FIFA Kombe la Dunia ---- Robo FainaliFIFA Kombe la Dunia ---- Robo Fainali
  • Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 robo Fainali inatarajia kuanza rasmi leo Alhamisi 9 July 2026, hii ni baada ya kumalizika kwa hatua ya 16 bora.
  • Mechi ya kwanza ya hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kuwakutanisha France vs Morocco leo saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Ikumbukwe toleo la Kombe la Dunia la FIFA 2026 limeandaliwa kwa ushirikiano wa nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico.
  • Mechi 4 zitapigwa baina ya timu 8 zilizofuzu kutoka hatua ya 16 bora ya mwaka huu, ambazo ni: Morocco, Norway, France, England, Belgium, Argentina, Switzerland na Spain, makala hii inakuletea ratiba ya mechi zote 4 zitakazochezwa, muda zitakapochezwa na viwanja vitakavyotumika na utabiri.

Ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026 robo fainali itaanza kutimua vumbi rasmi leo Alhamisi 9 July 2026, mechi ya kwanza ikiwa ni France vs Morocco itakayopigwa saa 5 usiku. Haya ni mashindano makubwa zaidi ya soka duniani, ambayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na mwaka huu Kombe la Dunia litafanyika kwa ushirikiano wa maandalizi ya nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico. Timu 8 zimefuzu na zinatarajia kuvaana hatua ya robo Fainali ambazo ni: Morocco, Norway, France, England, Belgium, Argentina, Switzerland na Spain. Makala hii inakuletea ratiba ya mechi zote 4 zitakazochezwa katika hatua ya robo fainali ya mashindano haya, utabiri, muda zitakapochezwa na viwanja vitakavyotumika.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa. Unaweza kuwea ubashiri wako moja kwa moja kwa kubonyeza mchanganuo wa odds kubwa chini ya kila picha.

Kuhusu mechi za FIFA Kombe la Dunia 2026 robo fainali

Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 Robo Fainali
Ratiba ya Robo Fainali

Robo fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 inatarajiwa kuanza kwa kishindo leo Alhamisi 9 July 2026, kwa mechi kali na kubwa ya France vs Morocco. Ratiba hii itaendelea kwa michezo mikubwa, inayotarajiwa kupigwa kuendana na kalenda yao. Hatua hii inahusisha sehemu kubwa ya mataifa yenye nguvu, na ubora mkubwa kisoka ambayo yamefuzu hatua hiyo, lakini pia yapo mataifa ambayo yameshangaza wengi ikiwemo Norway.

Mpaka sasa, baadhi ya vigogo wa soka duniani wameondolewa, huku timu zilizokuwa hazipewi nafasi kubwa kama Cape Verde zikiwa kivutio kikubwa. Morocco ndiyo timu pekee kutoka Afrika iliyobaki kwenye mashindano baada ya Argentina kuiondoa Misri katika hatua ya 16 Bora. Hatua ya robo fainali inahusisha timu moja kutoka Afrika, timu sita kutoka Ulaya na timu moja kutoka Amerika Kusini.

KUSOMA KUMBUKUMBU YA RATIBA YA 16 BORA, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora | Mechi zote 8 | Utabiri | Odds kubwa | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Morocco vs Ufaransa (9 July 2026 saa 5 usiku EAT)

FIFA Kombe la Dunia 2026 robo Fainali
France vs Morocco
FRANCE vs MOROCCO -
FRANCE vs MOROCCO

Ufaransa inaingia kwenye mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Boston, USA ikipewa nafasi kubwa ya ushindi, lakini Morocco imesisitiza kuwa lengo lao ni kutwaa ubingwa wa dunia. Morocco iko hatarini kumkosa mfungaji wake bora, Ismael Saibari, ambaye amefunga mabao matatu kutokana na jeraha. Ufaransa ina safu kali ya ushambuliaji ikiongozwa na nahodha Kylian Mbappé, aliyefunga mabao saba kati ya 14 ya timu yake kwenye mashindano haya.

Aidha, Michael Olise ndiye kinara wa pasi za mabao akiwa nazo tano, huku mshindi wa Ballon d’Or Ousmane Dembélé akifunga mabao manne. Katika hatua ya makundi, Les Bleus walikusanya alama zote tisa kwa kuzifunga Senegal (3-1), Iraq (3-0) na Norway (4-1). Baadaye waliifunga Sweden mabao 3-0 kabla ya kuiondoa Paraguay, kwa ushindi mwembamba wa 1-0 katika mchezo mgumu wa hatua ya 16 Bora.

Morocco nayo ilipitia safari ngumu. Ilianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Brazil, ikaifunga Scotland 1-0 na Haiti 4-2. Baadaye iliiondoa Uholanzi kwa mikwaju ya penalty, kabla ya kuwafunga wenyeji Canada mabao 3-0 katika hatua ya 16 Bora. Licha ya safari tofauti walizopitia, timu zote zina lengo moja ambalo ni kufuzu nusu fainali. Morocco pia inataka kulipiza kisasi cha kufungwa 2-0 na Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na mshindi wa Mchezo huu atakutana na mshindi wa mechi ya Spain vs Belgium.

