- Wababe Mexico vs Ecuador FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 32 bora watakutana kusaka mshindi atakayetinga 16 bora
- Julai Mosi 2026, saa 10:00 alfajiri kwa Afrika Mashariki, Uwanja wa Mexico City
- SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi kuelekea mchezo huo muhimu, takwimu na h2h
Ni Mexico vs Ecuador FIFA Kombe la Dunia 2026 wanakutana katika Raundi ya 32. Mchezo utachezwa Uwanja wa Mexico City, huku kikosi cha Javier Aguirre kikiendelea na kampeni bora ya Kombe la Dunia wakiwa nyumbani.Julai Mosi,2026 saa 10:00 alfajiri saa za Afrika Mashariki.
Isome ratiba kamili ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mechi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Mexico vs Ecuador angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kwa uwajibikaji.

Taarifa za mechi
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | FIFA Kombe la Dunia 2026 |
| Mechi | Mexico vs Ecuador |
| Tarehe | Julai 1, 2026 |
| Uwanja | Uwanja wa Mexico City |
| Hatua | 32 bora |
| Muda | Saa 10:00 alfajiri (EAT) |
| Jukwaa la kubashiri | SportPesa |
Safari ya Mexico hatua ya makundi
- Mexico vs Afrika Kusini: Ushindi wa 2-0 katika mchezo wa ufunguzi.
- Mexico vs Korea Kusini: Ushindi wa 1-0, ukionyesha nidhamu ya kiulinzi.
- Mexico vs Jamhuri ya Czech: Ushindi wa 3-0.
Mexico wameonyesha uwiano wa ubora wa kushambulia na nidhamu ya kiulinzi, jambo linalowafanya kuwa miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kuendelea katika mashindano haya. Mexico wamekuwa na safu ya ushambuliaji yenye nguvu ikiongozwa na Raúl Jiménez na Julián Quiñones, huku César Montes na Johan Vásquez wakisimamia ulinzi ambao haujaruhusu bao lolote katika mashindano haya.
Wakiwa na zaidi ya mashabiki 80,000 wenye shauku kubwa, kikosi cha Javier Aguirre kinatarajiwa tena kudhibiti mpira na kushambulia kwa presha ya juu tangu dakika ya kwanza.
Kwa upande wa Ecuador, wanawasili wakiwa na imani kubwa baada ya kufanya moja ya maajabu makubwa ya hatua ya makundi. Kikosi cha Sebastián Beccacece kilipindua matokeo na kuishinda Ujerumani kwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa kundi, matokeo yaliyowapa tiketi ya kufuzu kama moja ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu.
Ecuador walipitia mwanzo mgumu baada ya kupoteza kwa taabu dhidi ya Ivory Coast na kisha kutoka sare tasa ya kukatisha tamaa dhidi ya Curaçao licha ya kutengeneza nafasi nyingi.
Hata hivyo, walionyesha ari kubwa waliposhinda Ujerumani kwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa kundi. Nilson Angulo alisawazisha bao la Leroy Sané kabla ya Gonzalo Plata kufunga goli la ushindi, jambo lililoonyesha ustahimilivu na tishio lao la kushambulia.
Kwa sasa, Enner Valencia anaendelea kuwa silaha kubwa ya kushambulia kwa Ecuador, akikaribia kufikisha mabao 50 ya kimataifa, huku Moisés Caicedo akiendesha mchezo katikati ya uwanja kwa nidhamu na ubunifu.
Habari za kikosi cha Mexico

