Haiti vs Scotland Kombe la Dunia 2026: Utabiri, muda, h2h na vikosi | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

June 13, 2026
Haiti vs Scotland FIFA Kombe la Dunia 2026Haiti vs Scotland FIFAHaiti vs Scotland FIFA
  • Pambano kali la Haiti vs Scotland FIFA Kombe la Dunia 2026 linasubiriwa kwa shauku ikiwa ni rekodi mpya inakwenda kuandikwa.
  • Haiti imerejea kwenye mashindano haya makubwa baada ya kupita miaka 52 na wapinzani wao Scotland wanarejea baada ya miaka 28.
  • SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi wa mchezo, takwimu muhimu na mfumo wa timu zote mbili.

Haiti vs Scotland FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mechi ya Kundi C itakayochezwa Uwanja wa Boston. Mchezo huu utawakutanisha Haiti ambayo imerejea Kombe la Dunia baada ya miaka 52 dhidi ya Scotland ambayo inarudi kwenye mashindano baada ya miaka 28. SportPesa Blog inakuletea utabiri, muda wa mechi, H2H, taarifa za vikosi, wachezaji muhimu na nafasi za kila timu kupata matokeo, Juni 14, 2026.

SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026.Kwa mechi ya Haiti vs Scotland angalia odds, linganisha fomu ya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa kwa kubonyeza picha iliyopo chini. Beti kwa uwajibikaji.

Haiti-vs-Scotland-Blog-jpg
Haiti vs Scotland

SOMA HII: Ratiba ya Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mabingwa watetezi kikosi | Takwimu | SportPesa Blog

Jedwali la Taarifa za Mechi

KipengeleMaelezo
MechiHaiti 🇭🇹 vs Scotland
MashindanoFIFA Kombe la Dunia 2026
KundiKundi C
HatuaHatua ya Makundi
Tarehe14 Juni 2026
UwanjaBoston Stadium
MjiBoston, Marekani
Muda wa KuanzaSaa 4:00 Usiku (E.A.T)
Jukwaa la KubetiSportPesa

Haiti vs Scotland FIFA Kombe la Dunia 2026 utabiri unasemaje?

Haiti vs Scotland FIFA Kombe la Dunia 2026
Scotland. Source: SI

Timu hizi mbili Haiti vs Scotland zinakutana kwenye Kombe la Dunia 2026 wakiwa wamepitisha miaka zaidi ya 20 bila kushiriki mashindano haya makubwa. Haiti imerejea katika fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 52. Scotland ikirudi tena kwenye mashindano hayo baada ya kusubiri kwa muda wa miaka 28. Timu zote mbili zitakuwa na lengo moja tu kuanza kampeni yao kwa ushindi na kujikusanyia pointi tatu muhimu.

Utabiri wa Haiti vs Scotland unaonyesha mchezo wenye ushindani mkubwa kwa sababu timu hizi mbili zinarejea Kombe la Dunia baada ya muda mrefu, Haiti inaweza kutegemea kasi ya mashambulizi ya kushtukiza. Scotaland ina uzoefu zaidi kwenye eneo la mabeki na viungo.Matokeo yanayoweza kutokea ni magoli machache huku sare au ushindi mwembaba kwa upande wowote ukiwa na nafasi kubwa.

H2H

Rekodi zinaonyesha kuwa Haiti vs Scotland hawajawahi kukutana kwenye mechi za ushindani. Hivyo wanakwenda kukutana kwa mara ya kwanza katika FIFA Kombe la Dunia 2026.

Taarifa kuhusu Haiti

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Haiti, Sébastien Migné, anatarajiwa kukiongoza kikosi chake chenye wachezaji 26 kusaka ushindi. Huyu anapenda kuamini mfumo wa 4-4-2. Hivyo atawakakabili Scotland akitumia washambuliaji wawili.

Habari njema kwa mashabiki wa Haiti ni kwamba kiungo Jean-Ricner Bellegarde anaendelea kuimarika kiafya. Ikumbukwe kwamba alikuwa na changamoto za majeraha. Kutokana na kuwa imara anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza mchezo huo.

Hata hivyo, Haiti imekuwa na matokeo ya mchanganyiko katika mechi zake za hivi karibuni za ushindani. Ilipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Tunisia, ikalazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Iceland. Timu hiyo ilipokea kichapo cha magoli 2-1 kutoka Peru.

Taarifa kuhusu Scotland

WhatsApp Image ---------- at --------
Twenzetu Duniani, Odds za uhakika

SOMA HII: Australia vs Turkey FIFA Kombe la Dunia 2026, h2h, Utabiri kundi D | SportPesa Blog

Kwa upande wa Scotland, Kocha Mkuu Steve Clarke anatarajiwa kukiongoza kikosi chake chenye uzoefu mkubwa. Timu hiyo ilisubiri miaka 28 kurejea kwenye FIFA Kombe la Dunia 2026. Ina nyota wengi akiwemo kiungo Scott McTominay.

McTominay amerejea katika kiwango kizuri baada ya kuugua maumivu ya tumbo yaliyokuwa yakimkabili katika siku za hivi karibuni. Tayari ameimarika jambo linaloongeza nguvu katika safu ya kati ya Scotland. Katika mchezo wake wa mwisho wa kirafiki, Scotland ilipoteza kwa 1-0 dhidi ya Japan, lakini timu hiyo imeonyesha uimara mkubwa katika safu ya ushambuliaji kwenye mechi zake za ushindani.

Haiti kikosi kinachotarajiwa kuanza

Placide; Arcus, Ade, Delcroix, Expérience; Jean Jacques, Bellegarde, Providence, Isidor; Nazon. Hiki sio kikosi halisi ni makisio. Kikosi kamili kitatangazwa muda mfupi kabla ya mchezo husika.

Scotland kikosi kinachotarajiwa kuanza

Gunn; Hickey, Hanley, Souttar, Robertson; Doak, McTominay, Ferguson, McGinn; Adams, Shankland. Hiki ni kikosi kinachotarajiwa na sio rasmi. Kikosi halisi kitatolewa muda mfupi kabla ya mchezo siku husika.

Hitimisho

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na kiu ya kila timu kutaka kuanza vyema kampeni yake ya Kombe la Dunia. Haiti itakuwa ikitafuta kuandika historia mpya baada ya kurejea kwenye mashindano haya makubwa, huku Scotland ikitaka kuthibitisha kuwa kurejea kwake baada ya miaka 28 si kwa bahati mbaya. Mashabiki wa soka duniani wanasubiri kwa shauku na wana fursa yakuvuna mamilioni kupitia SportPesa kwa kusuka mkeka na kumbuka Beti kwa uwajibikaji.

Share this: