikana kwa utulivu, uwezo wa kuokoa hatari na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma. |
| Beki wa Kulia | Pedro Porro | Beki mwenye kasi anayechangia katika ulinzi na kushambulia kupitia upande wa kulia. |
| Beki wa Kati | Pau Cubarsí | Kijana mwenye kipaji anayesoma mchezo vizuri na kusaidia kujenga mashambulizi kutoka safu ya ulinzi. |
| Beki wa Kati | Aymeric Laporte | Beki mwenye uzoefu mkubwa anayetoa uimara katika safu ya nyuma na uongozi ndani ya kikosi. |
| Beki wa Kushoto | Marc Cucurella | Huchangia kwa nguvu katika ulinzi na hupanda mara kwa mara kusaidia mashambulizi ya Hispania. |
| Kiungo | Rodri | Kiungo wa ulinzi anayesimamia mzunguko wa mpira, kukaba na kudhibiti kasi ya mchezo. |
| Kiungo | Pedri | Kiungo mbunifu anayejulikana kwa pasi sahihi, umiliki mzuri wa mpira na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao. |
| Kiungo wa Kushambulia | Lamine Yamal | Winga mwenye kasi na mbinu za hali ya juu anayesumbua mabeki kwa chenga na uwezo wa kutengeneza nafasi. |
| Kiungo wa Kushambulia | Dani Olmo | Mchezaji mbunifu anayesaidia kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji pamoja na kutengeneza mabao. |
| Kiungo wa Kushambulia | Álex Baena | Hutoa ubunifu, pasi za mwisho na uwezo wa kupenya kupitia pembeni au katikati ya uwanja. |
| Mshambuliaji | Mikel Oyarzabal | Anaongoza safu ya ushambuliaji kwa harakati zake nyingi, umaliziaji mzuri na uwezo wa kufunga mabao katika nyakati muhimu. |
Ubelgiji

| Nafasi | Mchezaji | Maelezo |
|---|---|---|
| Kipa | Thibaut Courtois | Kipa mwenye uzoefu mkubwa anayetarajiwa kuwa nguzo muhimu kwa kuokoa hatari na kuiongoza safu ya ulinzi ya Ubelgiji. |
| Beki wa Kulia | Timothy Castagne | Hutoa mchango mkubwa katika ulinzi na pia hupanda kusaidia mashambulizi kupitia pembeni. |
| Beki wa Kati | Nathan Ngoy | Anategemewa kutumia nguvu na uwezo wake wa kusoma mchezo kuzuia mashambulizi ya wapinzani. |
| Beki wa Kati | Brandon Mechele | Beki mwenye utulivu na uwezo mzuri wa kuondoa hatari ndani ya eneo la penalti. |
| Beki wa Kushoto | Maxim De Cuyper | Huchangia ulinzi pamoja na kusaidia mashambulizi kupitia upande wa kushoto. |
| Kiungo | Hans Vanaken | Kiungo mwenye uwezo wa kutawala mpira na kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji. |
| Kiungo | Youri Tielemans | Mchezaji muhimu katika kupanga mashambulizi na kudhibiti kasi ya mchezo katikati ya uwanja. |
| Kiungo wa Kushambulia | Dodi Lukebakio | Hutoa kasi na ubunifu kwenye mashambulizi, akitengeneza nafasi na kutishia lango la wapinzani. |
| Kiungo wa Kushambulia | Kevin De Bruyne | Nyota wa timu anayesifika kwa pasi za mwisho, ubunifu na uwezo wa kuamua matokeo ya mechi. |
| Kiungo wa Kushambulia | Leandro Trossard | Huchangia kwa kasi, chenga na uwezo wa kufunga au kutengeneza mabao kutoka pembeni. |
KUANGALIA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA ENGLAND, SOMA HII: Prediction Norway vs England FIFA Kombe la Dunia 2026: Robo fainali, taarifa kuhusu mechi, odds, h2h
Utabiri Wetu (Ushindi kwa Spain)
Huenda mchezo huu ukawa wa ushindani mkubwa zaidi kuliko burudani, kwani Hispania hupendelea kumiliki mpira na kuwazuia wapinzani kupata nafasi kwa kuwabana muda wote. Ni wazi Ubelgiji watatumia sehemu kubwa ya mchezo huu kuzuia wasiruhusu bao, na kushambulia kwa kushtukiza japo huo utakuwa mtihani mgumu kwao. Kwa kuzingatia uchambuzi wa kitaalamu wa ubora wa vikosi, na rekodi za michuano iliyopita tunatabiri licha ya Mchezo mgumu, Spain wataibuka na ushindi. Haya ni maoni ya kiuhalili na sio matokeo halisi, hivyo Bashiri kistaarabu.
Hitimisho

Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaonyesha tunatarajia mchezo mgumu sana, lakini Spain wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi. Zingatia kuwa Ubashiri wetu nimaoni ya kiuhariri sio matokeo halisi hivyo chambua mkeka wako na ubashiri kistaarabu. Licha ya matarajio hayo, pia inatarajiwa mchezo utakuwa mgumu, fuatilia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.
KUJUA KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA FRANCE, SOMA HII: Prediction Ufaransa vs Morocco FIFA Kombe la Dunia 2026: Robo fainali, H2H, odds, taarifa muhimu