- Raúl Jiménez anatarajiwa kurejea baada ya kupumzishwa kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
- Raúl Rangel ataendelea kusimama langoni.
- Safu ya ulinzi: Jorge Sánchez, César Montes, Johan Vásquez na Jesús Gallardo.
- Kiungo: Érik Lira, Luis Romo na Marcel Ruiz.
- Mashambulizi: Julián Quiñones na Roberto Alvarado watamuunga mkono Jiménez mbele.
Habari za vikosi
Mexico
- Kikosi kipo kamili bila majeraha.
- Javier Aguirre anatarajiwa kumrejesha Raúl Jiménez baada ya kupumzishwa kwenye mchezo wa mwisho wa makundi.
- Raúl Rangel ataendelea kusimama langoni.
- Safu ya ulinzi: Jorge Sánchez, César Montes, Johan Vásquez, Jesús Gallardo.
- Kiungo: Érik Lira, Luis Romo, Gutiérrez.
- Mashambulizi: Roberto Alvarado, Jiménez, Julián Quiñones.
Ecuador
- Hakuna majeraha makubwa.
- Sebastián Beccacece anatarajiwa kuendelea na kikosi kilichoshinda dhidi ya Ujerumani.
- Gonzalo Plata na Nilson Angulo wataendelea baada ya kiwango kizuri.
- Enner Valencia ataongoza safu ya ushambuliaji.
- Kiungo: Moisés Caicedo ndiye injini ya katikati.
- Ulinzi: Willian Pacho na Piero Hincapié katikati ya safu ya nyuma.
Vikosi vinavyotarajiwa Mexico vs Ecuador
- Mexico XI: Rangel; Sánchez, Montes, Vásquez, Gallardo; Lira, Romo, Gutiérrez; Alvarado, Jiménez, Quiñones
- Ecuador XI: Galíndez; Franco, Ordóñez, Pacho, Hincapié; Yeboah, Caicedo, Vite, Angulo; Plata, Valencia
Mexico wanaingia hatua ya mtoano wakiwa na fomu bora kabisa, wakishinda mechi zao zote sita zilizopita katika mashindano mbalimbali na kuweka clean sheets katika michezo yote mitatu ya makundi ya Kombe la Dunia. Hii inaonyesha uwiano wa ulinzi imara na ufanisi wa kushambulia.
Kwa upande wa Ecuador, wanawasili wakiwa na morali baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya Ujerumani. Ingawa safari yao ya kufuzu Raundi ya 32 haikuwa rahisi, wameonyesha ustahimilivu, nidhamu ya kiufundi na uwezo wa kuumiza wapinzani wakubwa kupitia mashambulizi ya kushtukiza.
Prediction Mexico vs Ecuador
Kwa mujibu wa Opta Analyst amechambua kwamba Mexico atapata ushindi. Asilimia 46.4 amepewa Mexico huku Ecuador akipewa asilimia 24.4. Huu ni mchezo ambao mshindi lazima apatikane ikishindikana dakika 90 muda wa nyongeza. Matokeo yanaweza kuwa Mexico 3-0 Ecuado, haya ni maoni ya mhariri sio matokeo kamili.

H2H Mexico vs Ecuador
| Kipengele | Mexico | Ecuador |
| Mechi Zilizochezwa | 16 | 16 |
| Ushindi | 8 | 3 |
| Sare | 5 | 5 |
| Magoli Yaliyofungwa | 25 | 18 |
Mechi za hivi karibuni Mexico vs Ecuador
| Tarehe | Mashindano | Matokeo | |||
| Oktoba 15, 2025 | Kirafiki | Mexico 1–1 Ecuador | |||
| Julai 01, 2024 | Copa América | Mexico 0–0 Ecuador | |||
| Juni 05, 2022 | Kirafiki | Mexico 0–0 Ecuador | |||
| Oktoba 28, 2021 | Kirafiki | Mexico 2–3 Ecuador | |||
| Juni 09, 2019 | Kirafiki | Mexico 3–2 Ecuador | |||
Ujerumani vs Paraguay h2h zisome rekodi: Prediction Ujerumani vs Paraguay FIFA Kombe la Dunia 2026: Knockout, team news, h2h, odds
Jinsi ya Kubashiri kwenye SportPesa
Fungua ukurasa wa tukio la Mexico vs Ecuador kwenye SportPesa.
Chagua soko lako — Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB) mara tu mechi itakapoanza.
Weka dau lako na thibitisha ubashiri.