Vikosi vinavyotarajiwa

Ufaransa:

Maignan, Kounde, Upamecano, Saliba, Digne; Kone, Rabiot; Olise, Dembélé, Barcola; Mbappé.

Morocco:

Bounou; Hakimi, Diop, Halhal, Mazraoui; Bouaddi, El Aynaoui; Diaz, Ounahi, El Khannouss; Rahimi.

KUSOMA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA MOROCCO, SOMA HII: Prediction Ufaransa vs Morocco FIFA Kombe la Dunia 2026: Robo fainali, H2H, odds, taarifa muhimu

Spain vs Belgium (10 July 2026 saa 4 usiku EAT)

Spain vs Belgium
Spain vs Belgium
Spain vs Belgium -
Spain vs Belgium

Spain wanaingia Uwanja wa os Angles wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya ushindi, lakini Ubelgiji imeendelea kuimarika kadri mashindano yalivyoendelea. Hispania imefika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2010. Hatua ya 32 bora Spain waliifunga Austria 3-0 kabla ya kuiondoa Ureno kwa ushindi wa 1-0 kwenye 16 bora, Ubelgiji wao waliiondoa Senegal kwa mabao 3-2, kisha wakaifunga Marekani 4-1.

Vikosi vinavyotarajiwa

Hispania:

Unai Simón; Porro, Cubarsí, Laporte, Cucurella; Rodri, Pedri; Lamine Yamal, Dani Olmo, Baena; Oyarzabal.

Ubelgiji:

Courtois; Castagne, Mechele, Ngoy, De Cuyper; Tielemans, Raskin, Vanaken; Lukebakio, De Ketelaere, Trossard.

Norway vs England (12 July 2026 saa 6 usiku EAT)

Norway vs England
Norway vs England
England vs Norway -
England vs Norway

England inapewa nafasi kubwa ya kushinda kweny Mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Miami, lakini Norway sio wa kubeza. Hii ni baada ya kuandika historia, kwa kufika robo fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuiondoa Brazil kwa mabao 2-0. Norway ilimaliza ya pili katika kundi nyuma ya Ufaransa kabla ya kuziondoa Côte d’Ivoire na Brazil. England iliongoza kundi lake, ikaiondoa DR Congo 2-1 na baadaye kuifunga Mexico 3-2 katika moja ya mechi bora za mashindano hatua ya 16 bora.

Vikosi vinavyotarajiwa

Norway:

Nyland; Ryerson, Ajer, Heggem, Moller Wolfe; Berg, Berge, Ødegaard; Sørloth, Haaland, Nusa.

England:

Pickford; Konsa, Stones, Guéhi, O’Reilly; Rice, Anderson; Saka, Bellingham, Gordon; Kane.

KUSOMA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA ENGLAND, SOMA HII: Prediction Norway vs England FIFA Kombe la Dunia 2026: Robo fainali, taarifa kuhusu mechi, odds, h2h

Argentina vs Uswisi (12 July 2026 saa 10 alfajiri)

Argentina vs Switzerland
Argentina vs Switzerland
Argentina vs Switzerland -
Argentina vs Switzerland

Mabingwa watetezi Argentina wanaingia kwenye robo fainali baada ya ushindi wa kihistoria wa mabao 3-2 dhidi ya Misri, wakitoka nyuma 2-0 hadi dakika ya 78. Lionel Messi aliiongoza tena Argentina kwa kufunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao, Mpaka sasa ana mabao 8 pamoja na pasi 2 za mabao katika mashindano haya. Kabla ya kuifunga Misri, Argentina iliifunga Cape Verde mabao 3-2 katika mchezo mgumu.

Uswisi ilifika robo fainali baada ya kuiondoa Colombia kwa mikwaju ya penalti na kabla ya hapo kuifunga Algeria 2-0 kwenye hatua ya 32 bora. Hii ni robo fainali ya kwanza kwa Uswisi tangu mwaka 1954. Kocha wa Uswisi Murat Yakin anaamini timu yake inaweza kuiondoa Argentina.

Vikosi vinavyotarajiwa

Argentina:

Emiliano Martínez; Molina, Romero, Lisandro Martínez, Medina; Paredes; De Paul, Enzo Fernández, Mac Allister; Messi, Julián Álvarez.

Uswisi:

Kobel; Zakaria, Elvedi, Akanji, Rodríguez; Jashari, Xhaka, Freuler; Ndoye, Embolo, Rieder.

Hitimisho

Ratiba kamili ya robo fainali ya FIFA Kombe la Dunia 2026 ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wote. Kwa mashabiki wengi, ratiba hii inaonekana kuwa ingekuwa ya kuvutia sana kama mastaa wakubwa kama, Cristiano Ronaldo na Neymar wangefuzu lakini tayari wametolewa. Tusubiri na kuona vita itakayojiri katika hatua hii, na kujua nani anakwenda usu Fainali.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.